Wakuu naombeni mawazo yenu(ushauri)

Wakuu naombeni mawazo yenu(ushauri)

Nyamkata

Member
Joined
Nov 6, 2019
Posts
13
Reaction score
24
Wakuu naombeni mnisaidie mawazo, maana kuna kipindi mtu unakua kwenye wakati mgumu mpaka unaona kila uamuzi unaoufanya hauko sahihi. Wakuu hapa nilipo nina mke na tuna watoto wawili.

Mwaka 2017 niligundua kua kuna jamaa anatoka na mke wangu, nilipopata taarifa nilijaribu kumuuliza mke wangu kwa kuongea nae taratibu tena kwa busara kabisa ili nipate ukweli kuhusu jambo hilo ila matokeo yake alikuja juu sana na kutishia kua angekunywa Sumu kwa sababu namsingizia mambo ambayo hajayafanya.

Baada ya hali ile kutokea sikuendeleza mjadala ila nikamwambia kama hili jambo lina ukweli basi aache maana litatuharibia familia na huyo bwana anaemdanganya hana malengo yoyote mazuri na yeye zaidi ya kumharibia tu maisha kisha anapotea.

Wakati yote hayo yanaendelea mimi nilikua kazini. Na kazi yenyewe haikua na makazi maalumu. Tulikua tunahamishwa sehemu mbalimbali kulingana na project zinazokuepo. Ila nikiwa mbali nilikua najitahidi kufika nyumbani mara kwa mara, na pia nilimwambia awe huru wakati wowote atakapojisikia kuja nilipo, nimkatie tiketi awe anakuja.

September 2018 nikawa nimefika home ghafla nilipofika nikaingia ndani sijakaa hata dk 5 simu yake ikaita, ilikua sebuleni nikaichukua kuangalia namba nikakuta ni yule jamaa ndo kapiga, nikampa mtoto simu nikamwambia ampelekee mama alikua kwenye ofisi zake hapo hapo nyumbani, sikufuatilia walichoongea.

Kuanzia hapo nikawa namfuatilia na nikagundua kuwa tofauti na huyo Jamaa bado ana mahusiano na jamaa wengine wawili, usiku wake nikambana akanieleza ukweli ni kwamba alikua na mahusiano nao ila ameachana nao tayari. Ila nilichobaini si kweli kua ameachana nao maana nilipokua nafuatilia nilikuta mawasiliano bado yapo japo kila napomuuliza anajitetea sana.

Nilimchukua tukaenda kupima VVU nikakuta Mwenyezi Mungu alimnusuru yupo Safi. Baada ya hapo tukaendelea hivyo hivyo na baadae akapata ujauzito, ila kwa kipindi chote hiki alikua anaficha kweli simu yake, akija ndani anaiacha ofisini na usiku akilala anaizima.

Ila wakati mimba ina miezi 7 nikakuta msg ya yule jamaa wa mwanzo kabisa, akimtaka wakutane, nilimhoji tena huyu mwanamama lakini hakunipa jibu la kueleweka.

Baadae alijifungua salama, sema kwa bahati mbaya au nzuri mtoto ametoka copy ya mama yake, kwa kipindi cha uzazi sikuona mawasiliano yakiendelea. Ila sasa hivi mtoto ana miezi mitano na nimekuta mawasiliano yameanza tena.

Kwa hayo machache wakuu naomba mnisaidie mawazo yenu, maana binafsi bado sijaamua chochote. Na kama kuna swali mniulize tu maana nimejitahidi kufupisha.
 
Pole kwa yaliyokusibu na kama ni hadith za hawafu mwenye nguvu pia tunashukuru. Inaonekene una mashaka na mtoto wa mwisho alozaliwa cha msingi nenda kapime DNA utapata ukweli.

Usijelea mtoto wa watu baadae anakuja kukupiga unashangaa na wakati historia unaifaham. Na siku zote nyani hasahau pori lake.
 
Kingsmann,
Nashukuru kwa ushauri mkuu, kuna kipindi niliwaza hivyo ila hata nisiposhiriki nae INA maana ndo itakua hivyo for the rest of my life??

Because I am 30 now. Maana naona kurudishwa nyuma sana, maana nimejenga akiwepo na kuna miradi nimefanya akiwepo na nikampa yeye kuisimamia kutokana na Mimi kuwepo kwa mkaburu. Na pia gharama/muda wa kuanzisha Familia nyingine tena. Maana hapa Future siioni
 
Watu tupo tofauti sana Nimehisi mpaka kinyaa unajua kabisa mke wako hajatulia na bado unamkumbatia aisee badilika wanaume hatupo hivo
 
Ndugu ukweli ni kwamba mkeo kaisha wavulia nguo hao michepuko wake hivyo ni ngumu kubadili matokeo

Pia naamini hata yeye anatamani kuachana nao lkn anashindwa kwasababu imeisha kua hapo hata kumtimua sawa na bure

Kikubwa ichunguze kwa kiina nini kumepelekea kufanya hivyo lazima kuna sababu ukisha kuridhisha ndio angalia nini cha kufanya
 
Mkuu naona umeshindwa kufanya maamuzi mwenyewe.

Basi kama kuna mlezi hapo mzee wa makamo(Mzazi wako wa kiume/mzee yeyote) mshirikishe hili japo najua kabisa majibu yote unayo.


Pia hakikisha malezi kwa watoto yawn bora maana jukumu ni lako kwa sasa.
 
Pole kwa yaliyokusibu na kama ni hadith za hawafu mwenye nguvu pia tunashukuru. Inaonekene una mashaka na mtoto wa mwisho alozaliwa cha msingi nenda kapime DNA utapata ukweli. Usijelea mtoto wa watu baadae anakuja kukupiga unashangaa na wakati historia unaifaham. Na siku zote nyani hasahau pori lake
shukuru Mkuu, Jana nilipita kwenye thread ya sheria, nikaangalia taratibu za kupata vipimo vya Vinasaba, ila utaratibu wake una ugumu flank hivi. Na pia nikajaribu kuongea na mtaalamu mmoja hivi wa Afya akanambia kulingana na Ethics za taaluma yao kikubwa kinachoangaliwa kwenye kutoa majibu ya DNA Mara nyingi cyo interest ya mteja Bali wanaangalia Mazingira ya mtoto baada ya majibu yanaweza kuwaje. Hivyo wanaeza pia wakalazimika kukuambia mtoto ni wako ili Maisha ya mtoto yaweze kuendelea vizuri baada ya majibu.
 
Pole sana mkuu...maradhi ni mengi sana kumvumilia mtu wa namna yake...sio lazima kuwa na mme au mke asiye mwaminifu na hicho pia ni chanzo cha kuvunjika kwa ndoa kiimani
 
Duh pole sana mkuu ila kuchapiwa kunauma sana ila wewe jamaa unaroho ngumu sana ila kwamimi binafsi nahisi tungekuwa tumeshaachana nahuyo mwanamke zaman sana.

Kwanza kitendo2 chamkeo kushukiwa anatembea namtu fulani basi tayari nidosari kubwa sana kwenye ndoa yenu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom