Naona kama dunia nzima imeniangukia

Naona kama dunia nzima imeniangukia

Mkuu sidhan kama umepata matatizo kiasi hicho. Mwenye matatizo angekuja akiwa ameshaweka bond ama anahitaji kuuza gari ama kiwanja. Yaan wewe una assets bado unang'aa macho. Vipi kuhusu sisi wenye shida zaidi yako na hatuna asset? Mkuu una matatizo lakini wengine wanayo zaidi na hawana popote pa kushika.
Kabisaa!
Mbona hata simu ya smartphone angeuza...bado shida haijashika hatamu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
So, huna baba wala mama, au ndugu wa baba yako na mama yako? Mke wako hana baba wala mama, au ndugu wa mama wa mke wako au baba wa mke wako? Kaka, dada zako?
 
Kabisaa!
Mbona hata simu ya smartphone angeuza...bado shida haijashika hatamu.

Miss! si had ampate mteja hata wa hyo smartphone sasa! mie nimemuonea huruma kwakweli! ila asikate tamaa
 
Uza gari haraka au kaiweka dhamana sehem uchukue pesa kisha utarejesha mpeane mda ukishindwa una bargain gari basi maisha yanaendelea fanya hivyo kesho asubuhi na mapema
 
Pole Mkuu, pole sana...kwa kweli nimeshindwa hata kukupa like katika posti yako (nafsi inanisuta) ni kama vile nitakuwa nafurahia yaliyo/yanayo kukuta.

Najaribu kuwaza, labda pengine una ndugu ama rafiki wa karibu, jaribu kijishusha.... wafuate na uwaeleze swala zima, hususani mazingira yanayo mkabili SHEMEJI, dada, shangazi yetu, naamini unaweza kupata ama kutoka na ushauri utakao leta ufumbuzi wa tatizo.

Sijui pengine labda unapatikana MKOA gani...!

Naweza kukupa ushauri mwingine kuendana na MAZINGIRA.
Niko dar
 
Wakuu poleni na majukumu,

Nina umri wa miaka 34, mke na mtoto mmoja, nimepambana kweli kweli miaka 4 nyuma nimejenga kijijini kwetu nimenunua kiwanja pembeni kidogo ya mjini, nimemsomesha mke wangu kamaliza mwaka Jana, miaka 2 nyuma niliona mambo sio mabaya nikavuta kausafiri ka kunisaidia hapa na pale.

MATATIZO YANAANZA. Mwaka Jana nilibadilisha kituo kipya (sekta binafsi) kwa ahadi ya mshahara mkubwa. Dah mambo yakawa sio mambo mshahara ukawa hutoki mpaka miezi 3 hafu tunapewa nusunusu kumbuka hapo wife ameshakuwa mjamzito mimba inamsumbua kweli, mtoto anasoma na nadaiwa kodi ya nyumba. Ilinilazimu kuacha kazi baada ya kuvutana sana basi sikulipwa mishahara miezi mitatu katikati ya mwezi wa 5 nikapata kazi sehemu nyingine japo kwa mshahara mdogo nikalipwa mshahara nusu kwa vile nilianza katikati.

MAAJABU MENGINE HUKU. Leo in trh 4 July hatujalipwa mshahara wa June ninapoandika Uzi huu nimekaa jirani na nyumbani nafikiria nitaingiaje nyumbani kwa mke wangu, anaweza kujifungua muda wowote kuanzia sasa na ana complications, Jana ni kama vile tulilala njaa, leo mama na mtoto sijui wamekula nini, shule zimefunguliwa sina ada ya mtoto, mwenye nyumbani anadai kodi tena atakuwa ananisubiri nyumbani, nimejaribu kuuza gari na kiwanja lakini hakuna wateja. Nina mawazo sana ndugu zangu, ninachoogopa zaidi ni huyu mama mjamzito.

Ushauri wenu na sala zenu.
Kwani hicho kituo kipya cha kazi maboss wake ni watu gani?
 
Pole sana mkuu tuliza akili ,hayo unayoyapitia wewe sio wa kwanza na muda sio mrefu mambo yatakaa sawa uwe mwenye imani sana kipindi hiki kigumu cha maisha yako
 
Duh,mke pale mgonjwa,ada july hii hujalipa,kodi ya nyumba mtihani,na mshahara bado unauchungulia km umeingia na kila mara unakuta balance ipo under 10k,pole sana ila sababu ni mwanaume bas naamin kila kitu kitakua sawa soon.

Kwanza chukulia matatizo ni sehem ya maisha na ni ladha inayoyafanya maisha yawe kama maisha,ila tu yamekukuta wakat mambo meng yameingiliana pole

Una gar,sawa umeipark au inatembea,na kama inatembea kwenda kazin unatumia kiasi gan kwa mafuta? Kama umeipak sbu ya kukosa mafuta sawa ila kama bado unaitumia ntakulaumu,maana haiwezekan ukose hela ya kula ilihali gar inawekwa mafuta,japo hujasema ila ukwel u anaujua zaid kulko ss

Labda nikushauri kdgo cha kufanya japo sikulazimshi kufanya,angalia hapo ndan kwako kipi chepes cha kuuza,najua weng wamekushaur uuze gar au uliweke bond sawa una hiari,wengine wakashaur mrudishe mwanamke kwao sawa pia una hiari,na wengine wamesema uza kiwanja pia una hiari lakin je ukishauza utakua umesolve tatizo au umeongeza? Sawa kimfaacho mtu chake bt je ukiuza unadhan matatizo yatakwsha au yatakua umehamisha moja kwenda kushoto na lingine kwenda kulia?hapa naona utakua unapotea zaid,kwanza huna hela ya kula cha haraka kuuza ni simu yako maana saa yyte unaweza kupata hela ya kustiri siku mbili tatu au hata wiki kwa ajil ya msos nyumban,

Baada ya hapo mfate mwenye nyumba wako,kaa nae chini tena akiwa na mkewe mama mwenye nyumba mueleze A to Z tatizo linalokusibu naiman kabsa anaweza kukusaidia hasa akiona kabsa hal ya mkeo,

Then mfate muajiri wako mwambie naomba ruksa nikamuuguze mke hali yake sio nzur na mimba saa yyte anaweza jifungua,na hela hata mia sina,na wewe ndio muajiri plz najua mshahara haujatoka bt unaweza kunifanyia hata nusu nikamalize tatizo,kwa iman na ukwel huwez kosa msaada ppte,lakin umrudishe mke kwao kama wanavyokushaur kwa mtoto wa kiume sikushauri,pambana uonyeshe kwa nn wewe ni baba na usiuze cchte zaid ya simu yako halaf we tumia ya mkeo kufanya mambo yako yakutafuta cchte. Tchao
Xav bero asante sana.gari nimepark mkuu.ntafanya kama ulivyonishauri ndugu
 
Pole kwa matatizo. Ila hakuna kitu kinauzika kwa urahisi kama gari iwapo utaliuza kwa bei ya chini kabisa. Sasa hapo shida zimekujaa alafu unataka uuze gari kwa bei ya showroom na Magu mwenyewe kabana kila kona, it will not be possible.
Uza tu hilo gari hata kwa sh milioni mbili. Magari Japan hayajaisha utanunua jingine mambo yakikaa sawa...
 
Toka zamani ukioa Kama huyajui au uwezo huna mke alikuwa akijifungulia kwa wazazi wake kuna wakunga wa jadi kwenye koo waweza handle complications zingine kuliko madaktari bingwa waliosoma marekani kwa Trump. Huyo mwanamke asije kufia mikononi wapelekee waliomzaa
Inaonekana wewe kijana mdogo asiyejua majukumu kabisa....eti toka zamani yaaani mambo ya zamani unafananisha na mambo ya sasa...je kama hao wazazi wa uyo mwanamke wanaishi kijijini ambapo huduma za afya ni afifu na kutokana na hizo complication ikahitajika operation ya haraka itakuwaje?
 
Xav bero asante sana.gari nimepark mkuu.ntafanya kama ulivyonishauri ndugu
Ur Welcome Sir uapoomba kwa Mungu wako usizoee kujiombea wewe mwenyewe na familia tu bali ombea watu wate unaowajua na usiowajua lakin wana shida,,hii inakuwekea akiba kwa Mungu maana wapo pia wanaokuombea ambao huwajui,,Yatakwsha na tutafurah tukipata mrejesho hapa hapa Jukwaani
 
Duh,mke pale mgonjwa,ada july hii hujalipa,kodi ya nyumba mtihani,na mshahara bado unauchungulia km umeingia na kila mara unakuta balance ipo under 10k,pole sana ila sababu ni mwanaume bas naamin kila kitu kitakua sawa soon.

Kwanza chukulia matatizo ni sehem ya maisha na ni ladha inayoyafanya maisha yawe kama maisha,ila tu yamekukuta wakat mambo meng yameingiliana pole

Una gar,sawa umeipark au inatembea,na kama inatembea kwenda kazin unatumia kiasi gan kwa mafuta? Kama umeipak sbu ya kukosa mafuta sawa ila kama bado unaitumia ntakulaumu,maana haiwezekan ukose hela ya kula ilihali gar inawekwa mafuta,japo hujasema ila ukwel u anaujua zaid kulko ss

Labda nikushauri kdgo cha kufanya japo sikulazimshi kufanya,angalia hapo ndan kwako kipi chepes cha kuuza,najua weng wamekushaur uuze gar au uliweke bond sawa una hiari,wengine wakashaur mrudishe mwanamke kwao sawa pia una hiari,na wengine wamesema uza kiwanja pia una hiari lakin je ukishauza utakua umesolve tatizo au umeongeza? Sawa kimfaacho mtu chake bt je ukiuza unadhan matatizo yatakwsha au yatakua umehamisha moja kwenda kushoto na lingine kwenda kulia?hapa naona utakua unapotea zaid,kwanza huna hela ya kula cha haraka kuuza ni simu yako maana saa yyte unaweza kupata hela ya kustiri siku mbili tatu au hata wiki kwa ajil ya msos nyumban,

Baada ya hapo mfate mwenye nyumba wako,kaa nae chini tena akiwa na mkewe mama mwenye nyumba mueleze A to Z tatizo linalokusibu naiman kabsa anaweza kukusaidia hasa akiona kabsa hal ya mkeo,

Then mfate muajiri wako mwambie naomba ruksa nikamuuguze mke hali yake sio nzur na mimba saa yyte anaweza jifungua,na hela hata mia sina,na wewe ndio muajiri plz najua mshahara haujatoka bt unaweza kunifanyia hata nusu nikamalize tatizo,kwa iman na ukwel huwez kosa msaada ppte,lakin umrudishe mke kwao kama wanavyokushaur kwa mtoto wa kiume sikushauri,pambana uonyeshe kwa nn wewe ni baba na usiuze cchte zaid ya simu yako halaf we tumia ya mkeo kufanya mambo yako yakutafuta cchte. Tchao
Safii mkuu
Ukiwa mwanaume ni kukomaa tu hata kama unapitia magumu vp
 
Daah,.pole kamanda ila kukaa mbali na nyumba yako ni kukimbia tatizo tena upo katika kipindi ambacho mkeo anakuhitaji nahic kuliko vipindi vingine...hebu kuwa nae karibu hata awe na utata vipi jua kabeba mtoto wenu usimkimbie komaa lazima kipite hiki kipindi but kitapitaje "PAMBANA"

NB:fungu la kumi ni la lazima,inaweza kuwa umemuibia MUNGU saaana,.MUNGU akufanyie heri.
 
Pole sana lakini kabla ya yote beba mkeo kesho nenda kanisani usipoteze muda mambo yatakuja menyewe na kujiseti hata huyo boss wako ukimwendea kichwa kichwa kama haupo vizuri atakutolea nje kabla ya yote nenda kwa mchungaji hata kama si mlokole nenda kwa imani yako Mungu atakuona
 
Back
Top Bottom