Hellow JF
Naomba hata kama kuna Mtaalamu wa masuala ya psychology anisaidie kuniweka sawa.
Nimepata ajali na bajaj yangu sijui itachukua muda gani kurudi barabarani..
Lakini sijui marejesho YANGU yatasimama au vipi, na sijui ikipona ntarudi tena au ndio wataichukua moja kwa moja.
Ntakuwa nimekosa vyote yani niko hopeless
Yani Daaah sina ABC wala D
Msaada wa mawazo please.
Pole
1: Usiishi kwa kufikirika, kuwa proactive. Fanyia kazi yaliyopo kwenye mikono yako/usibaki kuyafikiria. Hapo muda unakuwa unakwenda, hivyo tumia muda wako vizuri bila panick.
2: Timiza wajibu wako kwa uaminifu, yaliyokutokea yaweza kumtokea yeyote na kwa madhira magumu zaidi.
3: Usijaribu kumtolea majibu yule ambaye haujamfikishia ujumbe, fikisha ujumbe kamilifu kwa kadri ya hali halisi na uwe chanya/be positive. Pata maoni halisi ya mhusika na uyafanyie kazi kikamilifu.
4: Amini aliyekufikisha hapo ulipo bado anaweza kukupitisha kwenye hilo na kukupeleka kwenye mafanikio zaidi.
5: Amini maisha ni kama barabara, huwezi kukosa kona na kona zenyewe ndo hizi ulizopo. Kata kona kwa uangalifu na spidi nzuri utafika.
6: Amini katika utaratibu wa maisha, usifikiri na kuamini katika kumaliza tatizo ghafla/kwa mkato hii inaweza kugharimu zaidi na kukuchanganya.
7: Pata wasaa na wenzako kijiweni ili kuangalia jinsi ya kutatua changamoto ndogo ndogo za kimaisha na michongo mipya. Kama umekuwa ukiishi ndani ya misingi ya kiutu basi usihofu.
8: Chukulia kila changamoto kama daraja la kupambana zaid, kuongeza juhudi wala changamoto isikunyong'onyeshe.
Nakutakia mafanikio mema.