Naombeni ushauri nimfanye nini mdogo wangu?

Naombeni ushauri nimfanye nini mdogo wangu?

Ile hela tuma kwenye namba hii kumbe ni mdogo wako?.

Ulivyopata taarifa za yy kushikwa na polisi wala usingemwambia bi mkubwa kwanza, ilibidi asote ndani kwa wiki kadhaa.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
Yaaani alinitia aibu mno sema tu niliwaza sana akionyeshwa kwenye tv habari hata mm kazin kwangu heshima itapungua na ukizingatia nipo wizara ya mambo ya ndani .......huyu hajifunzi kabisa

sent from HUAWEI
 
Kwanza kusanya vyeti vya kuzaliwa vya watoto wote na picha passport size zao kisha mchukue jamaa mpaka kwa mwajiri wake mwambie wewe ni kaka ake awafungulie bima za afya.Ikiwezekana hata mama yenu pia afunguliwe bima maana umesema ni m/kazi wa serikali.

Pili mshauri aoe kati hao wazazi wenzie ili amtunze na mama yenu.

Tatu au mshauri ajenge walau chumba sebule then akusanye watoto wale anaoweza kulea bila mama zao awalee.

Nne kama mna nyumba ya urithi na mama anaishi hapo mshauri kama kufanya hata uhamisho wa kikazi ahamie mkoa alipo mama ili familia yake huyo dogo ikae hapo.
 
Wakuuu habari poleni na pirika pirika ,
Nahitaji msaada kutoka kwenu wa kimawazo maana sasa naelekea kuvunja uduñgu na mdogo wangu kwa tabia zake ambazo hazibadiliki na wala hashituki kabisa

Nianze na historia
Kwetu tumezaliwa watatu wote ni wakiume ,mkubwa ni mimi halàfu anafata dogo ambaye naona kama ni kivuruge , na mdogo wetu wa mwisho ni daktari yupo dodoma

Kwa sasa mimi naishi na mama yetu mzazi ambaye ni mgonjwa kapooza nusu upande na baba alifariki mm nikiwa na miaka 5 mdogo wangu akiwa na miaka 3 na mdogo wetu wa mwisho miezi ,4

Kinachonifanya nije kwenu wanajukwaaa huyu dogo amekuwa na tabia ya kuwapa mabinti mimba halafu haadumii......mpk sasa anajumla ya watoto nane ...kila mmoja ana mama yake na watoto wengine wameletwa kwa bibi yao ambaye ni mama yangu sasa familia imekuwa kubwa kwa upande wangu ,kutokana na mm kuwa na watoto wawili wa mwanamke mmoja tulioana tukaachana sasa kuna timu ya watoto siti

Kinachonitia hasira huyu dogo kaanza kazi mwaka 2009 , lakini huwa hhaudumiii watoto wake kwa chochote ,kila siku hana hela hela wakati basic salary yake ni laki 7 na maana yupo TGTS D ,

Kinachonifanya niwe njia panda ni mama kila dogo anapofanya makosa mama naona kama anamkingia kifuu mwaka jana alisingizia kazini kwao kuwa mama kafariki ,na walimu wenzake wakamchangia hela ...na pole kibao baada ya siku alizokuwa ameomba za likizo kwa ajili ya mazishi

kumalizika hakurudi kazini kama alivyokuwa amedanganya ilibidi mwalimu mkuu wake anipigie simu niliona habari ngeni na nilimkatalia pale pale kuwa mama hajafariki ila namuuguza na huyo mwalimu wako hajafika hata hospitali kumuona mama ,kwa hiyo akawa amewatapeli walimu wenzake kwa stayle hiyo

Mwka jana huo mwez wa tisa alikamatwa mwanza gest x akiwa na line za simu zaidi ya 40 na simu mbili akifanya ule utapeli wa tuma kwenye namba hii akadakwa na watu wa cyber crime mpk mkojo ulimtoka akajikojolea kwa uwoga hakuamini kabisa ..

..!! Nilipigiwa simu kwenda kumuona polisi nilikataa wala kwenda kumuwekea dhamana ....mama alilamika sana unamuacha mwenzako unataka afungwe gerezani hawa watoto wake utawasomesha kutokana na hali ya mam ilinilazimu kwemda kuyamaliza nikatoa kama laki 7 kumaliza kesi na dogo aliaahidi akitoka atanirejeshea baada ya mshahara lakini hakufanya hivyo

Kwa sasa nakaa na timu ya watoto wake wa nne yeye anakula bata huku akiendelea kuwapachika mimba mabinti wasiojielewa huko kishapu shy ,

Mama ananishinikiza niwasomeshe English medium hawa watoto wanne wa dogo , kama wangu wanavyosoma shule nzuri ...nilichomjibu mama nilimwambia baba yao anakaxi nzuri hajawahi kutuma hela ya matumizi hata watoto wakiugua ni mm huo mzigo mm siuwezi hela natoa wapi? Na mm pia nina malengo yangu mama kanuna kampigia mwanae simu

Kinachoniuzi zaidi ni leo mwanaye mmoja kagongwa na piki piki akitoka shule ...na mtoto kaumia vibaya na hakumkatia bima mpk sasa dogo nipo naye bugando ...namuuguza nimeshatumia laki 6 mpk sasa... kuanzia vipimo ,dawa ,wakati nampigia cm akadai tusimpeleke mtoto hospital ya bugado japo rufaa tunayo

yeye hana hiyo hela kama ni hivyo tumwambie aliyemgonga na aliyemgonga yupo polisi kakamatwa ....ikanilazimu nilipe tu hela dogo atibiwe kuokoa maisha yake ....nimepigia cm sasa hivi anasema nimtumie nauli aje kumuona mtoto kesho je nifanye nini kumnyoosha huyu dogo aweze kujitambua maana ni wa mwaka 1987

NIMNYOSHE VIPI HUYU ASINISUMBUE NA MM NIANGALIE MIPANGO YANGU

sent from HUAWEI
Wachukue watoto wake wote ukawabwage kwake
 
Kwa huu mida ulioandika na jukwaa ulipoleta uzi kiukweli mzee umechanganyikiwa. Mtu kama mdogo wako ambaye ni mama's boy habadiliki mpaka mama akate sapoti yaani hata wewe ukisema unaachana naye kikubwa mama yupo basi kwake ni faraja na sababu ya kuendeleza ujinga.

Now hiyo siyo sababu ya wewe kujitwisha misalaba yake. Aanze kua responsible.

Mi kwetu wanaume tupo wawili na ninajitahidi sana kupanua ukoo target yangu ni watoto kuanzia nane nafikiri jamaa nimeshare naye huu mtazamo so pengine hazalishi kwa ubaya ni anaokoa ukoo.
Anaokoa/unaokoa ukoo kutokana na nini? Du! Kweli watu tunatofautiana
 
Mm nakushauli, chukua familia yake mpelekeee huyo mama yako mwache akasiliike mpaka basi na ilibidi uweke kikao cha watu wanne,chukua mtu mmoja kutoka upande WA kiume, awe baba mdogo au shangazi,chukua ndugu upande WA kikeni awe mama mdogo au mjomba , umwite mdogo wako umkabidhi familia yake , ikishindikana nenda kwa mkugenzi zungumza nae mshahawa wake ukatwe nusu uingie kwako kwa ajili ya kulea watoto

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
Hii ya mkurugenzi nzuri sanaaa
Sema inabdi wafanye hao wanawake aliozaa nao
 
Wakuuu habari poleni na pirika pirika ,
Nahitaji msaada kutoka kwenu wa kimawazo maana sasa naelekea kuvunja uduñgu na mdogo wangu kwa tabia zake ambazo hazibadiliki na wala hashituki kabisa

Nianze na historia
Kwetu tumezaliwa watatu wote ni wakiume ,mkubwa ni mimi halàfu anafata dogo ambaye naona kama ni kivuruge , na mdogo wetu wa mwisho ni daktari yupo dodoma

Kwa sasa mimi naishi na mama yetu mzazi ambaye ni mgonjwa kapooza nusu upande na baba alifariki mm nikiwa na miaka 5 mdogo wangu akiwa na miaka 3 na mdogo wetu wa mwisho miezi ,4

Kinachonifanya nije kwenu wanajukwaaa huyu dogo amekuwa na tabia ya kuwapa mabinti mimba halafu haadumii......mpk sasa anajumla ya watoto nane ...kila mmoja ana mama yake na watoto wengine wameletwa kwa bibi yao ambaye ni mama yangu sasa familia imekuwa kubwa kwa upande wangu ,kutokana na mm kuwa na watoto wawili wa mwanamke mmoja tulioana tukaachana sasa kuna timu ya watoto siti

Kinachonitia hasira huyu dogo kaanza kazi mwaka 2009 , lakini huwa hhaudumiii watoto wake kwa chochote ,kila siku hana hela hela wakati basic salary yake ni laki 7 na maana yupo TGTS D ,

Kinachonifanya niwe njia panda ni mama kila dogo anapofanya makosa mama naona kama anamkingia kifuu mwaka jana alisingizia kazini kwao kuwa mama kafariki ,na walimu wenzake wakamchangia hela ...na pole kibao baada ya siku alizokuwa ameomba za likizo kwa ajili ya mazishi

kumalizika hakurudi kazini kama alivyokuwa amedanganya ilibidi mwalimu mkuu wake anipigie simu niliona habari ngeni na nilimkatalia pale pale kuwa mama hajafariki ila namuuguza na huyo mwalimu wako hajafika hata hospitali kumuona mama ,kwa hiyo akawa amewatapeli walimu wenzake kwa stayle hiyo

Mwka jana huo mwez wa tisa alikamatwa mwanza gest x akiwa na line za simu zaidi ya 40 na simu mbili akifanya ule utapeli wa tuma kwenye namba hii akadakwa na watu wa cyber crime mpk mkojo ulimtoka akajikojolea kwa uwoga hakuamini kabisa ..

..!! Nilipigiwa simu kwenda kumuona polisi nilikataa wala kwenda kumuwekea dhamana ....mama alilamika sana unamuacha mwenzako unataka afungwe gerezani hawa watoto wake utawasomesha kutokana na hali ya mam ilinilazimu kwemda kuyamaliza nikatoa kama laki 7 kumaliza kesi na dogo aliaahidi akitoka atanirejeshea baada ya mshahara lakini hakufanya hivyo

Kwa sasa nakaa na timu ya watoto wake wa nne yeye anakula bata huku akiendelea kuwapachika mimba mabinti wasiojielewa huko kishapu shy ,

Mama ananishinikiza niwasomeshe English medium hawa watoto wanne wa dogo , kama wangu wanavyosoma shule nzuri ...nilichomjibu mama nilimwambia baba yao anakaxi nzuri hajawahi kutuma hela ya matumizi hata watoto wakiugua ni mm huo mzigo mm siuwezi hela natoa wapi? Na mm pia nina malengo yangu mama kanuna kampigia mwanae simu

Kinachoniuzi zaidi ni leo mwanaye mmoja kagongwa na piki piki akitoka shule ...na mtoto kaumia vibaya na hakumkatia bima mpk sasa dogo nipo naye bugando ...namuuguza nimeshatumia laki 6 mpk sasa... kuanzia vipimo ,dawa ,wakati nampigia cm akadai tusimpeleke mtoto hospital ya bugado japo rufaa tunayo

yeye hana hiyo hela kama ni hivyo tumwambie aliyemgonga na aliyemgonga yupo polisi kakamatwa ....ikanilazimu nilipe tu hela dogo atibiwe kuokoa maisha yake ....nimepigia cm sasa hivi anasema nimtumie nauli aje kumuona mtoto kesho je nifanye nini kumnyoosha huyu dogo aweze kujitambua maana ni wa mwaka 1987

NIMNYOSHE VIPI HUYU ASINISUMBUE NA MM NIANGALIE MIPANGO YANGU

sent from HUAWEI
mchape viboko 12
 
hiyo ni migogoro asilia ya familia nyingi za Kiafrika.......mie nlikuwa na binamu yangu we grow together...like braza's......aisee kanipa taabu huyu ngamia.......ila alikoma kabisa.....alikuwa ni mkopaji na vurugu za pombe......kila akiwekwa ndani naenda kumtoa......mama ndio wa kwanza " kweli umetulia na nduguyo yupo ndani.......last time hakuna alijua yuko wapi......Mungu anisamehe........alikamatwa kwa kosa la kipumbavu sana.....nikawa wa kwanza kupata taarifa.....niliwahi kituoni......nikamwambia mkuu wa kituo....huyu braza akae mpaka ijumaa....apelekwe mahakama.....then no dhamana.....akalinuse gereza for 2 weeks.......aisee amenyooka kabisa......tena ni mwinjilist wa kujitegemea......yaani katulia na familia iko njema......mpaka leo haamini nilichimfanyia.....ila ilisaidia.....
Bro hili lako bana....kwanza pole kwa kumuuguza mama.......usichoke.....huyo dogo mpeleke ustawi wa jamii....50% ya mshahara itakuja kwako iwalee watoto.....umiza kichwa as man.......mnyooshe....
 
Mkuu situation zako zipo kama zangu
Pole sana. Nimegundua wewe unampenda bi mkubwa halafu uyo mdogo wako mpuuzi ndio kipenzi cha bi mkubwa. Wasielewa hio situation inaudhi mno,maana hamna kitu atafanya bi mkubwa asikitetee na asikupe majukuku yasiokuhusu kisa tu amfurahishe kipenzi chake... na ukikataa kesi unaambiwa una roho mbaya halafu bi mkubwa ananuna kweli kweli na presha Juu mimi Mungu anisaidie uzazi wangu nisiwepo na nnaempenda sana maana najua how it feels kwa wengine kukandamizwa
 
Ili usikose waendeleza jina la ukoo
Watoto 8 minimum ndo jamaa amepanga! Kwani ukiwa na watatu (mawazo yangu) si inatosha kuendeleza jina? Labda ana ukwasi wa kutosha ingawaje kwangu mimi isingekuwa kigezo cha kuwa na watoto wengi hivyo.
 
M naona ubadilike wewe,acha kumbembeleza
Ushafanya kosa usirudie kupokea watoto wake
2.hao watoto so lazima waletwe kwako mda ndugu mwingine kama vipi wapeleeni hko
3.we usikubali kumsaidia majukumu yake wakati uwezo anao,wakati anakatika ulikuepo?kama vipi pelekeni ustaw wa jamii akahadumuie kwa lazima pia hyo n kazi ya wanawake zake na yeye ,unachokosea n kuendelea kuwachekea wakati mtu mwenyewe hata haaprexiate unachomfanyia ,
 
Epuka sana kukaa ndugu mkoa mmoja utajuta kuzaliwa nikutegemeana chuki na lawama kwenda mbele na kuzalisha maelewano hafifu
 
Peleka ustawi nahisi utasaidika. Mamlaka ikimkalia koooni, atakuwa na mtazamo mwingine.
Fanyia kazi huu ushauri atiwe adabu...

Abanwe kisawa sawa...

Alafu shaka nyie mtakuwa WAGOGO...
 
Beba watoto wake nenda kambwagie huko anakoishi(kishapu),mnatengeneza ukoo wa watu maskini tu hapo.
Pia hii nayo n nzuri mpelekee hko anakokaa hyo so kazi yako ya kulea ili hali babayao yupo hatukatai kusaidia kupo ila so kwa wakati huu,ye na wanawake zake wapambane mpelekee watoto wake hko kishapu
 
Huyo dogo hakujua gharama ya kuzlisha ovyoo, hii kesi Peleka ustawi wa jamii.
 
Mpelekee wanawe atunze mwenyewe
Hapo tatizo unalikumbatia wwe mkuu
Bi mkubwa naye pia analea tatizo kwa kumkingia kifua mara kwa mara
Mkuu pole kwa kutumia hizo pesa kwa ajili ya matibabu ila ungejiongeza awali bima ingesaidia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom