G8M8
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 432
- 389
Mimi ni kijana niliyekulia ktk familia ya kipato cha kawaida Sana.. Nilianza safari yangu ya kusoma kwa kujituma toka shule ya msingi na kuvuka hadi advance nikiwa na imani iliyo kwenye mind yangu nije kuwa na maisha mazuri lkn pia nilikuwa nikiwaza Sana maisha yatakuwaje baadae kwani nimesomeshwa na mama na mama yangu ana amini mwanaye nitakuwa na maisha mazuri baadaye nikija kuajiriwa.
Sasa baada ya kumaliza kidato cha Sita mwaka 2018 nilijiamini nitatoboa kabisa sikuwa na hofu nilichukua combination ya pcm lkn mambo yakawa tofauti kabisa nikashindwa kukizi vigezo vya kwenda chuo..
Baada ya kurudi toka jeshi sikuwa vizuri nikifikiria nimekosea wapi mbona mtihani nilifanya vizuri nikifikiria mengi mpaka nikahisi kuchanganyikiwa kwa sababu matarajio yamekuwa tofauti na mama yangu naye na mawazo kibao akiamini maisha kwangu ndio basi kwa kweli nilikuwa na wakati mgumu weak Zapata 3 au 2..
Ndani ya hizo siku nilijawa na wazo nirudie mtihani lkn nilishaomba ushauri Sana kwa watu hadi wazazi wa wenzangu nakumbuka niliambiwa achana na hayo mawazo kubaliana na yaliyo tokea chukua uamuzi mwengine lkn nilitaka kufanya kumridhisha mama nikalipiwa gharama za mtihani lkn baadae nikawa na wazo la kufanya biashara nitoke kimaisha Kwan kusoma lengo litakuwa ni kuajiriwa na hilo jambo halitafanya nifike ndoto zangu kwani nina malengo mengi sana hivyo huu uamuzi wa kurudia mtihani nilijutia sikuwa najishughulisha kabisa na kusoma zaidi kutumia mda wangu kufanya tafiti za biashara mbali mbali..
Imefikia mda sasa nataka kufanya vitendo ili nifike lengo kuu.. sasa mama aliniuliza mbona sikuoni ukisoma itabidi nimwambie kitu ambacho nalenga kufanya na mtihani sitofanya kwani nimeona maisha yamebadilika ni wakati wa kubadili fikra zetu kujiajiri siyo kuajiriwa..
Mama yangu hataki kabisa wazo langu na ameongea Sana anaamini siwezi kuwa na maisha mazuri kama sitofika chuo kikuu.. yeye na mzee wameongea Sana na nimeambiwa kama nina mawazo hayo basi niondoke nyumbani nikatafute mama aliyenizaa
Nipo na mawazo mengi sana mama yangu amekasirika na hataki kuniona nimesikitika Sana wazazi wetu kuwa na mawazo haya... Ameongea Sana kiasi hata mm mwenyewe nina mawazo Sana sijamvunjia heshima mama yangu lkn yamekuwa haya..
Naombeni ushauri nifanye nini kijana wenu...
Sent using Jamii Forums mobile app