Naombeni ushauri wenu dada zangu na kaka zangu

Nanamucho

Senior Member
Apr 8, 2023
115
557
Nimekuwa nikipitia changamoto mbalimbali katika maisha yangu ya mahusiano,najitahidi sana kumuomba mungu anisaidie nipate mtu sahihi na siyo wa kunichezea.

Wiki mbili zilizopita niliandika hapa niliyopitia kuhusu boyfriend wangu na namshukuru Mungu mliishia kunitukana sana na hamuelewi nachopitia kwa sasa ila yote namuachia Mungu muweza wa yote.

Nimekuja kwenu dada zangu na kaka zangu kuwaomba ushauri pengine nikawa nina makosa au niko sawa.

Baada ya lile sakata la Boyfriend wangu kiukweli nilimsamehe kutoka moyoni ila nilimwambia hatupaswi kuendelea tena na mahusiano.Juzi jumapili nilienda nilienda kanisani kwa Nabii mmoja hapa Arusha mkubwa tu na anafahamika,nilivyofika alipoanza kutabiri niliitwa mbele ya kanisa na kuniambia anayajua mambo yangu yote kuhusu boyfriend wangu na anaona namna gani napata mateso akaniambia kabla ya kuondoka napaswa kuonana nae ofisini kwake,kiukweli nilihisi moyo wangu kutulia kwasababu nilikuwa mikononi mwa Bwana,baadae kabisa mida ya jioni baada ya ibada nilimfuata ofisini kwake kutaka kuonana nae,alikuwa kama amenisahau ila nikamkumbusha akawa amenikumbuka na akaniambia mambo yangu ni mazito na nisipomkabidhi moyo wangu ili aukabidhi kwa kristo sito fanikiwa katika mambo yangu ya kimaisha na kimahusiano,hivyo akanitaka tarehe 4 .6.2023 nionane nae hotel ya Gran Melia usiku ili anisaidie,nilipokuwa naondoka alinipa hela ambazo hadi muda huu nimeshindwa kuzitumia nikiziogopa.

Yaani ndugu zangu sielewi nifanye nini,je kweli atakuwa na nia njema na mimi au anataka kutumia mwanya wa matatizo yangu ili ajinufaishe yeye?
 
Nimesoma mwanzo mwisho..
Kwanza pole kwa yaliyokukuta mrembo..
Mi na wewe rika moja tuu huna haja ya kuniita kaka ako..🤓😂😂😂
Kuhusi hiyo pesa wee tumia usiogope ila kwenda huko hotelini usiende..
Mwambie ""Naijua hiyo""
Kwa sasa upo single au ...?
Jimbo lipo wazi ...?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom