A3M
Member
- Jul 23, 2019
- 84
- 178
Habari wana JF natumai mko vizuri muda huu.Nichukue nafasi hii kuwatakia Waislam wote Eid-el-Adh-ha njema.Wadau siku kadhaa zilizopita niliweka Uzi hapa wa kutaka kupata uzoefu wenu wa kusafiri nchi za Ulaya na Marekani na nilieleza kuwa nimebahatika kupata visa ya Marekani kwaajili ya kwenda mkutano Mjini Washington D.C lakini sina uzoefu wa kusafiri hii ni mara yangu ya kwanza kupanda ndege.
Wapo walioniletea utani na wapo walionishauri vizuri hivyo nawashukuru wote walionipa mawazo mazuri.Wakuu ukweli Mimi Mhitimu wa Chuo kikuu ambae nimemaliza chuo mwaka 2012 na mara tu baada ya kumaliza nikabahatika kupata kazi moja ya kampuni kubwa hapa Jijini Daresalaam lakini malipo yalikuwa hayanitoshelezi hasa ukizingatia nilikuwa na mke na mtoto mmoja na pia nilikuwa nategemewa na mama yangu na ndugu zangu Saba ambao bado hawajamaliza kusoma wakati ule nilikuwa kama baba maana baba alishatangulia mbele ya haki na familia yangu ni masikini.
Ilifika wakati mama aliwaambia ndugu zangu wadogo kuwa kaeni nyumbani kaka yenu asome kisha akimaliza akapata kazi atawasomesha na ninyi.Kwa kweli tulikuwa na hali ngumu sana ya maisha ambayo sometime nikikumbuka huwa naumia sana.
Kwa sasa nina watoto watatu na nimefanikiwa kuwasomesha wadogo zangu wawili ambae mmoja anafanya kazi sasa na mwingine amemaliza chuo kikuu Mzumbe mwezi uliopita hivyo namshukuru mungu angalau maisha yamekuwa afueni maana nimemfungulia mama kiduka kidogo ambacho kinamsaidia kulipa umeme na maji na vitu vidogovidogo tunamshukuru Marehemu baba alituachia nyumba.
Sasa naomba ushauri wenu katika hili.Nategemea kwenda Marekani tarehe tarehe 17 mwezi huu je nisalie huko au nirudi nyumbani? Maana naona kila nikitazama hali mbaya ya maisha hapa kwetu nahisi siwezi kukamilisha malengo yangu maana nalipwa Mshahara mdogo na mimi kukopa sitaki japo nimeambiwa nakopesheka.
Je nibaki Marekani au nirudi Home?.Naomba ushauri wenu.Natanguliza Shukran kwa atakaenishauri vyema