Naona kama dunia nzima imeniangukia

Naona kama dunia nzima imeniangukia

Samjom

Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
27
Reaction score
24
Wakuu poleni na majukumu,

Nina umri wa miaka 34, mke na mtoto mmoja, nimepambana kweli kweli miaka 4 nyuma nimejenga kijijini kwetu nimenunua kiwanja pembeni kidogo ya mjini, nimemsomesha mke wangu kamaliza mwaka Jana, miaka 2 nyuma niliona mambo sio mabaya nikavuta kausafiri ka kunisaidia hapa na pale.

MATATIZO YANAANZA. Mwaka Jana nilibadilisha kituo kipya (sekta binafsi) kwa ahadi ya mshahara mkubwa. Dah mambo yakawa sio mambo mshahara ukawa hutoki mpaka miezi 3 hafu tunapewa nusunusu kumbuka hapo wife ameshakuwa mjamzito mimba inamsumbua kweli, mtoto anasoma na nadaiwa kodi ya nyumba. Ilinilazimu kuacha kazi baada ya kuvutana sana basi sikulipwa mishahara miezi mitatu katikati ya mwezi wa 5 nikapata kazi sehemu nyingine japo kwa mshahara mdogo nikalipwa mshahara nusu kwa vile nilianza katikati.

MAAJABU MENGINE HUKU. Leo in trh 4 July hatujalipwa mshahara wa June ninapoandika Uzi huu nimekaa jirani na nyumbani nafikiria nitaingiaje nyumbani kwa mke wangu, anaweza kujifungua muda wowote kuanzia sasa na ana complications, Jana ni kama vile tulilala njaa, leo mama na mtoto sijui wamekula nini, shule zimefunguliwa sina ada ya mtoto, mwenye nyumbani anadai kodi tena atakuwa ananisubiri nyumbani, nimejaribu kuuza gari na kiwanja lakini hakuna wateja. Nina mawazo sana ndugu zangu, ninachoogopa zaidi ni huyu mama mjamzito.

Ushauri wenu na sala zenu.
 
Wakuu poleni na majukumu.Nina uumri wa miaka 34,mke na mtoto mmoja.nimepambana kweli kweli miaka 4 nyuma.nimejenga kijijini kwetu nimenunua kiwanja pembeni kidogo ya mjini,nimemsomesha make wangu kamaliza mwaka Jana.miaka 2 nyuma niliona mambo sio mabaya nikavuta kausafiri cha kunisaidia hapa na pale. MATATIZO YANAANZA.Mwaka Jana nilibadilisha kituo kipya (sekta binafsi) kwa ahadi ya mshahara mkubwa.Dah mambo yakawa sio mambo.mshaha ukawa hutoki mpaka miezi 3 hafu tunapewa nusunusu.kumbuka hapo wife ameshakuwa mjamzito mimba inmsumbua kweli,mtoto anasoma na nadaiwa Kodi ya nyumba.Ilinilazimu kuacha kazi baada ya kuvutana sana bosi.sikulipwa mishahara miezi mitatu.katikati ya mwezi wa 5 nikapata kazi sehemu nyngne japo kwa mshahara mdogo.nikalipwa mshahara nusu kwa vile nilianza katikati.MAAJABU MENGINE HUKU.Leo in trh 4 July hatujalipwa mshara wa June. Ninapoandka Uzi huu nimekaa jirani na nyumbani nafikiria ntaingiaje nyumbani,kwa make wangu anaweza kujifungua muda wowote kwanzia sasa na ana complications,Jana ni kama vile tulilala njaa,leo mama na mtoto sijui wamekula nini,shule zimefunguliwa sina ada ya mtoto,mwenye nyumbani anadai Kodi tena atakuwa ananisubiri nyumbani.nimejaribu kuuza gari na kiwanja lakini hakuna wateja.Nina mawazo sana ndugu zangu.ninachoogopa zaidi ni huyu mama mjamzito.ushauri wenu na sala zenu
Mpeleke kwao akajifungulie kwao
 
kuwa na Imani mkuu ,haya ni majaribu,jaribu ni mtaji na yanamlango wa kutokea
 
mkuu kasema anacomplication ,anazaliaje nyumbani tena
Huko kwao hospitali hazipo? Wapelekee wenye mtoto wao waliomzaa asije kufia mikononi mwako Na ulofa wako. Asikufie mikononi warudishie waliomzaa na ueleze wazi kuwa ana complications na wewe sio mkunga wala doctor na pesa huna
 
Pole sana, hayo yote yanapita. Usikate tamaa utatoka tu Mungu anakuona.
 
Pole aisee, hizo ni hiccups tu za maisha, with due time everything will be alright.
 
Pole sana jamaa yangu.ushauri wangu kwanza mueleze mwenye nyumba hali halisi ulio nayo.pili huna ndugu au rafiki wa karibu wa kuweza kumshirikisha? Pole sana yanapita tu hayo usiwaze sana. We ni mwanaume ukikata tamaa wewe basi familia nzima imeangamia .jikaze
 
Back
Top Bottom