Naombeni ushauri nimfanye nini mdogo wangu?

Naombeni ushauri nimfanye nini mdogo wangu?

KANYEGELO

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,304
Reaction score
5,011
Wakuuu habari poleni na pirika pirika ,
Nahitaji msaada kutoka kwenu wa kimawazo maana sasa naelekea kuvunja uduñgu na mdogo wangu kwa tabia zake ambazo hazibadiliki na wala hashituki kabisa

Nianze na historia
Kwetu tumezaliwa watatu wote ni wakiume ,mkubwa ni mimi halàfu anafata dogo ambaye naona kama ni kivuruge , na mdogo wetu wa mwisho ni daktari yupo dodoma

Kwa sasa mimi naishi na mama yetu mzazi ambaye ni mgonjwa kapooza nusu upande na baba alifariki mm nikiwa na miaka 5 mdogo wangu akiwa na miaka 3 na mdogo wetu wa mwisho miezi ,4

Kinachonifanya nije kwenu wanajukwaaa huyu dogo amekuwa na tabia ya kuwapa mabinti mimba halafu haadumii......mpk sasa anajumla ya watoto nane ...kila mmoja ana mama yake na watoto wengine wameletwa kwa bibi yao ambaye ni mama yangu sasa familia imekuwa kubwa kwa upande wangu ,kutokana na mm kuwa na watoto wawili wa mwanamke mmoja tulioana tukaachana sasa kuna timu ya watoto siti

Kinachonitia hasira huyu dogo kaanza kazi mwaka 2009 , lakini huwa hhaudumiii watoto wake kwa chochote ,kila siku hana hela hela wakati basic salary yake ni laki 7 na maana yupo TGTS D ,

Kinachonifanya niwe njia panda ni mama kila dogo anapofanya makosa mama naona kama anamkingia kifuu mwaka jana alisingizia kazini kwao kuwa mama kafariki ,na walimu wenzake wakamchangia hela ...na pole kibao baada ya siku alizokuwa ameomba za likizo kwa ajili ya mazishi

kumalizika hakurudi kazini kama alivyokuwa amedanganya ilibidi mwalimu mkuu wake anipigie simu niliona habari ngeni na nilimkatalia pale pale kuwa mama hajafariki ila namuuguza na huyo mwalimu wako hajafika hata hospitali kumuona mama ,kwa hiyo akawa amewatapeli walimu wenzake kwa stayle hiyo

Mwka jana huo mwez wa tisa alikamatwa mwanza gest x akiwa na line za simu zaidi ya 40 na simu mbili akifanya ule utapeli wa tuma kwenye namba hii akadakwa na watu wa cyber crime mpk mkojo ulimtoka akajikojolea kwa uwoga hakuamini kabisa ..

..!! Nilipigiwa simu kwenda kumuona polisi nilikataa wala kwenda kumuwekea dhamana ....mama alilamika sana unamuacha mwenzako unataka afungwe gerezani hawa watoto wake utawasomesha kutokana na hali ya mam ilinilazimu kwemda kuyamaliza nikatoa kama laki 7 kumaliza kesi na dogo aliaahidi akitoka atanirejeshea baada ya mshahara lakini hakufanya hivyo

Kwa sasa nakaa na timu ya watoto wake wa nne yeye anakula bata huku akiendelea kuwapachika mimba mabinti wasiojielewa huko kishapu shy ,

Mama ananishinikiza niwasomeshe English medium hawa watoto wanne wa dogo , kama wangu wanavyosoma shule nzuri ...nilichomjibu mama nilimwambia baba yao anakaxi nzuri hajawahi kutuma hela ya matumizi hata watoto wakiugua ni mm huo mzigo mm siuwezi hela natoa wapi? Na mm pia nina malengo yangu mama kanuna kampigia mwanae simu

Kinachoniuzi zaidi ni leo mwanaye mmoja kagongwa na piki piki akitoka shule ...na mtoto kaumia vibaya na hakumkatia bima mpk sasa dogo nipo naye bugando ...namuuguza nimeshatumia laki 6 mpk sasa... kuanzia vipimo ,dawa ,wakati nampigia cm akadai tusimpeleke mtoto hospital ya bugado japo rufaa tunayo

yeye hana hiyo hela kama ni hivyo tumwambie aliyemgonga na aliyemgonga yupo polisi kakamatwa ....ikanilazimu nilipe tu hela dogo atibiwe kuokoa maisha yake ....nimepigia cm sasa hivi anasema nimtumie nauli aje kumuona mtoto kesho je nifanye nini kumnyoosha huyu dogo aweze kujitambua maana ni wa mwaka 1987

NIMNYOSHE VIPI HUYU ASINISUMBUE NA MM NIANGALIE MIPANGO YANGU

sent from HUAWEI
 
Kwa huu mida ulioandika na jukwaa ulipoleta uzi kiukweli mzee umechanganyikiwa. Mtu kama mdogo wako ambaye ni mama's boy habadiliki mpaka mama akate sapoti yaani hata wewe ukisema unaachana naye kikubwa mama yupo basi kwake ni faraja na sababu ya kuendeleza ujinga.

Now hiyo siyo sababu ya wewe kujitwisha misalaba yake. Aanze kua responsible.

Mi kwetu wanaume tupo wawili na ninajitahidi sana kupanua ukoo target yangu ni watoto kuanzia nane nafikiri jamaa nimeshare naye huu mtazamo so pengine hazalishi kwa ubaya ni anaokoa ukoo.
 
Muitie bata,kama kuna bonge la party akupe company.
Mkifika huko mpe via za kutosha kisha ni vibao kwa kwenda mbere,unampa vibao unampatia glas ashushie,we usiwe na hasira,unamtandika huku unacheka tu km vile hamna kilichotokea.
Atakuelewa sana
 
1985, 1987 na 1991

Pole kwa hilo dhahama. Bro, ukiwa unatafuta ushauri kwa mambo mazito kidogo, upe uandishi wako uzito, sina hakika kama tuna matumizi na X kwenye kiswahili chetu, kidogo inasababisha ukakasi.

Tukirudi kwenye mada, HUNA utakaloweza kufanya kurekebisha hiyo tabia ya bwana mdogo wako. Ni tatizo common kwa kila familia, kuna mmoja kati yenu atakuwa fyatu tu na ndio unakuta anawekwa chini ya mbawa za wazee.

Mnaishi nyumba ya familia au kila mtu ana kwake? Hao watoto wanaletwa kwako kwa kigezo cha kuwapeleka kwa bibi au ndio wanaletwa kwa mlezi wa wana wewe?

Unachoweza kufanya, kama unao moyo huo; huyo bwana kuwa muajiriwa inatosha kusema kila anachofanya ana kielewa. Sasa wewe usielewe anachokifanya.

Aaargh, kila nikijaribu kukushauri cha kufanya, naona kabisa nitakuwa nakudanganya tu kwakuwa tunazo kesi kama hizo kwa kila uzao wa baba zetu, kuna mwingine anaingia 50 Dec, watoto wanalelewa na ma-grand na wadogo zake, ikiwa na yeye mwenyewe pia anakaa kwa mzee. Mwingine naye ana watoto wanane, kila mmoja na mama'ake, mwingine anaingia 4th floor hivi karibuni, hatujui anakoishi, kama ana kazi au hana, anajua kila nyumbani kwa ndugu, ndio jinsi tunavyokutana nae.

Hao wote ni kutoka kwa familia tofauti. Ila ni mara chache kukuta uzao wa pili unakuwa chenga, ama wa kwanza au wa mwisho.

Bro, we fanya unavyoona nafsi yako inakuelekeza kufanya, mi sihangaiki na mijitu ambayo inaweza kujitetea, watoto hawawezi kujitetea, wanakuhitaji ILA pia wema ukizidi uwezo, ni dhambi wanasema waumini.
 
Muitie bata,kama kuna bonge la party akupe company.
Mkifika huko mpe via za kutosha kisha ni vibao kwa kwenda mbere,unampa vibao unampatia glas ashushie,we usiwe na hasira,unamtandika huku unacheka tu km vile hamna kilichotokea.
Atakuelewa sana
Ugomvi wa ndugu sio mwepesi kama utamtia vibao
 
...Kamata peleka polisi wakakusaidie au mkodie njemba za maana wakamfundishe adabu...
 
Muitie bata,kama kuna bonge la party akupe company.
Mkifika huko mpe via za kutosha kisha ni vibao kwa kwenda mbere,unampa vibao unampatia glas ashushie,we usiwe na hasira,unamtandika huku unacheka tu km vile hamna kilichotokea.
Atakuelewa sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ugomvi wa ndugu sio mwepesi kama utamtia vibao
Nishafanya hiyo process dogo mpk leo akiniona anapiga magoti na kusali Sara ya bikira Maria ,hapo kabla Kanilaza nje tu.Nyumba yangu,funguo yangu pesa yangu aah siku hiyo tulisahauliana vizuri tu.
Alikula makofi mengi sana huku tunapiga story tu.
Heshima kanielewa sana
 
Kama wajumbe wengine welivyosema, kesi kama hizi kila familia zipo

Mimi binafsi nalea mtoto wa kaka yangu. Uyu dogo baba yake yupo mama yake yupo. Mwanzo alikua anaishi kwa Babu/bibi yake(wazazi wetu) alikua anapata shida ya kwenda kusoma mbali, mimi kwa huruma kwa uyu mtoto nikamchukua ili nimsomeshe pia kuwapunguzia mzigo wazazi wetu lakin wazazi wa uyu mtoto ni kama hawana habari nae.

Huyu dogo ana mdogo wake pia anaishi kwa bibi/babu yake(wazazi wetu) mwendo ndo huohuo blaza hana habari na wanae pia dizaini kama Mshua anamtetea Blaza ivi. Ni kweli blaza hana Kazi ya kueleweka lakini pia hajali kuhusu Watoto wake

Nije kwenye Kesi yako, kwakua dogo anajiweza ana kazi yake nzuri tu basi kila mmoja abebe mzigo wake, itoshe kusema wewe kulea mama yenu na watoto wako inatosha na yeye alee watoto wake. Kusanya watoto wake nenda nao kwa baba yao(mdogo wako) nenda kamwambie watoto wako hawa hapa walee wewe una majukumu mengi. Usijali malalamiko ya mama na umweleze Ukweli maza kua kila mmoja abebe mzigo wake mwenyewe. Ahsante
 
Mara nyingi watu wa aina yako hua ni wapole sana na wenye huruma kwa hiyo mama na mdogo wako wanatumia huo udhaifu wako kukufanya watakavyo,

Ushauri wangu tafuta mwanamke uoe kisha hama hapo kwa mama na watoto wako mkaishi kwenu, kabla hujaondoka mpeleke mdogo wako ustawi wa jamii (kama mdau alivyoshauri hapo) kwa ajili ya matunzo ya watoto wake au mpelekee watoto wake huko alipo (hii sioni kama inafaa sababu ni kwenda kuwatesa watoto),

Mzazi wako anaonesha ana ubaguzi wa wazi wazi, ukisikiliza sana huwezi fanya maendeleo na utawaumiza watoto wako.
 
Pole Sana..tafuta namna ya kumfanya huyo nduguyo ahudumie hao watoto.
 
Mm nakushauli, chukua familia yake mpelekeee huyo mama yako mwache akasiliike mpaka basi na ilibidi uweke kikao cha watu wanne,chukua mtu mmoja kutoka upande WA kiume, awe baba mdogo au shangazi,chukua ndugu upande WA kikeni awe mama mdogo au mjomba , umwite mdogo wako umkabidhi familia yake , ikishindikana nenda kwa mkugenzi zungumza nae mshahawa wake ukatwe nusu uingie kwako kwa ajili ya kulea watoto

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
mnao changia hii mada hakuna hata mmoja wa style hiyo?[emoji848]

broo nimekuelewa najirekebisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom