Naombeni ushauri nnahisi nimerogwa!

Naombeni ushauri nnahisi nimerogwa!

Wana Jamvi, Mwenzenu leo nimekuja nnaomba ushauri, Ni zaidi ya miaka miwili sasa mambo yangu hayaendi jinsi inavyopaswa mpaka inanipelekea kuhisi kwamba inawezekana kuna kitu hakipo sawa.

Mwaka 2020 nikiwa niko kwenye ajira, kwenye kitengo muhimu, mtu anayetegemewa, mwenye record nzuri kazini, performance nzuri lakini nikachaguliwa kuwa miongoni mwa wanaopaswa kupunguzwa na ofisi kwa kigezo kuwa kampuni haifanyi vizuri. kwa hiyo kazi ilikoma mwezi wa 6 mwaka 2020.

wakati huo sikuona shida sana kwa kuwa nlikuwa na miradi kadhaa iliyokuwa na uwezo wa kuniweka mjini, nlikuwa na Vi IST vyangu viwili vinafanya biashara ya kubeba abiria kupitia mtandao.

lakini pia nlikuwa nnafuga kuku wa mayai wasiopungua 1000, na shambani kwangu nlikuwa nimepanda mazao ambayo niliyategemea kibiashara ambayo ni mapapai na migomba. kwa bahati mbaya mapapai hayakuzaa kama ilivyo tarajiwa na migomba nayo haikufanya vizuri,

baada ya kazi kuisha nilimpunguza dereva mmoja nikaanza kuendesha mwenyewe gari moja ili kujiongezea kipato, cha kushangaza hata hesabu ya gari nikawa sifikishi, hela haionekani, ukiwa barabarani hela unaiona lakini ukija kwenye akiba hakuna hela, ukiangalia matumizi sio makubwa ila hela haionekani.

mwanzoni mwa mwaka 2021, picha linaanza kule shambani kuku waakanza kufa kila siku unaokota kuku 100 mpaka 200, ugonjwa haujulikani, kuku wana chanjo zote, wamepewa dawa zote, chakula ni kile kile Daktari wa mifugo ilibidi na yeye anyooshe mikono kuku wote walikufa.

Rafiki yangu moja akanipeleka kwenye biashara nyingine, hiyo biashara inataka uwekeze hela nyingi kama milioni 30 kuendelea ndio utaona faida, nikawekeza kwenye hiyo biashara, mwaka wa kwanza sikupata kitu nikasema hapa nlikuwa nnatafuta uzoefu, mwaka wa pili bado sikupata faida yoyote ile, lakini wakati huo wengine wanapata faida na mafanikio yao yanaonekana wazi wazi.

Naombeni ushauri, kwa sasa sina pesa mtaji, zile IST niliuza ili kuongezea mtaji kwenye biashara ambayo nilitegemea ingenitoa lakini haikuwa hivyo. Naombeni Ushauri ndugu zangu.

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
Pole sana. Hapa naona kuna bad planning with a combination of unfortunate events camouflaged in wrong believes! Mchawi wako ni mawazo yako mwenyewe. Hujalogwa lolote ila imani yako ndiyo imekuloga. Siku zote binadamu akikwama kimaisha jambo la kwanza kufanya ni kukimbilia kuangalia kitu kilichomkwamisha nje ya nafsi (utendaji) wake. Hapa ndipo kosa huanza kuzaa makosa, na makosa yanazaa makosa zaidi na zaidi. Kwa mfano wewe umeshaona kuwa masahibu yako ni kwa sababu ya kulogwa. Hili litakufanya uendelee kufanya makosa kwa kila kitu utakachoamua kukifanya kwa sababu hujataka kukubali kuwa wewe ndiyo chanzo cha kukwama ili ujirekebishe.
 
Pole sana. Hapa naona kuna bad planning with a combination of unfortunate events camouflaged in wrong believes! Mchawi wako ni mawazo yako mwenyewe. Hujalogwa lolote ila imani yako ndiyo imekuloga. Siku zote binadamu akikwama kimaisha jambo la kwanza kufanya ni kukimbilia kuangalia kitu kilichomkwamisha nje ya nafsi yake. Hapa ndipo kosa huanza kuzaa makosa, na makosa yanazaa makosa zaidi na zaidi. Kwa mfano wewe umeshaona kuwa masahibu yako ni kwa sababu ya kulogwa. Hili litakufanya uendelee kufanya makosa kwa kila kitu utakachoamua kukifanya kwa sababu hujataka kukubali kuwa wewe ndiyo chanzo cha kukwama ili ujirekebishe.
Sawa mkuu

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Unaposema akiba akiba unayoweka huioni kwamba inavapour au??
Yaani umeweka pesa mpesa, tigo pesa au benki, mwisho wa siku huikuti??

Kwenye kuku usimamizi wako ukoje, kwa mimi nadhani hakuna uchawi ni vile tu kipindi uko job hukuona mapungufu kwakua mshahara ulikuweka mjini na faida ya hiyo miradi hukuihitaji sana kama unavyoihitaji sasa.
 
Unaposema akiba akiba unayoweka huioni kwamba inavapour au??
Yaani umeweka pesa mpesa, tigo pesa au benki, mwisho wa siku huikuti??

Kwenye kuku usimamizi wako ukoje, kwa mimi nadhani hakuna uchawi ni vile tu kipindi uko job hukuona mapungufu kwakua mshahara ulikuweka mjini na faida ya hiyo miradi hukuihitaji sana kama unavyoihitaji sasa.
ni ngumu kuelewa kama hayajakukuta

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Sitaki niseme yalionifika lakini miaka 3 nyuma nimekutana na mambo mengi tu. Hasa kwenye kipato na biashara imeyumba sanaa. Nilichofanya kila nikipata hela natoa sadaka kwa mwezi naweza toa sadaka hata ya 100,000. Mwenyezi Mungu anapokupa neema yake, nawe toa sadaka kwa ajili yake.
 
Kuna kipindi chaa kushuka, unapigika mpaka laki unaipata kwa manati, ukivuka hapo utatoboa mazima. Hizi ni ups and down za maisha na hata ukiroga kuondoa mikosi utapata nafuu ya mda kisha unarudi mle mle so vumilia uvuke hicho, kipindi kesho ni nzuri
 
Back
Top Bottom