Naombeni ushauri kwa hili lililonikuta

Fanya mtihani na kazana ufaulu.

Kwani ukisoma Kuna shida gani??
Kwani ukifanya biashara huku ukiwa na digrii Kuna shida gani??

Biashara sio kazi rahisi Kama unavyofikiri labda ukubali kupata sh kumikumi zisizokidhi maisha.

Lkn ukiajiriwa hata Kama unalipwa laki kwa mwezi una amani yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya kilicho ndani ya moyo wako, ushakuwa mtu mzima sasa hutakiwi kuyumbishwa na mawazo ya wazazi/ndugu hatma ya maisha yako iko mikononi mwa Mungu na wewe mwenyewe.
Nafasi waliyo nayo wazazi/ndugu zako ni kukushauri tu na kukuonyesha njia sahihi katika maisha.

Muombe sana Mungu yeye ndiye ajuaye ukweli wewe ni nani hakuna mwingine.
unamwambia aombe Mungu na hapo hapo unamwambia afate kilichomoyoni mwake asiyumbishwe na wazazi, unajua neno la Mungu linasemaje kuhusu wazazi? sasa bila kutengeneza na kutafuta kwanza amani na wazazi wake hayo maombi atakayoomba yatakuwa maombi gani?
 
Kitu kimoja ambacho watu wengi wanajuta kwenye maisha Ni kufanya mambo kuwapendeza watu.

Fanya unachopenda kwa juhudi zote wazazi wako watakuelewa baadae..

Kitu kimoja ambacho Ni chako na unamiliki wewe Moja kwa Moja Ni maisha yako sasa wewe una uamuzi uwe jambazi,uwe padri use mfanyabiashara, uwe mwalimu uwe mvuta bangi ...ishi kama una hati miliki ya maisha yako... wazazi wako walishakuleta duniani inatosha waheshimu ila sio kupangiana maisha...

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuheshimu Ni pamoja na kusikiliza ushauri mwema wa wazazi.

Eti unashauri kabisaaa maisha Ni yake hata akiwa jambazi.....au mvuta bangi....hujui tu mzazi au familia inapitia shida gani mtu akiwa mwizi ama mvuta bangi.

Haya ukimwambia aamue unajua mtaji atapata wapi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mdogo wangu nakushauri.USOME KWANZA, NARUDIA TENA..NAKUOMBA USOME KWANZA.. NARUDIA NAKUOMBA USOME.
Hakuna kitu unachokiwahi leo ambapo kesho hautakikuta..kusoma kuna kufungulia uwanja mpana wa kucheza na maisha...mfano kwa masomo yako hayo ukienda somea ujuzi wowote hata I.T tu tayari utaweza kufanya mambo kulingana na ujuzi wako,na ujuzi wako ukawa ndio mtaji badala ya kuajiliwa..
NARUDIA..NAOMBA USOME DOGO.. MAMA YAKO SIO.MJINGA WALA MPUUZI.
Fanya utafiti ni watu wangapi walio kwenye biashara na wanasema kama wangesoma wangekuwa mbali zaidi..ndio ujue umuhimu wa kusoma... Kwenye kusoma hakuna kupoteza mdogo wangu
Hausomi ili uajiliwe tambua hilo

Wa sangara
 
unamwambia aombe Mungu na hapo hapo unamwambia afate kilichomoyoni mwake asiyumbishwe na wazazi, unajua neno la Mungu linasemaje kuhusu wazazi? sasa bila kutengeneza na kutafuta kwanza amani na wazazi wake hayo maombi atakayoomba yatakuwa maombi gani?
Kilicho ndani ya moyo wake kinaweza kuwa ndiyo jibu sahihi ya kile Mungu alichomuandalia na vile vile kinaweza kuwa siyo sahihi.
Ili awe na uhakika sasa ndiyo anatakiwa kumuomba Mungu yeye ndiye mwenye majibu yote.

Kuhusu suala la wazazi wake sijaona pahala alipoandika amegombana nao, ila wao ndiyo wanagombana naye wakitaka afuate wanachotaka wao. Hivyo tatizo haliko kwake liko kwao.

Nimalizie kwa kukuuliza swali kidogo ndugu yako anapokuchukia nawe ukatafuta suluhu naye akakataa. Je aweza zuia maombi yako kwa Mungu?
 
uzito wa ndugu na wazazi ni tofauti, na point hapa ni wazazi
 
Mimi ni kijana niliyekulia ktk familia ya kipato cha kawaida Sana.. nilianza safari yangu ya kusoma kwa kujituma toka shule ya msingi. nilifanikiwa kuvuka hadi advance nikiwa na imani iliyo kwenye mind yangu nije kuwa na maisha mazuri lkn pia nilikuwa nikiwaza Sana maisha yatakuwaje baadae kwani nimesomeshwa na mama na mama yangu ana amini mwanaye nitajakuwa na maisha mazuri baadaye nikija kuajiriwa.. sasa baada ya kumaliza kidato cha Sita mwaka 2018 nilijiamini nitatoboa kabisa sikuwa na hofu nilichukua combination ya pcm. lkn mambo yakawa tofauti kabisa nikashindwa kukizi vigezo vya kwenda chuo.. baada ya kurudi toka jeshi sikuwa vizuri nikifikiria nimekosea wapi mbna mtihani nilifanya vizuri nikifikiria mengi mpaka nikahisi kuchanganyikiwa kwa sababu matarajio yamekuwa tofauti na mama yangu naye na mawazo kibao akiamini maisha kwangu ndio basi kwa kweli nilikuwa na wakati mgumu weak Zapata 3 au 2.. ndani ya hizo siku nilijawa na wazo nirudie mtihani lkn nilishaomba ushauri Sana kwa watu hadi wazazi wa wenzangu nakumbuka niliambiwa achana na hayo mawazo kubaliana na yaliyo tokea chukua uamuzi mwengine lkn nilitaka kufanya kumridhisha mama nikalipiwa gharama za mtihani lkn baadae nikawa na wazo la kufanya biashara nitoke kimaisha Kwan kusoma lengo litakuwa ni kuajiriwa na hilo jambo halitafanya nifike ndoto zangu kwani nina malengo mengi sana hivyo huu uamuzi wa kurudia mtihani nilijutia sikuwa najishughulisha kabisa na kusoma zaidi kutumia mda wangu kufanya tafiti za biashara mbali mbali.. imefikia mda sasa nataka kufanya vitendo ili nifike lengo kuu.. sasa mama aliniuliza mbna sikuoni ukisoma itabidi nimwambie kitu ambacho nalenga kufanya na mtihani sitofanya kwani nimeona maisha yamebadilika ni wakati wa kubadili fikra zetu kujiajiri siyo kuajiriwa.. Mama yangu ataki kabisa wazo langu na ameongea Sana anaamini siwezi kuwa na maisha mazuri kama sitofika chuo kikuu.. yeye na mzee wameongea Sana.. na nimeambiwa kama nina mawazo basi niondoke nyumbani nikatafute mama aliye nizaa nipo na mawazo mengi sana mama yangu amekasirika na ataki kuniona nimesikitika Sana wazazi wetu kuwa na mawazo haya... Ameongea Sana kiasi hata mm mwenyewe nina mawazo Sana sijamvunjia heshima mama yangu lkn yamekuwa haya.. Naombeni ushauri nifanye nini kijana wenu...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza akili yako ya kitoto bado. Yani baba na mama yako bado wako pamoja alafu unadiriki kabisa kusema "nimesomeshwa na mama"! Unajua coordination kati ya baba na mama yako au unasikiliza maneno ya mama???
matter core yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuogopa kuondoka nyumbani ni uoga ingia kitaa pambana fanya kile unachokipenda
 
Mimi ni kijana niliyekulia ktk familia ya kipato cha kawaida Sana.. nilianza safari yangu ya kusoma kwa kujituma toka shule ya msingi. nilifanikiwa kuvuka hadi advance nikiwa na imani iliyo kwenye mind yangu nije kuwa na maisha mazuri lkn pia nilikuwa nikiwaza Sana maisha yatakuwaje baadae kwani nimesomeshwa na mama na mama yangu ana amini mwanaye nitajakuwa na maisha mazuri baadaye nikija kuajiriwa.. sasa baada ya kumaliza kidato cha Sita mwaka 2018 nilijiamini nitatoboa kabisa sikuwa na hofu nilichukua combination ya pcm. lkn mambo yakawa tofauti kabisa nikashindwa kukizi vigezo vya kwenda chuo.. baada ya kurudi toka jeshi sikuwa vizuri nikifikiria nimekosea wapi mbna mtihani nilifanya vizuri nikifikiria mengi mpaka nikahisi kuchanganyikiwa kwa sababu matarajio yamekuwa tofauti na mama yangu naye na mawazo kibao akiamini maisha kwangu ndio basi kwa kweli nilikuwa na wakati mgumu weak Zapata 3 au 2.. ndani ya hizo siku nilijawa na wazo nirudie mtihani lkn nilishaomba ushauri Sana kwa watu hadi wazazi wa wenzangu nakumbuka niliambiwa achana na hayo mawazo kubaliana na yaliyo tokea chukua uamuzi mwengine lkn nilitaka kufanya kumridhisha mama nikalipiwa gharama za mtihani lkn baadae nikawa na wazo la kufanya biashara nitoke kimaisha Kwan kusoma lengo litakuwa ni kuajiriwa na hilo jambo halitafanya nifike ndoto zangu kwani nina malengo mengi sana hivyo huu uamuzi wa kurudia mtihani nilijutia sikuwa najishughulisha kabisa na kusoma zaidi kutumia mda wangu kufanya tafiti za biashara mbali mbali.. imefikia mda sasa nataka kufanya vitendo ili nifike lengo kuu.. sasa mama aliniuliza mbna sikuoni ukisoma itabidi nimwambie kitu ambacho nalenga kufanya na mtihani sitofanya kwani nimeona maisha yamebadilika ni wakati wa kubadili fikra zetu kujiajiri siyo kuajiriwa.. Mama yangu ataki kabisa wazo langu na ameongea Sana anaamini siwezi kuwa na maisha mazuri kama sitofika chuo kikuu.. yeye na mzee wameongea Sana.. na nimeambiwa kama nina mawazo basi niondoke nyumbani nikatafute mama aliye nizaa nipo na mawazo mengi sana mama yangu amekasirika na ataki kuniona nimesikitika Sana wazazi wetu kuwa na mawazo haya... Ameongea Sana kiasi hata mm mwenyewe nina mawazo Sana sijamvunjia heshima mama yangu lkn yamekuwa haya.. Naombeni ushauri nifanye nini kijana wenu...

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua mdogo wangu hata mimi nimepitia njia kama yako miaka ya nyuma huko.Ila kwenye kurudia mtihani wa form six niliamua mwenyewe kwa moyo wangu.Nilireseat masomo mawili na nikatoboa, hapo nyuma watu wengi walinishauri vitu vingi lakini maamuzi ya mwisho nilifanya mwenyewe. Baada ya matokeo nilifanya vizuri then nikaaply chuo nikapata+bum juu. Nimegraduate 2017 now nina maisha yangu, japo hela ya mboga sikosi.Kikubwa fanya ambacho unakiweza, jitume kwa unachokiamini, sali kwa imani yako utatoboa.
 
Kuheshimu Ni pamoja na kusikiliza ushauri mwema wa wazazi.

Eti unashauri kabisaaa maisha Ni yake hata akiwa jambazi.....au mvuta bangi....hujui tu mzazi au familia inapitia shida gani mtu akiwa mwizi ama mvuta bangi.

Haya ukimwambia aamue unajua mtaji atapata wapi??

Sent using Jamii Forums mobile app
Ushauri mwema unajua maana yake ???????

Mapema Sana inabidi ujifunze sio kisa mtu anakupenda au mzazi wako au rafiki yako Basi ushauri atakaokupa utakufaaa sio yeye tu hata wewe inabidi uelewe hilo mapema.

Na niliposema Ana hati miliki ya maisha yake nilikuwa na maana hata leo hii akiamua kuwa mvuta bangi bado ni maisha yake yeye ndo ataamua afanyaje na maisha yake.
Ukiamua kutumia maisha yako kufuata ushauri wa ndugu,jamaa na marafiki ni wewe na uamuzi wako....narudia tena maisha Ni yako ukitakae kuvuta bangi nayo sawa,kuwa jambazi sawa,kuwa Malaya sawa,kuwa mchungaji sawa...huyo unayemsikiliza Sana na yeye keshamaliza na na yake funny enough hana analojua kuhusu wewe Zaid yako wewe mwenyewe.

Nipe ushauri tusipangiane Cha kufanya kisa wewe Ni mzazi wangu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kahustle tu mtaani..hii mentality ya 'mwanangu soma ufike hadi chuo kikuu upate kazi uwe na maisha mazuri'
Imemteka mamako...na wazazi wengi wa siku hizi wanayo..mi siipendi kwakweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikiwa form one mwishoni (October) pale IFUNDA TECHNICAL SECONDARY SCHOOL, wakati natakiwa kuchagua FANI, moyoni nataka UMEME lakini baba ALISHANIAMBIA TOKA MWEZI JUNI KWAMBA NIKACHAGUE MECHANICAL.... mimi sikuwa naipenda… NIKACHAGUA UMEME NIKIWA NIMEANDAA MAELEZO KIBAO YA KWANINI NIMECHAGUA UMEME...

Alinielewa
 
Kijana mm nikushauri kitu kimoja,

Nenda kaongee na wazazi wako, wailize wao wanataka usomee degree ya kitu gani endapo utafaulu kidato cha 6,

Then waulize wataweza kumudu ada pamoja na mahitaji yako yote muhimu kwa Muda wa masomo
Means degree ya mika mitano
Utamaliza mwaka 2025, (2020/2021 - 2025) wataweza kukuhudumia na vyuo kwa sasa gharama zipo juu.

Chance bado unayo kubwa, kama unaona itakua ni ngumu kwa hilo, kasome hata diploma ya engineer yoyote ambayo haiitaji kusubiri ajira kama, civil au umeme ni rahis kujiajiri.

Mbali na apo maisha sio poa yanachapa balaa.

Pia kumbuka kusali,
Muombe Mungu ndie tumaini, hufanya njia pasipo na njia.

Asante Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi Mwenyewe nilifeli Kidato cha sita, Matokeo yalikuja tofauti na matarajio yangu,nilikata tamaa!!!. Lkn MUNGU mwenye Huruma na Neema nyingi alinitia Moyo, nikasoma Diploma ya Kilimo, Baadaye nikaajiriwa Serikalini na sasa nipo SUA najiendeleza.Hapa SUA kuna Maprofessa ambao hawakupita A-level, kwa hiyo Usikate tamaa, nenda ukasome Diploma km Matokeo yanakuruhusu Kusoma Diploma, lah!!, hayaruhusu, nenda kasome Certificate, wewe bado mdogo, Nakwambia utatoboa hadi PHD, na hauta amini. Muhimu usikate tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom