Naombeni ushauri niende kubaki Marekani au nirudi nyumbani

A3M

Member
Jul 23, 2019
84
178
Habari wana JF natumai mko vizuri muda huu.Nichukue nafasi hii kuwatakia Waislam wote Eid-el-Adh-ha njema.Wadau siku kadhaa zilizopita niliweka Uzi hapa wa kutaka kupata uzoefu wenu wa kusafiri nchi za Ulaya na Marekani na nilieleza kuwa nimebahatika kupata visa ya Marekani kwaajili ya kwenda mkutano Mjini Washington D.C lakini sina uzoefu wa kusafiri hii ni mara yangu ya kwanza kupanda ndege.

Wapo walioniletea utani na wapo walionishauri vizuri hivyo nawashukuru wote walionipa mawazo mazuri.Wakuu ukweli Mimi Mhitimu wa Chuo kikuu ambae nimemaliza chuo mwaka 2012 na mara tu baada ya kumaliza nikabahatika kupata kazi moja ya kampuni kubwa hapa Jijini Daresalaam lakini malipo yalikuwa hayanitoshelezi hasa ukizingatia nilikuwa na mke na mtoto mmoja na pia nilikuwa nategemewa na mama yangu na ndugu zangu Saba ambao bado hawajamaliza kusoma wakati ule nilikuwa kama baba maana baba alishatangulia mbele ya haki na familia yangu ni masikini.

Ilifika wakati mama aliwaambia ndugu zangu wadogo kuwa kaeni nyumbani kaka yenu asome kisha akimaliza akapata kazi atawasomesha na ninyi.Kwa kweli tulikuwa na hali ngumu sana ya maisha ambayo sometime nikikumbuka huwa naumia sana.

Kwa sasa nina watoto watatu na nimefanikiwa kuwasomesha wadogo zangu wawili ambae mmoja anafanya kazi sasa na mwingine amemaliza chuo kikuu Mzumbe mwezi uliopita hivyo namshukuru mungu angalau maisha yamekuwa afueni maana nimemfungulia mama kiduka kidogo ambacho kinamsaidia kulipa umeme na maji na vitu vidogovidogo tunamshukuru Marehemu baba alituachia nyumba.

Sasa naomba ushauri wenu katika hili.Nategemea kwenda Marekani tarehe tarehe 17 mwezi huu je nisalie huko au nirudi nyumbani? Maana naona kila nikitazama hali mbaya ya maisha hapa kwetu nahisi siwezi kukamilisha malengo yangu maana nalipwa Mshahara mdogo na mimi kukopa sitaki japo nimeambiwa nakopesheka.

Je nibaki Marekani au nirudi Home?.Naomba ushauri wenu.Natanguliza Shukran kwa atakaenishauri vyema
 
Hongera Sana Kwa Majukumu
Pia Kwasasa Naamini Unakwenda US
Tafadhali Jitahidi Uende Ukatimize Malengo Yako Halafu Ukimaliza Rudi Home Uje Upambane Hapa Hapa.

Kuna Member Mmoja Alileta Thread Yake Humu Jukwaani Kuomba Ushauri, Yeye Yupo Ulaya Mashariki Tangu 1988 Akifanya Kazi Ndogo Ndogo Na Alikuwa Na Dollars 5000 Kama Sijakosea

Sasa Akawa Anauliza Vp Nyumbani Akirudi Na Pesa Hiyo Anaweza Kujenga Na Biashara Yoyote
Nadhani Wewe Mwenyewe Jibu Unalo
 
  • Thanks
Reactions: A3M
Kwa mimi sijawahi kusafili nje ya nchi,ila kwa maono yangu ni bora ukaludi nyumbani kwani teyari usha kuwa na familiya Mke na watoto ni vema ukaludi ukawa karibu na familiya yako.

Tambua uko unaanza moja,uoni kama itakuwa ngumu pale pindi familiya itakapo itaji msaada wa kifedha kutoka kwako?

Ni maoni,ila kwa utakalo ona sahihi kufanya basi Mungu akubaliki kaka.
 
Habari wana JF natumai mko vizuri muda huu.Nichukue nafasi hii kuwatakia Waislam wote Eid-el-Adh-ha njema.Wadau siku kadhaa zilizopita niliweka Uzi hapa wa kutaka kupata uzoefu wenu wa kusafiri nchi za Ulaya na Marekani na nilieleza kuwa nimebahatika kupata visa ya Marekani kwaajili ya kwenda mkutano Mjini Washington D.C lakini sina uzoefu wa kusafiri hii ni mara yangu ya kwanza kupanda ndege.Wapo walioniletea utani na wapo walionishauri vizuri hivyo nawashukuru wote walionipa mawazo mazuri.Wakuu ukweli Mimi Mhitimu wa Chuo kikuu ambae nimemaliza chuo mwaka 2012 na mara tu baada ya kumaliza nikabahatika kupata kazi moja ya kampuni kubwa hapa Jijini Daresalaam lakini malipo yalikuwa hayanitoshelezi hasa ukizingatia nilikuwa na mke na mtoto mmoja na pia nilikuwa nategemewa na mama yangu na ndugu zangu Saba ambao bado hawajamaliza kusoma wakati ule nilikuwa kama baba maana baba alishatangulia mbele ya haki na familia yangu ni masikini.Ilifika wakati mama aliwaambia ndugu zangu wadogo kuwa kaeni nyumbani kaka yenu asome kisha akimaliza akapata kazi atawasomesha na ninyi.Kwa kweli tulikuwa na hali ngumu sana ya maisha ambayo sometime nikikumbuka huwa naumia sana.Kwa sasa nina watoto watatu na nimefanikiwa kuwasomesha wadogo zangu wawili ambae mmoja anafanya kazi sasa na mwingine amemaliza chuo kikuu Mzumbe mwezi uliopita hivyo namshukuru mungu angalau maisha yamekuwa afueni maana nimemfungulia mama kiduka kidogo ambacho kinamsaidia kulipa umeme na maji na vitu vidogovidogo tunamshukuru Marehemu baba alituachia nyumba.
Sasa naomba ushauri wenu katika hili.Nategemea kwenda Marekani tarehe tarehe 17 mwezi huu je nisalie huko au nirudi nyumbani? Maana naona kila nikitazama hali mbaya ya maisha hapa kwetu nahisi siwezi kukamilisha malengo yangu maana nalipwa Mshahara mdogo na mimi kukopa sitaki japo nimeambiwa nakopesheka.Je nibaki Marekani au nirudi Home?.Naomba ushauri wenu.Natanguliza Shukran kwa atakaenishauri vyema
ubaki marekani kwa nani ? na kwa mchongo upi ? hivi unajua hata ukiwa mbinguni bila mchongo ni kama motoni tu ? kama unaenda kwa mkutano then kuna mchongo hapo sawa
 
Njoo Marekani kama ulivyoomba visa, ukae kwa muda huo, urudi nyumbani.

Kama unataka kuhamia Marekani, fuata sheria za kuhamia.

Kama unataka kusoma, fuata sheria za visa ya kusoma.

Ukija Marekani kinyume na sheria unajiwekea msingi mbaya, hata kazi utakazokuja kupata zitakuwa ni za malipo ya chini.
 
Njoo Marekani kama ulivyoomba visa, ukae kwa nuda huo, urudi nyumbani.

Kama unataka kuhamia Marekani, fuata sheria za kuhamia.

Kama unataka kusoma, fuata sheria za visa ya kusoma.

Ukija Marekani kinyume na sheria unajiwekea msingi mbaya, hata kazi utakayokuja kupata zitakuwa ni za malipo ya chini.
Hata akitafuta Mhaiti wa kufunga nae ndoa?
 
Habari wana JF natumai mko vizuri muda huu.Nichukue nafasi hii kuwatakia Waislam wote Eid-el-Adh-ha njema.Wadau siku kadhaa zilizopita niliweka Uzi hapa wa kutaka kupata uzoefu wenu wa kusafiri nchi za Ulaya na Marekani na nilieleza kuwa nimebahatika kupata visa ya Marekani kwaajili ya kwenda mkutano Mjini Washington D.C lakini sina uzoefu wa kusafiri hii ni mara yangu ya kwanza kupanda ndege.Wapo walioniletea utani na wapo walionishauri vizuri hivyo nawashukuru wote walionipa mawazo mazuri.Wakuu ukweli Mimi Mhitimu wa Chuo kikuu ambae nimemaliza chuo mwaka 2012 na mara tu baada ya kumaliza nikabahatika kupata kazi moja ya kampuni kubwa hapa Jijini Daresalaam lakini malipo yalikuwa hayanitoshelezi hasa ukizingatia nilikuwa na mke na mtoto mmoja na pia nilikuwa nategemewa na mama yangu na ndugu zangu Saba ambao bado hawajamaliza kusoma wakati ule nilikuwa kama baba maana baba alishatangulia mbele ya haki na familia yangu ni masikini.Ilifika wakati mama aliwaambia ndugu zangu wadogo kuwa kaeni nyumbani kaka yenu asome kisha akimaliza akapata kazi atawasomesha na ninyi.Kwa kweli tulikuwa na hali ngumu sana ya maisha ambayo sometime nikikumbuka huwa naumia sana.Kwa sasa nina watoto watatu na nimefanikiwa kuwasomesha wadogo zangu wawili ambae mmoja anafanya kazi sasa na mwingine amemaliza chuo kikuu Mzumbe mwezi uliopita hivyo namshukuru mungu angalau maisha yamekuwa afueni maana nimemfungulia mama kiduka kidogo ambacho kinamsaidia kulipa umeme na maji na vitu vidogovidogo tunamshukuru Marehemu baba alituachia nyumba.
Sasa naomba ushauri wenu katika hili.Nategemea kwenda Marekani tarehe tarehe 17 mwezi huu je nisalie huko au nirudi nyumbani? Maana naona kila nikitazama hali mbaya ya maisha hapa kwetu nahisi siwezi kukamilisha malengo yangu maana nalipwa Mshahara mdogo na mimi kukopa sitaki japo nimeambiwa nakopesheka.Je nibaki Marekani au nirudi Home?.Naomba ushauri wenu.Natanguliza Shukran kwa atakaenishauri vyema
Hongera sana ndugu. sana sana. kweli unayaweza majukumu. hujazungumzia kutafuta kazi nyingine yenye kipato kikubwa, pili unabaki hapa ya nini kaka?! mke unaye. watoto pia. mama umemwezesha, ndugu ndio usiseme. sasa cha kukuweka hapa ni nini????!!! nenda US of A upate zaidi uweke boma lako kamtaji kagari pale huku waendelea kuwasaidia ndugu mama na familia yako mpaka mwili utakapochoka au kutimiza malengo. ebu panda ndinga haraka sana kaka..
 
Habari wana JF natumai mko vizuri muda huu.Nichukue nafasi hii kuwatakia Waislam wote Eid-el-Adh-ha njema.Wadau siku kadhaa zilizopita niliweka Uzi hapa wa kutaka kupata uzoefu wenu wa kusafiri nchi za Ulaya na Marekani na nilieleza kuwa nimebahatika kupata visa ya Marekani kwaajili ya kwenda mkutano Mjini Washington D.C lakini sina uzoefu wa kusafiri hii ni mara yangu ya kwanza kupanda ndege.Wapo walioniletea utani na wapo walionishauri vizuri hivyo nawashukuru wote walionipa mawazo mazuri.Wakuu ukweli Mimi Mhitimu wa Chuo kikuu ambae nimemaliza chuo mwaka 2012 na mara tu baada ya kumaliza nikabahatika kupata kazi moja ya kampuni kubwa hapa Jijini Daresalaam lakini malipo yalikuwa hayanitoshelezi hasa ukizingatia nilikuwa na mke na mtoto mmoja na pia nilikuwa nategemewa na mama yangu na ndugu zangu Saba ambao bado hawajamaliza kusoma wakati ule nilikuwa kama baba maana baba alishatangulia mbele ya haki na familia yangu ni masikini.Ilifika wakati mama aliwaambia ndugu zangu wadogo kuwa kaeni nyumbani kaka yenu asome kisha akimaliza akapata kazi atawasomesha na ninyi.Kwa kweli tulikuwa na hali ngumu sana ya maisha ambayo sometime nikikumbuka huwa naumia sana.Kwa sasa nina watoto watatu na nimefanikiwa kuwasomesha wadogo zangu wawili ambae mmoja anafanya kazi sasa na mwingine amemaliza chuo kikuu Mzumbe mwezi uliopita hivyo namshukuru mungu angalau maisha yamekuwa afueni maana nimemfungulia mama kiduka kidogo ambacho kinamsaidia kulipa umeme na maji na vitu vidogovidogo tunamshukuru Marehemu baba alituachia nyumba.
Sasa naomba ushauri wenu katika hili.Nategemea kwenda Marekani tarehe tarehe 17 mwezi huu je nisalie huko au nirudi nyumbani? Maana naona kila nikitazama hali mbaya ya maisha hapa kwetu nahisi siwezi kukamilisha malengo yangu maana nalipwa Mshahara mdogo na mimi kukopa sitaki japo nimeambiwa nakopesheka.Je nibaki Marekani au nirudi Home?.Naomba ushauri wenu.Natanguliza Shukran kwa atakaenishauri vyema
Hapana husizamia kihivyo tumia huo mda kutafuta college yoyote ili upate form ya kujiunga urudi nyumbani ndo uombe viza ya mwanafunzi ili uweze kufanya kazi kihalali
 
We naenda urudi bana, mambo ya kuzamia si mazuri unaweza ukakaa miaka zaidi ya 30 hujapata karatasi kumbuka una familia na watoto itakuwa si poa kabisa.

Hayo mambo kwako too late ulitakiwa ufanye kabla hujaitwa mume au baba ukishakuwa na familia tanguliza maslahi ya familia mbele usiwe mbinafsi wa kujifikiria wewe tu.
 
Nakukumbusha una watoto na mke.

Usiwasahau utakapofanya maamuzi yoyote.
 
Endelea kukaa kwenye foleni ya kwenye bomba. Wa mbele wanazidi kusogea. Wengine wanastaafu wengine wanafarki. Soon utajikuta uko kwenye top management. Ukienda ng'ambo utaishia kuwa kruta.
 
Mkeo na watoto unataka kumuachia Nani?kama tukikushauri ubaki marekani????

Au ndo mke keshakushinda unataka kutelekeza???
 
Back
Top Bottom