Naombeni ushauri wakuu, ndani pamewaka moto

Issue ipo hivi....
Wife alisafiri, baada ya kurudi juzi na kama kawaida nikampokea kwa furaha tele kisha nikampeleka home na nikamuacha anahangaika na watoto pale.

Picha lilianza baada ya wife kuamua kufanya usafi hasa wa chumbani kwetu maana tumepanga chumba kimoko kwenye nyumba yenye wapangaji shazi.

Lahaula walaquwata, mara wife kagongana na nguo ya ndani ikiwa chini ya uvungu wakuu.
Sasa moto uliowaka hapa mwenzenu sijui la kufanya, sasa wakati tukiendelea kuzozana mara ghafla nikamuona panya anaingia kutoka mlango wa room ya jirani akiwa na hereni kaiuma mdomoni, na kwasababu tulikuwa kwenye mzozano mkali nilishindwa kumwambia wife atazame nilizo kiona maana mzushi rat alikuwa tayari kama kashtuka na akaitema ile hereni na kukimbia nje chap.

Sasa wakuu hapa nimeamua kuondoka home ili nipishe mgogoro kwa muda na tayari yule panya ameiacha ile hereni na hapa nawaza wife akiiona, jumlisha na ile nguo aka kabati tena nalifananisha na zile za huyu jirani yetu wa mlango tunao tazamana nao.

Wakuu, ebu nipeni maujanja maana ukweli sijawahi ingiza spare tyre geto wakati wife hayupo, for sure panya ndio kaniletea hili timbwili.

Naombeni maujanja ili ninusuru ndoa yangu mimi ndege janja nilie naswa kwenye tundu bovu leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Chai tena chai ya majani ya chai bila hata iliki na mdalasini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo kila muda ni muda wa mambo serious, jamaa kaamua kuweka changamsha akili tu.

Ni kama yale mafumbo ya darasani, ya bata mbele ya bata na bata nyuma ya bata jumla ni bata wangapi?

Halafu punguzeni kutumia akili nyingi JF.
Mfano post ambayo ni ya kweli na ya uzushi unaitofautishaje? I mean unajuaje huyu mtu anahitaji msaada au ana tania?
 
Alipoondoka yaani mlipokuwa mnapanga safari si mlivunja jungu?? Hiyo mechi ya kuagana alifanikiwa kupata goli ngapi?? Sasa, hakikisha kapata magoli yale yale na moja la nyongeza kumthibitishia kuwa, ugwandu ulikuwa nao
 
Alipoondoka yaani mlipokuwa mnapanga safari si mlivunja jungu?? Hiyo mechi ya kuagana alifanikiwa kupata goli ngapi?? Sasa, hakikisha kapata magoli yale yale na moja la nyongeza kumthibitishia kuwa, ugwandu ulikuwa nao
Ahsante kwa ushauri mkuu, hili nalichukuwa likatumike

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom