Dr hyperkid
JF-Expert Member
- Jun 7, 2019
- 13,979
- 27,550
hiki si kijiwe cha wajinga dogo,ni vyema ukaachana na fikra za kichangudoa
Wasambaa hao wanapenda Sana chai 😂Hivi huwa mnafaidika nini kupika hizi chai mchana wote huu na jua lote kali hivi..?
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]anataka tu tutoke majasho na hatuna magari
Anyway vitafunio viko wapi nile zangu mie
Anakosea sana kukuita changudoa 🥺🥺🥺Uchangudoa wangu hapo uko wapi?,kutaka ushauri ni kosa jamani?
Mwaya tena !!!Hupendi kuitwa kaka!basi nisamehe mwaya
yoteuliyoandika hapo ni fikra za kichangudoa huko arusha baridi linawatesa sana sioUchangudoa wangu hapo uko wapi?,kutaka ushauri ni kosa jamani?
Nanamucho achana nao hao ndo walivyo wakaka hawa..Umewahi kunila bure?,kwanini unanidharirisha?
Hivi nyie mnadhani kila mwanamke humu ndani ni malaya kama hao mnaokutana nao huko makwenu?
Wajinga ndiyo waliwao.Nimekuwa nikipitia changamoto mbalimbali katika maisha yangu ya mahusiano,najitahidi sana kumuomba mungu anisaidie nipate mtu sahihi na siyo wa kunichezea.
Wiki mbili zilizopita niliandika hapa niliyopitia kuhusu boyfriend wangu na namshukuru Mungu mliishia kunitukana sana na hamuelewi nachopitia kwa sasa ila yote namuachia Mungu muweza wa yote.
Nimekuja kwenu dada zangu na kaka zangu kuwaomba ushauri pengine nikawa nina makosa au niko sawa.
Baada ya lile sakata la Boyfriend wangu kiukweli nilimsamehe kutoka moyoni ila nilimwambia hatupaswi kuendelea tena na mahusiano.Juzi jumapili nilienda nilienda kanisani kwa Nabii mmoja hapa Arusha mkubwa tu na anafahamika,nilivyofika alipoanza kutabiri niliitwa mbele ya kanisa na kuniambia anayajua mambo yangu yote kuhusu boyfriend wangu na anaona namna gani napata mateso akaniambia kabla ya kuondoka napaswa kuonana nae ofisini kwake,kiukweli nilihisi moyo wangu kutulia kwasababu nilikuwa mikononi mwa Bwana,baadae kabisa mida ya jioni baada ya ibada nilimfuata ofisini kwake kutaka kuonana nae,alikuwa kama amenisahau ila nikamkumbusha akawa amenikumbuka na akaniambia mambo yangu ni mazito na nisipomkabidhi moyo wangu ili aukabidhi kwa kristo sito fanikiwa katika mambo yangu ya kimaisha na kimahusiano,hivyo akanitaka tarehe 4 .6.2023 nionane nae hotel ya Gran Melia usiku ili anisaidie,nilipokuwa naondoka alinipa hela ambazo hadi muda huu nimeshindwa kuzitumia nikiziogopa.
Yaani ndugu zangu sielewi nifanye nini,je kweli atakuwa na nia njema na mimi au anataka kutumia mwanya wa matatizo yangu ili ajinufaishe yeye?
Sipo tayari kuona unatesekaBado najiuliza kama kweli anania njema na mimi kwanini Gran Melia?,kiukweli sitokwenda na kama ni kuteseka ngoja niteseke tu