Naona kijana anaanza kuchemka sasa!

Nina mambo ya kukuweka sawa Bwana ndogo Kabwe.Kwanza sijafurahia na ULEVI wako wa umaarufu wa muda mfupi tuliokupa wakati ukitetea maslahi ya TAIFA,tulijua umaarufu huo ungejenga na kuimarisha chama na mapambano makali dhidi ya ufisadi.
MOSI:Heshima hujengwa kwa miaka lakini hubomoka ndani ya sekunde moja,kwa hiyo Zitto mapambano tuliyoyaona ya kizalendo na kukupa full suport angalia usilewe huo umaarufu na kuona kwamba ndo njia ya kwenda Ikulu.NO.Jisahiishe kwa hilo
PILI.Angalia usijekubomoa misingi ya kizalendo walionayo wapambanaji wa mafisadi ikaonekana wote ndo walewale wanajenga jina kwenda ikulu.Ni dhahiri kwamba huna ubia na chama cha CHADEMA,kwa hiyo ukivurunda watakutupilia mbali hili wao kama waendeleze mapambano halisi kwa ajili ya kumkomboa mkulima na mtu wa kipato cha chini anayeishi chini ya dola moja kwa siku NA SI KUKUMBATIA MSALITI KAMA WEWE ULIYEPEWA UBUNGE NA WANANCHI BADALA YA KUWAKOMBOA UNATUMIA MUDA MWINGI KUJIPIA DEBE KWENDA IKULU.pia jisahihishe kwa hilo
 
Ni mawazo yake lakini hapo kuanzia sasa anatakiwa awe makini sana wakati anapotoa matamko yake maana ni rais mtarajiwa na ili aweze kujiweka vizuri aachane na "wadogo" zangu.
 
Chonde chonde, Wakuu! Huyu mheshimiwa ameeleza adhma yake tu ya kuwa hapo BAADAE anakusudia kugombea urais na kupitia chama hicho hicho alimo hivi sasa. Sidhani kama mbunge anania ya kugombea urais ataanza kuharibu huko kwenye jimbo lake! Kwa waliomchagua hii ni nafasi nzuri ya kumbana maana kila atakachokitenda kitapimwa wakati akitaka kugombea urais. Na nadhani watu wa kutoka kwenye jimbo lao hawatasikitika kama iko siku watapata mgombea urais kutoka katika jimbo lao.

Naamini amesema hivi kuwa'assure' wanachama wenzake kuwa hana nia ya kuwasaliti kama walivyofanya wengine waliomtangulia. Vile vile anawatahadharisha tembo walio katika chama chake kuwa iko siku na yeye atataka kuukwa u 'big potato'. Sijaona bado tatizo hapa.

Cut the guy some slack.
 
...Kama kawaida, lundo la maneno kwa kitu ambacho kipo obvious!! ama kweli kipenda roho hula nyama mbichi.
...Zitto kachemka, na si suala la siasa za kizamani au za kisasa!! lakini hapa tupo kwenye gumzo na baraza lazima liendelee!!!! MIE PIA NAKUBALI KWAMBA ALICHOFANYA NI SAHIHI....Big Up ZITTO KABWELA, way to GO dude!!
...sio kila kitu,"leteni hoja" huo ni utoto!! unaweza ku-argue for or against kitu chochote hata kama si cha kweli. mara nyingi kwenye mazingira ya namna hiyo lengo linakuwa ni ushindi pasipo kujali facts!! kwa mwendo huo.....kweli tutafika?? hivi kwa akili yako deep deep inside, unaamini kwamba politically, Zitto Kabwela hajachemsha!!?? labda sina hoja......nanawa mikono, yamenishinda!!.

UKiona kada mpinzani anakupa thanks zisizoisha ujue kabisa unaongea pumba. Si unajua tena kadi ni NZI lazima afuate .......... Ukiwa unajiamini kuna wasiwasi gani kusema unataka uwe rais? Kama huna mpanga wa kuunda mtandao, kuchafua wenzio kwenye magazeti, kwenda kwa waganga wa kienyeji ili upate urais unakuwa na wasiwasi gani. Tuache wivu wa kijinga kabisa hasa sisi vijana. Wote tunakuwa kama tunaombea Zitto afanye kosa tumuangamize sijui sisi tukoje!

Asante sana zitto kwa msimamo wako na kazi nzuri kwa taifa. Mimi sijari kama mtu anafanya kazi kwa kutaka uraisi au kujikomba kama ana deliver mimi kwangu huyo mtu ni muhimu. na zito ni muhimu sana kwa taifa hili kuiliko NZI wengi
 
Watu mnanishangaza sana, Msekwa aliposema atagombea Usipika alipogombea mkaanza kumtukana kuwa ni mroho wa madaraka, kwanini agombee wakati alishatangaza kutogombea, Zito katangaza mapema nia yake siku za usoni mnasema ana uroho wa madaraka niambieni kipi bora kati hayo kutangaza au kutotangaza?
 
Zitto Kabwe says has eyes set on the...

2008-06-11 09:23:35
By Leonard Mubali, PST, Kibondo


The Kigoma North Member of Parliament, Zitto Kabwe, has said his ambition is to become President of the United Republic of Tanzania ``when the right time comes``.

HAina shida, ni determination nzuri, na KAtiba ya nchi inaruhusu kama una sifa zinazotakiwa. Cha muhimu ni kuwa na GOOD REASONS! Swali ni GOOD REASONS ni zipi? NIkitaka kuwa Rais sababu nimekuwa inspired na mafanikio ya Obama inaweza kuwa sababu nzuri? Kupambana na mafisadi? Kuendeleza kazi walioianza mafiusadi? Am not sure....
 
Mimi nadhani alichosema Zito hakina ubaya wowote ila pia nadhani kwa baadhi ya well wishers (including myself) wake wanaona katika mazingira tuliyonayo Tanzania Zitto angeendelea kukaa nalo hilo moyoni ila aendelee kuchapa kazi! Kama ni mtu wa kuwa rais atakuwa almradi recordi yake ipo! Wasiwasi ni kwamba baada ya kutangaza, ataangaliwa kama mnafiki yaani kila alichokuwa akikifanya kama mbunge ilikuwa ni kujifagilia njia ya urais! Pia anaweza kuwa ameji expose kwa critics wake! Shida ya mazingira yetu si kama katika demokrasia zilizokomaa, hurdles ni nyingi sana! Tusichukue tamaduni za Marekani bila tahadhari! Nchi hii ni changa sana, ina uswahili mwingi mno, mtu wa kawaida wa Tanzania hafikiri kama mtu wa kawaida wa Marekani au Ulaya! Siasi ni pamoja na kuijua jamii yako vizuri.

Mimi pia naona tangazo kama la Zitto na siasa hizi za vyama tete vya upinzani linaweza kuleta migawanyiko isiyo na sababu. Wakati huu ambao watu wengi wanadhani wapinzani wangekaza msuli kupambana na ufisadi kwa kuimarisha bunge (kuwa na wabunge wengi) anatokea mtu anatangaza kuutaka urais (hata kama si kesho) na kuacha ubunge! Kwangu mimi (si lazima niwe iwe sahihi kwa wengine) tangazo la Zitto lina sound kama ametumwa ku disrupt concentration kwenye vita ya ufisadi!! This anouncement is simply NOISY, disrupting and untimely!

Binafsi namfagilia sana Zito kwa record yake na nakerwa na watu wanaomkebehi!! Hata kumwita Kabwela! Nadhani kwa muda mfupi amefanya mambo mazuri mengi kuliko wazee waliokaa miaka mingi sana bungeni! Tatizo langu ni Zitto ku dilute record yake kwa kuonenakana na uchu wa madaraka ya urais!! Pia habari (ingawa ni ya zamani) kuwa Zitto hatagombea tena ubunge, si habari njema kwa demokrasia na upinzani kwa ujumla. Huyu mtu anatakiwa sana bungeni, unless ana sababu nzuri sana za kutogombea! Kama anataka kuwa rais anatakiwa aonyeshe uchungu na nchi hii na si tu kuwatumia wananchi kukidhi haja zake anapotaka yeye!!! Tutasemaje, kiti cha Kigoma kikipotelea CCM tena! Nani tutamlaumu! Mbowe alipoteza kiti kule Machame, akijua kabisa urais hatashinda! Akina Sengondo nao badala ya kwenda kuwania ubunge, wanagombea urais wanaojua hawatashinda! Hivi hata takwimu (kura za maoni) haziwezi kutuongoza kubashiri mambo madogomadogo?

Let's focus on ufisadi, muda ukija akina Zitto na wenzie watoe matangazo yao. Nchi hii haihitaji mjadala wa rais sasa, inahitaji kukombolewa kutoka kwa watekaji (mafisadi). Zitto fanya kazi, urais ni nafasi moja tu! Watu wengi wenye sifa na mikakati mingi sana wameulilia sana urais hawajaupata! Mbona hamjifunzi! If you were meant to be a 'big potato' (in your own words) you will be, but for now let's (or just leave us alone to) focus on the topical issue - ufisadi!
 
Hayo mambo watu wanasema wakiwa secondary school, hawayasemi tena wakiwa wanasiasa mpaka siku inapofika wanapoamua kugombea.

Kama Zitto katamka hivyo leo, basi huyo keshashindwa tayari, sahau yeye kuwa rais wa Tanzania.
 
Kazi ipo Zitto na ana ndoto ya kufika magogoni,kupigiwa salute na kufunguliwa milango ya gari,ndoto ya mwanasiasa wa bongo bwana kushika madaraka makubwa na kumiliki mijisenti.
Zitto kaona kaka,baba zake "wanavyofaidika" na kunenepepsha matumbo yao an yeye kaona kakaaa miaka kibao ubungeni hajapata ile keki ya taifa kakusudia kuipata.Ni anaota jamani.
Na sina hakika kama ule ukoo pale Chadema utamkubalia kugombea juu pale
 
Mimi nadhani mjadala usiwe kama kachemka au lah, kwa sababu inawezekana anakuja na super strategy mpya ambayo ni mpya machoni mwa wengi.

Zitto alishasema kuwa hagombei ubunge 2010, kwa kutumia conventional wisdom tungeweza kuona akiacha ubunge maana yake anaacha siasa, lakini yeye mwenyewe anajua jinsi atakavyobaki viable kwenye siasa hata akiachana na ubunge. Na sasa amesema anataka urais muda wake ukifika.

Basi tunachohitajika kufanya labda ni kujifunza kijana huyu anayeonekana kuja na strategy mpya kwanza ya kuachia ubunge( rungu pekee alilonalo kuwawakilisha wananchi ), pili kutangaza kuutaka urais kabla hata umri wake haujakaribia miaka 40 inayohitajika let alone uchaguzi kuwa mbali.

Tuangalie nini tunaweza kujifunza kutoka kwake kabla, tukishaona hana lolote la maana ndio tuseme amechemka.

Kwa sasa ninachoweza kusema kwa swali la kama amechemka au lah ni mapema mno kupata jibu.
 
Mimi nadhani mjadala usiwe kama kachemka au lah, kwa sababu inawezekana anakuja na super strategy mpya ambayo ni mpya machoni mwa wengi.

Zitto alishasema kuwa hagombei ubunge 2010, kwa kutumia conventional wisdom tungeweza kuona akiacha ubunge maana yake anaacha siasa, lakini yeye mwenyewe anajua jinsi atakavyobaki viable kwenye siasa hata akiachana na ubunge. Na sasa amesema anataka urais muda wake ukifika.

Basi tunachohitajika kufanya labda ni kujifunza kijana huyu anayeonekana kuja na strategy mpya kwanza ya kuachia ubunge( rungu pekee alilonalo kuwawakilisha wananchi ), pili kutangaza kuutaka urais kabla hata umri wake haujakaribia miaka 40 inayohitajika let alone uchaguzi kuwa mbali.

Tuangalie nini tunaweza kujifunza kutoka kwake kabla, tukishaona hana lolote la maana ndio tuseme amechemka.

Kwa sasa ninachoweza kusema kwa swali la kama amechemka au lah ni mapema mno kupata jibu.
Mkuu kwani alisema hagombei 2010 ubunge kwa sababu zipi?
 
Kama kayasema kweli Zito mwenyewe maneno haya nampongeza kwa kuonyesha WAZI nia yake hiyo. Hii nitofauti kidogo na MTINDO uliozoeleka humu JF wa kuwataka watu wawe Marais wetu. La msingi atueleze tu anataka kulifanyia nini TAIFA letu.
 


Mimi nadhani alichosema Zito hakina ubaya wowote


....baada ya kutangaza, ataangaliwa kama mnafiki

.... Pia anaweza kuwa ameji expose kwa critics wake!

...tangazo kama la Zitto na siasa hizi za vyama tete vya upinzani linaweza kuleta migawanyiko isiyo na sababu.

...tangazo la Zitto lina sound kama ametumwa ku disrupt concentration kwenye vita ya ufisadi!!

...This anouncement is simply NOISY, disrupting and untimely!

...Tatizo langu ni Zitto ku dilute record yake kwa kuonenakana na uchu wa madaraka ya urais!!

... Watu wengi wenye sifa na mikakati mingi sana wameulilia sana urais hawajaupata! Mbona hamjifunzi!

Naona umechanganya madawa!
 
Wengi tumezoea politics za unafiki na kuficha ficha. Hatuna uwazi. Wanaotaka kuwa viongozi wanakaa kimyaaa as a result wanakwepa scrutiny yoyote ile kutoka kwa wananchi. By the time wanagombea hakuna mtu anayejua madudu yao ya nyuma. Thats what we have currently. Kifupi viongozi wetu hatujui rekodi na madudu yao ya nyuma kwa sababu wanakuwa kama surprise gift ya birthday.

What Zitto did, to me, Ameamua kuset higher standards na kweli he will be accountable. If he will live to the same level he has pronounced himself remains to be seen. But to me its a good thing! Akivurunda, watu wataweka rekodi, siku ikifika..watadownload file. Simple.

Kwanza wananchi ingebidi tumshukuru Zitto, maana ametupa mda mrefu kidogo ambao tutamchunguza na kujua kweli anafaa kuwa commender inchief au ni longo longo. Period. Hatuna haja ya kumdhihaki Zitto. Tatizo kubwa watu wanaogombea ndani ya CCM wanaogopa kujitangaza..sababu ni nyingi lakini unaweza kuonekana kama hufuati line, you can even lose your job kwa kutamani kiti cha mkuu wa kaya akiwa bado hai/madarakani..Thats the main reason kwa nini walio ndani ya CCM (in most African countries this is the case)......hawawezi kudeclare ambitions zao mapema...one can easily lose his/her job. And guess who is the loser? WE wananchi ambao tunapewa candidate ambaye inabidi tumchague within three months! can you make any analysis within such short period?

I say Thanks Zitto, but, just know.....All eyes are on you now! Kila lakheri!

Masanja
 
Huyo jamaa kwa namna moja ni mpiganaji asiyechoka na ni mjanja kwa kulingana na historia ya maisha yake. Lakini historia hiyo hiyo itamhukumu kwa nyakati tofauti za uongozi wake toka Kibohehe mpaka kuwa Secretary wa DARUSO pale Mlimani wengi tunamfahamu. Huenda kuwa keshabweteka au anatumiwa(sina ushahidi ni assumtion).Lakini jamaa ukijaribu kuangalia ni mpiganaji.
 
Nakubaliana na wewe,lakini hata hivyo inakuwa vyema kuwa mkweli anapoulizwa swali....Ambition kama hiyo inaonyesha kuwa ana wahka wa kutaka kuongoza nchi yake....je mnakumbuka Hillary aliposema kuhusu ya Obama?

Hapo mkuu mm sisemi....angalia kwa vile kasema mbongo mwenzetu watu kibao hapa ooh kachemsha ooh kajiharibia ooh sijui nn?wabongo ndo tulivyo siku zote ni kudiscourage watu,..sasa walitaka asemaje?
 
Hiki Ni Kihoja Cha Mwaka,wewe Zito Kabwe Kweli Unawaza Kuja Kuwa Rais Wa Tanzania??????????????????????????????
 
Du! hapa kazi ipo, maana siasa hii ya bongo ina mambo yake. Lakini mimi naona ka-mfumo kanakotulea wengi wetu humu ndani ndiko hasa kanamushekeri. Kwa sababu hata wale wanaojiita wataalam wa fani fulani madhalan uhasibu, uhandisi, uanasheria, wachumi na kada nyingine nyingi kwa bahati mbaya hawakuwahi kuwa na ndoto. Kwa mantiki hii nani anaweza kuniambia kukubali kwamba mtu anaweza akaeleza ndoto zake ni akazifikia na ili hali yeye, mimi na wewe hatujawahi kuwa na ndoto. Kuna haja ya mabadiliko na mabadiliko yenyewe ndio yaanzie hapa. Hii kuna gharama ya mabadiliko yoyote yale? kama jibu ndio basi Kabwe ndio anaonyesha gharama halisi ya nia ya kuibadilisha tanzania na mifumo yake ambayo wengi imetudumanza. Watu wamezoea kuyaweka mambo fulani fulani kuwa siri hata pale ambapo hakuna hitaji la kufanya hivyo. Jamani mfumo, mfumo! Mimi sipendi sioni kuchemsha au kutochemsha ila naona wingu la ajabu ambalo lenye taswira ya kwamba maandeleo kwetu yatachelewa sana. Sijahukumu maana nami bado sijaona kosa la kuwa wazi kwa bwana Zitto kuwa na haja ya kutimiza dhamira yake ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi kwa mujibu wa katiba.
 
Back
Top Bottom