Naombeni ushauri nnahisi nimerogwa!

Naombeni ushauri nnahisi nimerogwa!

Sitaki niseme yalionifika lakini miaka 3 nyuma nimekutana na mambo mengi tu. Hasa kwenye kipato na biashara imeyumba sanaa. Nilichofanya kila nikipata hela natoa sadaka kwa mwezi naweza toa sadaka hata ya 100,000. Mwenyezi Mungu anapokupa neema yake, nawe toa sadaka kwa ajili yake.
Hili la sadaka nitalifanyia kazi, Japo hujasema, imeona mabadiliko yoyote baada ya kuanza kutoa sadaka?

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Kuna kipindi chaa kushuka, unapigika mpaka laki unaipata kwa manati, ukivuka hapo utatoboa mazima. Hizi ni ups and down za maisha na hata ukiroga kuondoa mikosi utapata nafuu ya mda kisha unarudi mle mle so vumilia uvuke hicho, kipindi kesho ni nzuri
Ni kweli mkuu

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Hicho ni kiburi, mwingine hakuwahi kuwa na investment hata ya 1m, wewe umekuwa na ya 30m, na zaidi.

Hivi ulifikiri ukichukua IST yako utapata hela zaidi ya dereva mwenye uzoefu? Umefeli mwenyewe tu.

Kuna wamama Muhimbili, na watoto wadogo wasio na hatia wanakufa, mbona watu wenginr hawafi?
Mkuu mbona kama una makasiriko?
 
Ushauri ni acha tamaa ya mafanikio ya haraka. Acha tamaa na kiraluralu cha kutaka kuwaoneshea watu umefanikiwa.
 
Wana Jamvi, Mwenzenu leo nimekuja nnaomba ushauri, Ni zaidi ya miaka miwili sasa mambo yangu hayaendi jinsi inavyopaswa mpaka inanipelekea kuhisi kwamba inawezekana kuna kitu hakipo sawa.

Mwaka 2020 nikiwa niko kwenye ajira, kwenye kitengo muhimu, mtu anayetegemewa, mwenye record nzuri kazini, performance nzuri lakini nikachaguliwa kuwa miongoni mwa wanaopaswa kupunguzwa na ofisi kwa kigezo kuwa kampuni haifanyi vizuri. kwa hiyo kazi ilikoma mwezi wa 6 mwaka 2020.

wakati huo sikuona shida sana kwa kuwa nlikuwa na miradi kadhaa iliyokuwa na uwezo wa kuniweka mjini, nlikuwa na Vi IST vyangu viwili vinafanya biashara ya kubeba abiria kupitia mtandao.

lakini pia nlikuwa nnafuga kuku wa mayai wasiopungua 1000, na shambani kwangu nlikuwa nimepanda mazao ambayo niliyategemea kibiashara ambayo ni mapapai na migomba. kwa bahati mbaya mapapai hayakuzaa kama ilivyo tarajiwa na migomba nayo haikufanya vizuri,

baada ya kazi kuisha nilimpunguza dereva mmoja nikaanza kuendesha mwenyewe gari moja ili kujiongezea kipato, cha kushangaza hata hesabu ya gari nikawa sifikishi, hela haionekani, ukiwa barabarani hela unaiona lakini ukija kwenye akiba hakuna hela, ukiangalia matumizi sio makubwa ila hela haionekani.

mwanzoni mwa mwaka 2021, picha linaanza kule shambani kuku waakanza kufa kila siku unaokota kuku 100 mpaka 200, ugonjwa haujulikani, kuku wana chanjo zote, wamepewa dawa zote, chakula ni kile kile Daktari wa mifugo ilibidi na yeye anyooshe mikono kuku wote walikufa.

Rafiki yangu moja akanipeleka kwenye biashara nyingine, hiyo biashara inataka uwekeze hela nyingi kama milioni 30 kuendelea ndio utaona faida, nikawekeza kwenye hiyo biashara, mwaka wa kwanza sikupata kitu nikasema hapa nlikuwa nnatafuta uzoefu, mwaka wa pili bado sikupata faida yoyote ile, lakini wakati huo wengine wanapata faida na mafanikio yao yanaonekana wazi wazi.

Naombeni ushauri, kwa sasa sina pesa mtaji, zile IST niliuza ili kuongezea mtaji kwenye biashara ambayo nilitegemea ingenitoa lakini haikuwa hivyo. Naombeni Ushauri ndugu zangu.

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
Ushauri wangu nenda kwa Mwamposa umerogwa ndg yangu.
 
Hili la sadaka nitalifanyia kazi, Japo hujasema, imeona mabadiliko yoyote baada ya kuanza kutoa sadaka?

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
Mkuu nakupa short story nimepitia mtihani mkubwa sana, hela kwangu na furaha tokea udogoni ndio maisha yangu.
Sasa kulitokea mambo flani ya kifamilia, sikutegemea maishani kama yangetokea. Nilipitia magumu sana sana furaha na hela ilipotea, mzee wangu akanambia mwanangu sadaka ni kinga ya mabaya.

Toa sadaka na muombe Mungu akulinde na akufanyie wepesi mambo yako. Mkuu hapa nilipo furaha ninayo tena sana tu hela inakuja kidogo dogo sio kama mwanzo.
Lakini najua kutokana na uchumi ulivyo ndio maana, ukichanganya najua nitafanya makubwa kuliko mwanzo. Ushauri wangu kwako toa sadaka unapo toa sema nia yako ya kutoa sadaka hio.
 
Mkuu nakupa short story nimepitia mtihani mkubwa sana hela kwangu na furaha tokea udogoni ndio maisha yangu. Sasa kulitokea mambo flani ya kifamilia sikutegemea maishani kama yangetokea. Nilipitia magumu sana sana furaha na hela ilipotea, mzee wangu akanambia mwanangu sadaka ni kinga ya mabaya. Toa sadaka na muombe Mungu akulinde na akufanyie wepesi mambo yako. Mkuu hapa nilipo furaha ninayo tena sana tu hela inakuja kidogo dogo sio kama mwanzo. Lakini najua kutokana na uchumi ulivyo ndio maana ukichanganya najua nitafanya makubwa kuliko mwanzo. Ushauri wangu kwako toa sadaka unapo toa sema nia yako ya kutoa sadaka hio.
Asante sana mkuu

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
 
Hili la sadaka nitalifanyia kazi, Japo hujasema, imeona mabadiliko yoyote baada ya kuanza kutoa sadaka?

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
Eneo hilo la sadaka ni MUHIMU sana mkuu usidharau wala usisahau hapo ndipo baraka zako zilipo mkuu haiwezekani uwe na mtaji wa 30ml nk. Afu usitoe sadaka mkuu ni kosa kubwa sana unajua matajiri wengi wanatoa sana sadaka ndio mafanikio yao hukua zaidi.
 
Sijaelewa mkuu, nieleweshe zaidi, nipo tayari kukusikiliza

Sent from my SM-M135FU using JamiiForums mobile app
Maoni yangu madogo
Biashara ya nafaka ni biashara nzuri sana ukiwa na mtaji mkubwa kama huo wako unapata urahisi wa kuzungusha
Nina uzoefu na mchele
Unaweza kununua mpunga ukaja kukoboa na kuuza mchele au unaweza tu kununua na mchele na kuuza
Soma soko la eneo ulilopo wanakula zaidi mchele gani bei zao utapata pa kuanzia
Kwa kipindi hiki mchele ipo ni fursa ukiwa na mtaji
 
Back
Top Bottom