Naona aibu kusema nina masters ya Mzumbe

Naona aibu kusema nina masters ya Mzumbe

Hyo ndo elimu ya bongo kuna wakufunzi wwngine wana PhD lakin anachokifundisha hata yy akijui yaan ni balaa tupu
 
Wadau wa JF
Salam natumaini mu wazima! mimi ni muhitimu wa Masters of Business Administration ( Corporate Management) Mzumbe University kiukweli sioni kama nilijifunza kitu kipya kwenye hiyo Masters maana kuanzia Coursework (Assignments) kuna walimu walikuwa wanajitangaza kuwa ukihitaji kufanyiwa Assignment unatoa hela kidogo anakufanyia. Kufika hatua ya Dissertation ndo nikaelekezwa kwa "Prof" (kwa bahati ndo alikuwa supervisor wangu chuoni) ana ofisi binafsi Mjini, nikaenda tukakubaliana bei yeye ndo akawa anafanya kila kitu mimi nimekuja kukabidhiwa Dissertation ikiwa imeshasainiwa na supervisor nikaenda ku-submit. Kiukweli roho yangu inanisuta maana sijaitendea haki taaluma.
.
Manne:

1. Ulitoa rushwa
2. Prof alipokea rushwa na kutumia madaraka yake vibaya
3. Wote mnastahili kupelekwa TAKUKURU
4. Toa taarifa tangu sasa jamaa waanze kazi yao.
 
nimeamua kurudia upya Master degree UDSM

Hayo ndiyo matunda ya ujinga na ubabaishaji wetu sisi wanafunzi. Umeona sasa? Hiyo ndiyo gharama ya ujinga wako.
Kuandikiwa dissertation ni ujinga wa mwanafunzi mwenyewe. Haina demarcation ya moja kwa moja na chuo husika. Ujinga wako ndiyo umekufikisha hapo
 
Labda sio Mzumbe nayoijua mimi iliyonipa basic skills hadi badae law school nikaona kama maji na kuichukua just per one shot.
 
Hujasema kama ni arts au sayansi. Ni dhambi kubwa katika masomo ya sayansi, kama ni doctor umechukua cheti cha kuuwa watu. Haya mambo yao na nimeshuhudia hasa wanawake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom