Naombeni ushauri wenu dada zangu na kaka zangu

Naombeni ushauri wenu dada zangu na kaka zangu

Bado najiuliza kama kweli anania njema na mimi kwanini Gran Melia?,kiukweli sitokwenda na kama ni kuteseka ngoja niteseke tu
Ningekuwa Arusha ningekusindikiza kwenda kula kuku wa kuoka, mkiwa wawili hawezi kukuambia kuingia chumbani aibu.
 
Nimekuwa nikipitia changamoto mbalimbali katika maisha yangu ya mahusiano,najitahidi sana kumuomba mungu anisaidie nipate mtu sahihi na siyo wa kunichezea.

Wiki mbili zilizopita niliandika hapa niliyopitia kuhusu boyfriend wangu na namshukuru Mungu mliishia kunitukana sana na hamuelewi nachopitia kwa sasa ila yote namuachia Mungu muweza wa yote.

Nimekuja kwenu dada zangu na kaka zangu kuwaomba ushauri pengine nikawa nina makosa au niko sawa.

Baada ya lile sakata la Boyfriend wangu kiukweli nilimsamehe kutoka moyoni ila nilimwambia hatupaswi kuendelea tena na mahusiano.Juzi jumapili nilienda nilienda kanisani kwa Nabii mmoja hapa Arusha mkubwa tu na anafahamika,nilivyofika alipoanza kutabiri niliitwa mbele ya kanisa na kuniambia anayajua mambo yangu yote kuhusu boyfriend wangu na anaona namna gani napata mateso akaniambia kabla ya kuondoka napaswa kuonana nae ofisini kwake,kiukweli nilihisi moyo wangu kutulia kwasababu nilikuwa mikononi mwa Bwana,baadae kabisa mida ya jioni baada ya ibada nilimfuata ofisini kwake kutaka kuonana nae,alikuwa kama amenisahau ila nikamkumbusha akawa amenikumbuka na akaniambia mambo yangu ni mazito na nisipomkabidhi moyo wangu ili aukabidhi kwa kristo sito fanikiwa katika mambo yangu ya kimaisha na kimahusiano,hivyo akanitaka tarehe 4 .6.2023 nionane nae hotel ya Gran Melia usiku ili anisaidie,nilipokuwa naondoka alinipa hela ambazo hadi muda huu nimeshindwa kuzitumia nikiziogopa.

Yaani ndugu zangu sielewi nifanye nini,je kweli atakuwa na nia njema na mimi au anataka kutumia mwanya wa matatizo yangu ili ajinufaishe yeye?
Utagongwa na kupewa vihela vya kula hovyo hovyo tu na mikosi ambayo itachukua tena hiyo pesa yote na ubaki masikini na mikosi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Badala utumie pesa ulopewa kufuta stress zako za mapenzi bado unawaza kusaidika kwenye mapenzi! Nenda akubake ufe na sonona
 
Back
Top Bottom