Daa pole sana mkuu. Nina mdogo wangu ambae nae kazaliwa mwaka huohuo 1987, kwa kweli alikua msumbufu sana na mtaani alishawaliza wengi kwenye nyumba zao.
Yeye hajazaa zaa nje kama huyu wako ila yeye alikua mwizi hatari lakini cha ajabu alikua anajutia tabia yake. Yaani akimaliza mishe yake ndio anajuta kwanini kafanya hivyo.
Lakini maisha yamemweka kwenye mstari saiv, baba na mama waliokua wanamtetea hawapo tena, na aliacha baada ya kuponea chupuchupu kwenye tairi la gari na petrol [emoji23].
Ni suala la muda tu huyo mdogo wako atanyooka tu. AFU cha ajabu kingine watoto wa dizaini hii ya usumbufu ndio wanaopendwa sana na wazazi.