Naombeni ushauri nimfanye nini mdogo wangu?

Naombeni ushauri nimfanye nini mdogo wangu?

Watu na waume zao halafu wanataka kulelewa watoto wao. Mtoto alelewe na wazazi wake hata kama atakuwa anakula bamia TDS kuliko kulelewa na mtu mwingine hata kama atakuwa anakula mboga saba TDS.
Kibaya zaidi wanaendelea kufyatua zaidi
 
Mitoto kumi ndani ya nyumba lazima familia ilaanike kwa umasikini.

Huwa naitizama familia moja ina watoto ishirini. Watoto kumi wa bi mkubwa na watoto kumi wa bi mdogo.

Wameshakuwa watu wazima na wao wamezaa watoto wao pia. Familia imekuwa na wajukuu zaidi ya sitini.

Vitoto vitoto vingi kama utitiri. Vingine hujui hata vimezaliwa saa ngapi. Kila siku watu wanaingia leba asubuhi na jioni!

Wote wanaishi kwenye boma la matope lenye vijumba vitatu vya kuzunguka.

Umasikini, dhiki, njaa, kwashakoo! Doooohh!!

Hapana kabisa.
Hahah watu wa familia kama hio unayoisema niwe mkweli hata siwaoneagi huruma kabisa kwa sababu wao wenyewe hawajionei huruma na umaskini wao.

Acha wapambane tu na hali yao.
 
Ukoo wa kimasikini[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji28]
Hahah umaskini ni wa kupambana nai kwa hali yoyote ile from family level mpk huko kwny ukoo kwa ujumla.

Sasa kumuendekeza mtu ambae anajifanya yeye ni kidume cha mbegu kinazalisha tu ovyo ovyo ni ujinga sana.
 
Wakuuu habari poleni na pirika pirika ,
Nahitaji msaada kutoka kwenu wa kimawazo maana sasa naelekea kuvunja uduñgu na mdogo wangu kwa tabia zake ambazo hazibadiliki na wala hashituki kabisa

Nianze na historia
Kwetu tumezaliwa watatu wote ni wakiume ,mkubwa ni mimi halàfu anafata dogo ambaye naona kama ni kivuruge , na mdogo wetu wa mwisho ni daktari yupo dodoma

Kwa sasa mimi naishi na mama yetu mzazi ambaye ni mgonjwa kapooza nusu upande na baba alifariki mm nikiwa na miaka 5 mdogo wangu akiwa na miaka 3 na mdogo wetu wa mwisho miezi ,4

Kinachonifanya nije kwenu wanajukwaaa huyu dogo amekuwa na tabia ya kuwapa mabinti mimba halafu haadumii......mpk sasa anajumla ya watoto nane ...kila mmoja ana mama yake na watoto wengine wameletwa kwa bibi yao ambaye ni mama yangu sasa familia imekuwa kubwa kwa upande wangu ,kutokana na mm kuwa na watoto wawili wa mwanamke mmoja tulioana tukaachana sasa kuna timu ya watoto siti

Kinachonitia hasira huyu dogo kaanza kazi mwaka 2009 , lakini huwa hhaudumiii watoto wake kwa chochote ,kila siku hana hela hela wakati basic salary yake ni laki 7 na maana yupo TGTS D ,

Kinachonifanya niwe njia panda ni mama kila dogo anapofanya makosa mama naona kama anamkingia kifuu mwaka jana alisingizia kazini kwao kuwa mama kafariki ,na walimu wenzake wakamchangia hela ...na pole kibao baada ya siku alizokuwa ameomba za likizo kwa ajili ya mazishi

kumalizika hakurudi kazini kama alivyokuwa amedanganya ilibidi mwalimu mkuu wake anipigie simu niliona habari ngeni na nilimkatalia pale pale kuwa mama hajafariki ila namuuguza na huyo mwalimu wako hajafika hata hospitali kumuona mama ,kwa hiyo akawa amewatapeli walimu wenzake kwa stayle hiyo

Mwka jana huo mwez wa tisa alikamatwa mwanza gest x akiwa na line za simu zaidi ya 40 na simu mbili akifanya ule utapeli wa tuma kwenye namba hii akadakwa na watu wa cyber crime mpk mkojo ulimtoka akajikojolea kwa uwoga hakuamini kabisa ..

..!! Nilipigiwa simu kwenda kumuona polisi nilikataa wala kwenda kumuwekea dhamana ....mama alilamika sana unamuacha mwenzako unataka afungwe gerezani hawa watoto wake utawasomesha kutokana na hali ya mam ilinilazimu kwemda kuyamaliza nikatoa kama laki 7 kumaliza kesi na dogo aliaahidi akitoka atanirejeshea baada ya mshahara lakini hakufanya hivyo

Kwa sasa nakaa na timu ya watoto wake wa nne yeye anakula bata huku akiendelea kuwapachika mimba mabinti wasiojielewa huko kishapu shy ,

Mama ananishinikiza niwasomeshe English medium hawa watoto wanne wa dogo , kama wangu wanavyosoma shule nzuri ...nilichomjibu mama nilimwambia baba yao anakaxi nzuri hajawahi kutuma hela ya matumizi hata watoto wakiugua ni mm huo mzigo mm siuwezi hela natoa wapi? Na mm pia nina malengo yangu mama kanuna kampigia mwanae simu

Kinachoniuzi zaidi ni leo mwanaye mmoja kagongwa na piki piki akitoka shule ...na mtoto kaumia vibaya na hakumkatia bima mpk sasa dogo nipo naye bugando ...namuuguza nimeshatumia laki 6 mpk sasa... kuanzia vipimo ,dawa ,wakati nampigia cm akadai tusimpeleke mtoto hospital ya bugado japo rufaa tunayo

yeye hana hiyo hela kama ni hivyo tumwambie aliyemgonga na aliyemgonga yupo polisi kakamatwa ....ikanilazimu nilipe tu hela dogo atibiwe kuokoa maisha yake ....nimepigia cm sasa hivi anasema nimtumie nauli aje kumuona mtoto kesho je nifanye nini kumnyoosha huyu dogo aweze kujitambua maana ni wa mwaka 1987

NIMNYOSHE VIPI HUYU ASINISUMBUE NA MM NIANGALIE MIPANGO YANGU

sent from HUAWEI
Uko mkoa ganii nije nikushauriiii just for 4 days

Sent using mt4 app
 
Ila research pia inasema watoto wengi wa pili huwa ni wa nje na ndio maana wengi wanatabia tofauti katika familia

Ila mkuu wewe ndo unalea ujinga
Yani hii huruma sijui mnaitoa wapi!?

Mtu anakazi, asomeshi watoto wake, na wewe unasomesha kisa mama ananuna, aisee!? Ili mradi yeye unamuhudumia, kwenye hilo mwache anune tu mkuu, huna dhambi
Utaratibu wangu uleule, kuambiana kupo, kusikilizana hakupo. Usikubali kupangiwa kila kitu
Kosa lako ni lile lile unafiki. Unauamia lakina unavumulia kwa kuogopa kuonekana mbaya
Usikubali kupangiwa, mpelekee wanae acha ujinga,
 
Mara nyingi watu wa aina yako hua ni wapole sana na wenye huruma kwa hiyo mama na mdogo wako wanatumia huo udhaifu wako kukufanya watakavyo,

Ushauri wangu tafuta mwanamke uoe kisha hama hapo kwa mama na watoto wako mkaishi kwenu, kabla hujaondoka mpeleke mdogo wako ustawi wa jamii (kama mdau alivyoshauri hapo) kwa ajili ya matunzo ya watoto wake au mpelekee watoto wake huko alipo (hii sioni kama inafaa sababu ni kwenda kuwatesa watoto),

Mzazi wako anaonesha ana ubaguzi wa wazi wazi, ukisikiliza sana huwezi fanya maendeleo na utawaumiza watoto wako.
Akiondoka hapo Nani atamlea huyo mama mgonjwa?
 
Hebu tuambie huyo Dr wa dodoma yeye anaishije?
 
Pesa hainunui utu kijana...huwezi mkimbia mama mgonjwa kisa kumuogopa huyo kivuruge!
Na unafki ni mbaya kuliko chochote, ukifanya kitu fanya kwa moyo wako na upendo wako na sio ufanye kitu ili watu wakuone unafanya hali ya kua moyoni unaumia na kusononeka.
 
Na unafki ni mbaya kuliko chochote, ukifanya kitu fanya kwa moyo wako na upendo wako na sio ufanye kitu ili watu wakuone unafanya hali ya kua moyoni unaumia na kusononeka.
Huyu ana haki ya kusononeka,una mgonjwa na watoto sita kweli jamani kwa maisha gani ya Sasa?Ndio maana anaomba ushauri...
 
Huyu ana haki ya kusononeka,una mgonjwa na watoto sita kweli jamani kwa maisha gani ya Sasa?Ndio maana anaomba ushauri...
Mgonjwa anafurahi akiona mwanae anayemuangalia akiumia ili asimkere mtoto mpendwa wake anayeishi mbali nae, kwa maisha haya haya anamshauri muangalizi wake awaingize wajukuu wa mtoto mpendwa wake international school.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom