Wavuta bangi huwa wanaangalia mtu. Ameona labda wewe ni mpole, laini na mwoga ndiyo maana anakutishia lengo umpe pesa hana lolote huyo.Wakuu kwema.
Nimekuwa nikiishi kwa amani sana mpaka pale nilipoenda kupanga mtaani,
Kuna mpangaji mgeni ila inaonekana yeye ni mwenyeji hapa mtaani , ni mvutaji bangi mkubwa mno, utulivu hakuna.
Juzi natoka zangu kampas nakuta mtu kanisubiri akisema nimeiba kitu chake ambacho hata mimi sikijui kwakweli,
Kaukuza ugomvi anasumbua sana.
Nasasa kasema atanifanya kitu kibaya kwakweli amekuwa akinitishia sana, ukizingatia pia jamaa ana magenge ya wavuta bangi wenzake, na wala huwezi kuzungumza naye akakuelewa anapiga kelele tu.
Wakuu naombeni msaada wa kimawazo, sijawahi kutishiwa hivi, Siwezi kuhama kwasababu nimelipa kodi ya miezi nane pia sina hela. Siwezi kuishi nahofia usalama wangu hivi
Tuliokaa uswahilini tunawajua hao! Wanataka ukiwakuta kujiweni unawapa hai, oya washkaji vipi! Buku la fegi hilo! Ndiyo furaha yao. Hata urud saa sita usiku hawakuteki! Utawasikia! Mwanetu huyu! Sasa wewe umeenda kukaa uswahilini mtoto wa kishua! Kama hauwezi kujipendekeza kwao, basi unatakiwa uvae uso wa mbuzi mpige mkwara asikuzoee. Kakamaa! Pia, kama unaweza tafuta marafiki wa muda polisi au wajeda kadhaa, siku moja uwende nao pale kwako mjifanye kama ni marafiki ili ajue kuwa akizingua unamletea noma