Naombeni ushauri nnahisi nimerogwa!

Naombeni ushauri nnahisi nimerogwa!

Sijaenda ila nina mpango wa kwenda

Watu wangu wengi wa karibu biashara zao zinaenda vizuri sana na wanAenda kwa waganga sana

zAmani mimi sikupenda haya mambo lakin sahv nimeanza kuyaamin,ukitaka mambo yako yaende vizuri haraka lazima uwaone wataalamu uoge

Maana huku kwetu kwa watu weusi unaweza fanyiwa ujinga na mtu ambae hata humjui na wala hana tatizo na wewe
Fuatilia kwa karibu maisha wanayoishi, mara nyingi furaha yao huwa haidumu

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Vipi ukoo wenu au ukweni hakuna historia ya kuchawiana na kutupiana maulozi
 
Pole sana mkuu
Screenshot_20211225-200710.png
 
Sitaki niseme yalionifika lakini miaka 3 nyuma nimekutana na mambo mengi tu. Hasa kwenye kipato na biashara imeyumba sanaa. Nilichofanya kila nikipata hela natoa sadaka kwa mwezi naweza toa sadaka hata ya 100,000. Mwenyezi Mungu anapokupa neema yake, nawe toa sadaka kwa ajili yake.
Sadaka inanguvu sana
 
Ukianza kuwaza kwamba unalogwa, ujue unaelekea kuharibu maisha, there are difficult moments, hutaki tu kukubaliana nazo.

Unafikiri huu uchawi ulingoja upunguzwe kazi? Pambana na maisha, acha kuwaza unalogwa, hakuna mtu anakuloga.

Shikamana tu na imani yako, lakini sio kwa mawazo kamba unalogwa, hakuna mtu anayekuloga ndugu yangu.
Comment nzuri kwangu
 
Pole sana,

Ila hio situation ni kawaida mzee, alaf usijeweke sana kwenye mazingira ya kua huna mapungufu, kubali una mapungufu mengi tu yan amini pia hata kupunguzwa kazini sio kua umeonewa ilitokea kwa sababu,

Kubali hujakamilika uku ukilia na Mungu uku ukijitahidi kujirekebisha ipo nana ila usijiumize,
Swala la Mganga mzee mganga wako ni wee mwenyewe, amini katika Mungu au Miungu ulionayo alaf katika kuomba labda vikubwa unavyovitaka na kuona vinachelewa angalia na unavyoviona vidogo vilivyojibiwa shukuru toa sadaka

Huo ni mchakato tu kawaida, kuna mda karma kukufunza, kuna mda kuandaliwa kwa mazingira mengine, jione bora ila si bora kuzidi wengine

Humu ndani kuna watu tukikupa mapito humu mzee unaweza elewa una kila sababu ya kumshukuru Mungu wako alaf bado tuna bol yan sawa tunaona hatujibiwi vikubwa tuombavyo ila mbona vidogo vyote vinajibiwa katika hali isiyo ya kawaida kwaiyo wakati upo huo mchakato tu

KUKATA TAMAA NI MWIKO NI SUMU
 
Kila Mwanadamu kwenye huu ulimwengu lazima apite kwenye majaribu. Jaribu ni kipimo Cha Imani Yako pia. Komaa kama Ayubu. Kuna wenzako Wagonjwa zaidi ya Miaka 5, wengine walemavu, wengine wapo jela. Wewe ni nani husipate jaribu? Endelea kumuamini Mungu litapita utainuka upya.
 
Back
Top Bottom