Naona aibu kusema nina masters ya Mzumbe

Naona aibu kusema nina masters ya Mzumbe

Yan me nimefanya hizo za wanafunz wa mzumbe wanafika hata mia, ni wavivuu na hawatak kujishughulisha na wako busy sana na mambo yao kuliko shule basi we unawagonga bei tu
 
Wadau wa JF
Salam natumaini mu wazima! mimi ni muhitimu wa Masters of Business Administration ( Corporate Management) Mzumbe University kiukweli sioni kama nilijifunza kitu kipya kwenye hiyo Masters maana kuanzia Coursework (Assignments) kuna walimu walikuwa wanajitangaza kuwa ukihitaji kufanyiwa Assignment unatoa hela kidogo anakufanyia.

Kufika hatua ya Dissertation ndo nikaelekezwa kwa "Prof" (kwa bahati ndo alikuwa supervisor wangu chuoni) ana ofisi binafsi Mjini, nikaenda tukakubaliana bei yeye ndo akawa anafanya kila kitu mimi nimekuja kukabidhiwa Dissertation ikiwa imeshasainiwa na supervisor nikaenda ku-submit. Kiukweli roho yangu inanisuta maana sijaitendea haki taaluma.



Boya kwelikweli ,waliodisco wengi wanahasira Na walimu waliowafundisha Na chuo wanakichafua
 
wanaochafua Chuo, sio MU tu Chuo chochote ni wale wambao wanataka vyuo vyao vionekane the best au wale walisoma ktk vyuo hivyo then wakafeli. Elimu ya Bongo kweliina shida ktk Vyuo vyotee, ila sio to the extent ya mtoa mada anavyokandia, kama mtoa mada alidisco enzi hizo atulie tu.
Tusome
 
bad enough at the end of the day mtu kama wewe mleta mada ndio unakuja kuwa mtunga sera ktk taasisi nyeti ya kitaifa.mweee!
Yupo serikalini,ni muajiriwa wa taasisi ya ums huyu jamaa.anadhani hafahamiki
 
Ukiona hivi mtoa mada atakuwa "alikatwa shingo" sasa anafanya juu chini kuichafua Mzumbe.
Au ulikamatwa na kibuti, ukasafirishwa na ambulensi hadi Msamvu!
Huo ushuzi ulioandika kuichafua MU ushindwe na ulegee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom