Naombeni ushauri, nimepigwa na butwaa

Naombeni ushauri, nimepigwa na butwaa

Mwenyew nashangaa! Why anaangalia zaid hela na biashara za maria?
Moja kat ya sifa nzur ninayopenda mwanamke yoyote awe nayo ni utafutaji wa hela mwanamke anakuwa anavutia zaid kama haremb mwandiko kwenye haya maisha kiukweli maria kawa mtafutaji sana mpk utadhani sio yeye anajua kuongoza biashara zake vema
 
Mkuu mimi nadhani Maria ndo mke sahihi kwanza unamfahamu pili ni mtu wa kusamehe, Alikufuma akakusamehe ila alipokosea yeye wewe ukamuacha lakini bado akakatafuta tena akiwa hana hata shida ya pesa zako.
Na kama unataka kutapeliwa na wadada wa mjini basi endelea kuhudumia uyo mwana chuo wako, mana shida zake za chuo zikiisha tegemea kukanwa hapo.
Ludi kwa maria wako John
 
Mambo ya nani uishi naye maisha yako yote sio mambo ya kuombea ushauri JF. Funga na umuombe Mungu akuoneshe - shetani anaipenda sana hiyo sekta - anajua akikuvuruga hapo tu ameua ndege wengi sana kwa jiwe moja.
 
Habarini za mihangahiko wakubwa zangu najua wengi ni wakubwa kwangu waliomo humu ndani kwa hiyo naombeni mnisaidie Hili suala linalolisumbua sana akilini katika haya maisha kiasi cha kunipa stress.

Nawasihi mnipe ushauri ambao utanisaidia ndugu yenu na wala msichukulie kama ni ishu nyepesi kiukweli imeniumiza sana Inaweza kukutokea na wewe.

Ipo hivi mwanzoni kipindi nasoma huko Singida Mwenge secondary kisha nikapiga chuo flani cha sanaa nikapata kazi mbeya tayari nilianzaga uhusiano na binti flani wa kinyaturu jina lake Maria alikua mrembo sema tulikuja kugombana nae na hii ni mda mfupi baada ya kumchukua toka kwao na kwa kuwa kwao maisha hayakuwa mazuri mama ake alimkubalia tu aje Mbeya nimtafutie kazi pia niishi naye na kumleta mbeya nilipokuwa napiga kazi ishu yenyewe tuliokwaruzana.

ilikuwa hivi nilimtafutia kazi ndio lakini kuna siku alinikamata namchepuko wangu flani wa chuo flan pale mbeya akaniuliza kwann unanifanyia hivi John kwangu hupat nini kiukweli nilimjibu vibaya nilimwambia "kwanza we nshakutaftia kazi ukiamua kapange chumba chako mwanamke mwenyewe mshamba na haupendezi " huyo maria alilia sana yaani sijui kwanini nilijitoa ufahami nikamjibu hivyo kana kwamba nilikuwa sina mapenz naye bali kumchezea.

Ni matatizo ya dunia nilifanya kosa. Tukaendelea kuwa wapenzi lakini kuna ishu nyingine tena ikatokea na hii msala ulikuwa kwake nilikamata simu yake anachat na wanaume wengine na charting zipo katika mkao wa kimahusiano ye alinijib shortcut kwamba anachat nao hajawah ku sex nao me nikaona huyu ananiletea za mazoea ya kiniaje kwani me boya niamin kwamba awe na mahusiano na mtu alafu asigegedwe nikaamua ku mshit nikamwacha Mbeya me nikaja Dar nikahamia kikazi na nikavunja mawasiliano naye ingawa kuna kipindi tulishawahi hadi na kuwa na mipango ya ndoa nadhani tulivoachana ye aliumia zaidi kwasababu mimi nilishakuwa wa mjini hapa Tanzania napenda kujichanganya nikaamua kushit mipango yote na mawasiliano na ndugu zao kimsingi nilibadilisha line.

Sasa nimekuja Dar kwenye kazi zangu za sanaa bahati nzuri nikapata office ipo mjini nikapata na mdada mzuri tu na yeye ni mwanafunzi wa chuoni semister ya mwisho ametokea kunizimikia sana na kama unavojua umri unaenda na Dar starehe nyingi kwa huyu mtoto wa chuo nilikuwa nipo mbioni nafanya mipango ya kutambulishana ndoa na kaharusi sio mbaya tungefanya hata mwakani lakini huyu msichana wa mwanzo Maria amebadilika sana kimtizamo amekuwa na akili sana ya maisha toka nimwache kwenye kazi yake Mbeya.

Maria week kama mbili ziizopita amenitafuta kwa jamaa yangu flani akapewa namba akatoka Mbeya a kaja mpaka Dar na ndege, alinitumia meseji kuwa nipo Dar tukutane sehem nikaona sio mbaya labda ana ujumbe mzito nilivokutana nae amenipa maneno kuntu na ya uchungu sana kiasi kwamba nimepagawa huruma imenishika moyo umekuwa mzito amenambiaa tafadhal John me wewe toka zamani tunapendana sa kwann tumeachana kwa sababu hazina msingi.. Maria ye umri wake ni kama tupo sawa huyu wa chuo nimempita miaka minne

Kiukweli alafu huyu Maria amekuwa mzuri sana siku hizi anavaa vizuri anafanya biashara zake amekuwa na maendeleo ananiambia anachotaka me na ye tufunge ndoa akanambia binadamu hajakamilika kuna vingi tuna weka mistake tusamehane akanambia ukweli alikuwa na mahusiano na wanaume kama wawili pale mbeya na mmoja ni rafiki yangu mfanyabiashara pale Mbeya basi baada ya kukiri makosa yake akaniambia tusamehane yote alafu tufanye mipango ya harusi na kwamba binadamu ni kiumbe dhaifu na kwamba wote ukicheki tulikosea hivyo basi ana haki ya kusamehewa na anachoangalia mbele kwa sasa ni mimi and yeye tujenge familia bora yenye maendeleo akanipa simu niongee na mama yake mama ake akanisihii kuwa tuache utoto tumeshakuwa wakubwa tusamehane.Dondoo zile za maria na mamake zimeniumiza sana kihisia nimejikuta nalia karibia ucku kucha .

Lakini dah me sina time nipo busy tayari na huyu msichana wangu mpya ambaye yupo college hapa Dar mtoto ni wa kichaga mama ake mkubwa anayeishi nae kawalea malezi mazuri. Kwa kuwa na moyo mmoja basii nishaamuaga kuwa na mpenzi mmoja sasa nashindwa kuamua nichague yupo na ndipo lilipo hitaji langu la msaada wenu wa huku Dar hatuna muda mrefu naye ananipenda sema pia mtoto wa huku Dar naye ananiheshim sana yupo kwa wazaz wake ugali dona maisha yanandelea.

Naogopa huyu wa Dar ni tamuumiza sanasana anamiamni namsaidia vitu vingi chuo naanzaje kumuacha Maria ndani ya moyo wangu ni jina kubwa kuzid lowaza. Natetemeka kila nikikumbuka Saut yake akiniambia kuwa ye ni mtu mzuri na maalum kwa ndoa yangu nisikosee na ukicheki Maria yuko bomba siku hizi kazi yake inampatia hela ni anapenda mafanikio.
Ifahamike kuwa sio kweli ninachokipendea kwa maria ni pesa bali ni jinsi ana vo hustle kutwa kuzitafuta, hata hivo pesa aliyonayo sio kubwa sana ila kwa muda mfupi alioanza kazi na hasa ukiangalia ni mtoto wa kike kwa kwel ana hitaji pongezi.. Kama huku Dar ningepata mwanamke wa ajabu (sifa zao unazijua) nisingejiuliza mara mbili ningemchukua mtoto maria jumla ila ugumu ni kuwa hata huyu mtoto wa Dar anajitahid kunipenda na kunionyesha ana iman asilimia Mia kuwa akimaliza shule lzm nimuoe japo mipango yote sikuwah kumwmbia dadake naye tunaheshimiana nae anasema tufunge harus mapema atatusapot kimtindo Naombeni kujua yupi hapo ni mke wangu sahihi. Maria ana leta hizi mambo najikuta nmuonea huruma hili jambo linatengeneza history kubwa ya mapenzi lazima iwe history nzuri yenye faida ila naogopa kumuumiza mmoja wao mawazo mpaka najikuta nimekuwa mlevyi nakunywa pombe nyingi.

Sio sinema wala sio ndoto bali nimeshindwa kuamua na kama mnavojua suala la ndoa sio la kujaribu na hitaji kuweka akili na hisia sawa ili nisibugi
Ushauri wangu kwako bakia na huyo dada wa college maria muombe radhi na umwambie yameisha ila tusiendeleze tena mapenzi kwani sio vema kuwaumiza madafa 2
 
Ushauri wangu kwako bakia na huyo dada wa college maria muombe radhi na umwambie yameisha ila tusiendeleze tena mapenzi kwani sio vema kuwaumiza madafa 2
Ushaur wako umeenda shule weng waliniambia nifanye hivo
 
Utoto unakusumbua
Watu km nyie hamkosekan mnadhani wenzenu hatuishi kwenye hii dunia ipo siku yatakutokea na u kubwa wako huo hautakuja kuamin
Eti utoto?? Hio singo ya kiboya km hujailewea post panda bodaboda goo sio lzm kukoment
 
Wewe jamaa ni mshamba wa mapenzi,maneno mengi mara maria,mara dar wewe ni malay.......be careful ukimwi upo.
 
Na huyo wa chuo yupo na ww kwa sababu una kaz na unamsaidia

Amin ktk hilo
Wanawake wa chuo nani asyewajua

Ila hata ukirudi kwa maria nakushauri acha utoto

Michepuko syo dili
 
maria maria maria...,,angala moyo wako upo wapi no matter of how she hustle,,unaweza fikiri maria ni mtafutaji kumbe anahongwa
 
Watu km nyie hamkosekan mnadhani wenzenu hatuishi kwenye hii dunia ipo siku yatakutokea na u kubwa wako huo hautakuja kuamin
Eti utoto?? Hio singo ya kiboya km hujailewea post panda bodaboda goo sio lzm kukoment
Umepanik? Kunya rungu
 
Sasa ishu inakua ngumu wapi huyu wa chuo ananipenda sana kila siku ananisisitizia nisije kumtenda kiukweli na yeye ametulia ingawa sio mtafutaji kama alivo maria.. Nashukuru mungu huyu wa chuo na ye huwa ana nidham na hela ananikumbushaga mambo muhim ya kufanya ili nipate maendeleo ni mshaur mzur tu

Usituchoshe badili dini, wabadili na hao wachumba zako, oa wote....kesi imeisha
 
Kwahiyo wewe jamaa unatakaje Labda maana sikupati,kuna waliopendekeza oa Maria umesema unamwonea huruma mwanachuo kwakua anaheshima katulia naliomba usimtende haya wengine wamesema oa mwanachuo unasema akili Yake haijakua ama si mtafutaji kama Maria sasa usaidiwaje? Pendekezo langu waache wote mpaka pale utakapo kua kiakili nakujua nini unakitafuta kwa mwanamke ndo uoe sio hizi blah blah Mara huyu hivi Mara yule hivi unatuchosha bana.
 
Ok, kwa ninavyo ona hapo huyu maria yupo matured zaidi kuliko wa chuo, huyu maria anajua ndani na nje ya maisha na mahusiano, lakini huyu wa chuo bado mgeni wa maisha na mapenzi pia, inawezekana huko mbele mkaja mkazinguana kutokana na ugeni wake
 
Ok, kwa ninavyo ona hapo huyu maria yupo matured zaidi kuliko wa chuo, huyu maria anajua ndani na nje ya maisha na mahusiano, lakini huyu wa chuo bado mgeni wa maisha na mapenzi pia, inawezekana huko mbele mkaja mkazinguana kutokana na ugeni wake
Nimekusoma sana ntafanya uamuzi mgumu kwa ajili ya Watoto wangu bora tuoane na maria
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom