Naombeni ushauri kwa hili lililonikuta

Naombeni ushauri kwa hili lililonikuta

Pole dogo..

Kuna njia mbili za kufikia ndoto zako

1. Njia rahisi sana ukiwa umesoma hadi chuo kikuu.. si kweli kwamba ukifika chuo unakwenda kuishia kuajiriwa.. si kweli.. ukimaliza chuo utakuwa na uelewa mpana na hivyo ni rahisi sana kufanya chochote unachokitaka

2. Njia ngumu sana ukiwa hujasoma na una ndoto unahitaji kuzifikia.. utachakaa balaa.. itakuchukuwa miaka hata 20.. labda uwe mwizi, tapeli au mfanya magendo..

Yangu ni hayo kwa sasa
 
Ushauri mzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri unaweza kufanya yote kwa pamoja, mana inaonekana kusoma hutaki bali ni kuwaridhisha wazee na sio jambo baya, wewe endelea na ishu za kuchunguza biashara kimya kimya, halafu ukipata mda home kaa na madaftari yako sehemu Ile ambayo wazazi wapo. At the end utaishi maisha aliyokupangia Mungu na sio uyatakayo mwenyewe.
Asante kwa ushauri #lakin niliwahi mwambia nataka nifanye nisome huku nna biashara akakataa #

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapo kweli mtihani unao mdogo wangu, ni hivi ili uweze kuwa na amani na ufanye vitu kwa uhakika ni lazma utengeneze amani na wazazi wako mana mwisho wa yote wao watabaki wazazi na ndio kimbilio lako la mwisho na wewe bado mdogo sana kuanza maisha huku wazazi wako wakiwa na kinyongo na wewe, sasa fanya hivi wewe kubaliana nao, resit mtihani lakini huku mambo yako mengine unayotaka kufanya yakiendelea, mana kusoma hakumzuii mtu kufanya biashara kama kweli ana moyo wa kufanya hivyo, na hata ikitokea umefaulu vzr ukachaguliwa kwenda chuo we nenda mana hiyo degree itakuwa faida kwako pia, mbona wako vijana wengi wanasoma chuo lakini pia wanajishugulisha na biashara kiasi kwamba wakimaliza wala hawahangaiki na ajira na hata wakitafuta inakuwa sio kwa presha, na kingine kuwa na elimu ya chuo ni kama ngao kwenye maisha yako kesho na kesho kutwa biashara zimegoma kabisa utatafuta ajira ikusaidie kimaisha wakati unatafuta namna ya kutatua changamoto zilizojitokeza kibiashara au kimaisha kiujumla
Ushauri mzuri huu ....lakini pia awe makini sana....namanisha.
 
Asante kwa ushauri #lakin niliwahi mwambia nataka nifanye nisome huku nna biashara akakataa #

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unatakiwa mambo mengine ufe nayo kiume, wazee baadhi ya mda ni watu wa kurudisha nyuma na wala hawalaumiwi kwa hilo kwakua ndivyo walivyo kuwa brainwashed kuwa maendeleo lazma ufike chuo kikuu, au huwezi kusoma huku ukifanya mambo mengine, kwa hio mambo mengine wewe ukishajua yana maslahi nawe komaa nayo kisiri siri tu. Si kila jambo linaanikwa
 
Mimi ni kijana niliyekulia ktk familia ya kipato cha kawaida Sana.. Nilianza safari yangu ya kusoma kwa kujituma toka shule ya msingi na kuvuka hadi advance nikiwa na imani iliyo kwenye mind yangu nije kuwa na maisha mazuri lkn pia nilikuwa nikiwaza Sana maisha yatakuwaje baadae kwani nimesomeshwa na mama na mama yangu ana amini mwanaye nitakuwa na maisha mazuri baadaye nikija kuajiriwa.

Sasa baada ya kumaliza kidato cha Sita mwaka 2018 nilijiamini nitatoboa kabisa sikuwa na hofu nilichukua combination ya pcm lkn mambo yakawa tofauti kabisa nikashindwa kukizi vigezo vya kwenda chuo..

Baada ya kurudi toka jeshi sikuwa vizuri nikifikiria nimekosea wapi mbona mtihani nilifanya vizuri nikifikiria mengi mpaka nikahisi kuchanganyikiwa kwa sababu matarajio yamekuwa tofauti na mama yangu naye na mawazo kibao akiamini maisha kwangu ndio basi kwa kweli nilikuwa na wakati mgumu weak Zapata 3 au 2..

Ndani ya hizo siku nilijawa na wazo nirudie mtihani lkn nilishaomba ushauri Sana kwa watu hadi wazazi wa wenzangu nakumbuka niliambiwa achana na hayo mawazo kubaliana na yaliyo tokea chukua uamuzi mwengine lkn nilitaka kufanya kumridhisha mama nikalipiwa gharama za mtihani lkn baadae nikawa na wazo la kufanya biashara nitoke kimaisha Kwan kusoma lengo litakuwa ni kuajiriwa na hilo jambo halitafanya nifike ndoto zangu kwani nina malengo mengi sana hivyo huu uamuzi wa kurudia mtihani nilijutia sikuwa najishughulisha kabisa na kusoma zaidi kutumia mda wangu kufanya tafiti za biashara mbali mbali..

Imefikia mda sasa nataka kufanya vitendo ili nifike lengo kuu.. sasa mama aliniuliza mbona sikuoni ukisoma itabidi nimwambie kitu ambacho nalenga kufanya na mtihani sitofanya kwani nimeona maisha yamebadilika ni wakati wa kubadili fikra zetu kujiajiri siyo kuajiriwa..

Mama yangu hataki kabisa wazo langu na ameongea Sana anaamini siwezi kuwa na maisha mazuri kama sitofika chuo kikuu.. yeye na mzee wameongea Sana na nimeambiwa kama nina mawazo hayo basi niondoke nyumbani nikatafute mama aliyenizaa

Nipo na mawazo mengi sana mama yangu amekasirika na hataki kuniona nimesikitika Sana wazazi wetu kuwa na mawazo haya... Ameongea Sana kiasi hata mm mwenyewe nina mawazo Sana sijamvunjia heshima mama yangu lkn yamekuwa haya..

Naombeni ushauri nifanye nini kijana wenu...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mambo ungeyaweka wazi pengine ungepata ushauri wenye mapana zaidi, mfano je kwa sasa kuna kashughuli yoyote unayofanya? lakini ngoja tukushauri kwa kile ulichosema

Hili jambo unaweza kulifanya kwa namna mbili, kwa njia ya mikimiki (hard way) au njia laini kidogo lakini ndefu (smooth but long way)

Hard way

Kwa kuwa unajua unachofanya, fumba macho, fumba masikio tafuta kile unachotaka. Kwa sisi tunaotoka Familia za kimasikini, njia rahisi ya kutafuta mtaji (bila kujali ni mdogo kiasi gani, cha msingi utoshe kuanzisha kabiashara yako) ni kutafuta ka ajira ambapo, kila mshara/posho utakayoipata unapaswa kuihesabu kama hela yako ya mwisho kupata kwenye maisha yako. SAVE IT. Kama unaweza save 30%,kama unaweza save 50%, kama unaweza save 90%. Tunza akiba (mtaji) kama huna akili nzuri. Kisha unaweka malengo ya kufanya kazi mwaka mmoja au miwili, Baada ya hapo nenda kafanya mradi wako

Smooth but long way

Kwa kuwa umeshajiandikisha kufanya mitihani, nakushauri soma kisha nenda ufanye mitihani lakini moyoni ukijua nini ambacho unakitafuta. Kufanya mitihani kutawa please wazazi wako lakini wakati huo huo utakuwa umejiongezea wigo wa fursa na machaguo

Baada ya mitihani unaweza kwenda kutimiza ndoto zako kwa kujali matokeo ya mitihani uliofanya au bila kujali

Kitu ninachoweza kusema, katika kutafuta mtaji (ukiwa umeajiriwa) usije ukafika hatua ukajiona upo salama, kamwe kwenye ajira haupo salama. Na walioajiriwa wengi wanashindwa kutoka kufuata ndoto zao kwa kuwa wanahisi pale waliopo ni salama. Kinachonichekesha'ga' ni pale anayeingiza milioni 3 kwa mwezi anajiona yupo salama kwenye ajira na anayeingiza Tsh laki na hamsini elfu anajiona pia yupo salama.....

Kinachowafanya wajione wapo salama ni ile posho wanayopata kila mwisho wa mwezi

Ukweli ni kwamba kwa Familia za kiafrika nyingi (sehemu ambayo ubebari umechelewa kuingia) ni ngumu sana kukuelewa unapowaambia kuwa una imani na ajira binafsi kuliko kazi.

Angalia ndoto zako, kuna mifano mingi sana ambapo watoto walifuata ndoto zao na wakaachana na ndoto za wazazi wao na sasa wazazi wanakiri walikosea
 
Mimi mtoto wangu Lazima nimpeleke veta huko atapata ujuzi utakaomsaidia, zama hizi kusoma had chuo kikuu ni kutafuta pressure na mawazo tena kudharauliwa kwa kupoteza muda.
 
Asante kwa ushauri mzuri nashkuru mungu... Now nimeanza hatua za kuifata ndoto yangu changamoto nakatishwa tamaa na ndugu zangu wa damu lkn mm huwa moyo wangu umeamua kwaiyo kama wanapiga guitar tu.. nawaambia nitakuja kuwa mtu fulani mm lkn wananiona chizi kwaiyo nakomaa kweli kweli juhudi zangu Kuna ambao wameshaanza kuhisi kitu.. Asante Sana mkuu
 
Usirudi nyuma,fanya kile ulichoamua moyoni. Wazazi hawawezi kukuzira. Nyumbani kwenu MUHIMU uondoke. Siku ya kuondoka,mwambie mama,naondoka nataka nifanye bashara mamangu,naomba nielewe. Mwambie kabisa nakupenda na nakujali mamangu. Hicho kitendo cha kuondoka nyumbani kitakupa hasira ya kupambana sana,utatoboa. MUHIMU uwe mwangalifu mjini wanawake wazuri wengi wasije wakakupoteza kabisa. Angalizo unapoendelea kufanya shughuri zako au biashara usikumbuke nyuma,yaani usijutie uamuzi wako wa kuacha kusoma na kuchagua biashara,vile vile usiyaingize kichwani maneno ya wazazi,yasije yakakuathiri wakati wa biashara utakakokuwa (kwa maana ya kila unapoanguka kibiashara utaona ni laana za wazazi kumbe ni kawaida au ni uzembe wako hasa kukumbatia uliyoambiwa na wazazi). Komaa bila kufikiria kuna laana
 
Nashkuru Sana. Mkuu hadi now sijasepa home ila najishughulisha narudi jioni.. now mungu anazidi kunipa nguvu kwani napambana japo nakatishwa tamaa na ndugu zangu Kuna siku wataelewa me sikuwa mjinga niliamua na ninaelekea kufanikiwa.. Asante Sana mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom