Naombeni Ushauri kuna mtu amenitishia

Naombeni Ushauri kuna mtu amenitishia

Wakuu kwema.

Nimekuwa nikiishi kwa amani sana mpaka pale nilipoenda kupanga mtaani,
Kuna mpangaji mgeni ila inaonekana yeye ni mwenyeji hapa mtaani , ni mvutaji bangi mkubwa mno, utulivu hakuna.

Juzi natoka zangu kampas nakuta mtu kanisubiri akisema nimeiba kitu chake ambacho hata mimi sikijui kwakweli,
Kaukuza ugomvi anasumbua sana.
Nasasa kasema atanifanya kitu kibaya kwakweli amekuwa akinitishia sana, ukizingatia pia jamaa ana magenge ya wavuta bangi wenzake, na wala huwezi kuzungumza naye akakuelewa anapiga kelele tu.

Wakuu naombeni msaada wa kimawazo, sijawahi kutishiwa hivi, Siwezi kuhama kwasababu nimelipa kodi ya miezi nane pia sina hela. Siwezi kuishi nahofia usalama wangu hivi
Ww ni mwanafunzi ,tuanzie hapo
 
Mpeleke kwa mapolifisiem
 
Kama hataki kuongea na wewe ni vizuri kutoa taarifa Polisi.
Bhana, Polisi wana mambo mengi. Wanaweza kuanza kukugeuza ww ni ATM yao, wanaweza kukuharibia zaidi na jambo hilo likachukua sura mpya kabisa likakufanya ww uwe ndo unawindwa na wasiojulika kila siku. Hebu fanya hivi: Watafute marafiki zake huyo mvuta bangi e.g. ukimpata ambaye ni boda itakuwa ni nzuri zaidi, halafu uwe na urafiki nao. Watakusaidia sana na mtaa utaupenda.
 
Mtumie mtu Aongee nae, ikiwezekana mnunulie hicho kitu chake kipya muyamalizee hata kama hujachukua,then unadisconnect ukaribu nae ni salamu kwa Amani basii. Vitaa huiweziii wew nikikugrade,ukimpeleka police atatoka tu ndoo kitawakaa zaidi.Tumia akili kulimaliza.
 
Ukishindwa kuelewana na mvuta bangi jua wewe ndio mkuda
Una hoja. Inafaa wakusikilize.
Kwa uzoefu wangu; Wengi wa wavuta bangi ni watu rahisi sana kuelewana nao kwani hawanaga makuu. Kwa mfano unaweza kukuta hii kesi ya mtoa mada kitisho alichopewa ni ili asimsahau huyo mwamba kwenye kula mema ya nchi. Unaweza kukuta labda anahitaji kitu (fedha kidogo sana) lakini anashindwa atumie gia gani kumwingia mtoa mada?. Mbona hataji hicho kitu chake kilichoibiwa? Hapo mtoa mada inabidi ajiongeze kutambua kwamba hicho Kitu chake ni fedha; na hiyo fedha ipo mfukoni kwa mtoa mada.
 
Mtumie mtu Aongee nae, ikiwezekana mnunulie hicho kitu chake kipya muyamalizee hata kama hujachukua,then unadisconnect ukaribu nae ni salamu kwa Amani basii. Vitaa huiweziii wew nikikugrade,ukimpeleka police atatoka tu ndoo kitawakaa zaidi.Tumia akili kulimaliza.
Safi kabisa. Huu👆 👆 ni ushauri wa kiutu-Uzima zaidi. Kukimbilia Polisi ni suluhisho la muda mfupi sana na baadaye jambo hili hili litarejea tena kwa ukali zaidi.
 
Nunua toy lile linalofanana kabisa na mguu wa kuku ,lichomeke kwa suruali upandishe kidogo tshit ili lionekane makusudi, halafu jipitishe kwa kujiamini mbele yake bila kumsemesha chochote.
 
Wakuu kwema.

Nimekuwa nikiishi kwa amani sana mpaka pale nilipoenda kupanga mtaani,
Kuna mpangaji mgeni ila inaonekana yeye ni mwenyeji hapa mtaani , ni mvutaji bangi mkubwa mno, utulivu hakuna.

Juzi natoka zangu kampas nakuta mtu kanisubiri akisema nimeiba kitu chake ambacho hata mimi sikijui kwakweli,
Kaukuza ugomvi anasumbua sana.
Nasasa kasema atanifanya kitu kibaya kwakweli amekuwa akinitishia sana, ukizingatia pia jamaa ana magenge ya wavuta bangi wenzake, na wala huwezi kuzungumza naye akakuelewa anapiga kelele tu.

Wakuu naombeni msaada wa kimawazo, sijawahi kutishiwa hivi, Siwezi kuhama kwasababu nimelipa kodi ya miezi nane pia sina hela. Siwezi kuishi nahofia usalama wangu hivi
Bongo hakuna magenge ya wahuni,hao wote warembo tuu, ungekuwa south Africa ndio ungejua nini maana ya magenge ya wahuni na wahuni wenyewe
 
Wavuta bangi huwa wanaangalia mtu. Ameona labda wewe ni mpole, laini na mwoga ndiyo maana anakutishia lengo umpe pesa hana lolote huyo.

Tuliokaa uswahilini tunawajua hao! Wanataka ukiwakuta kujiweni unawapa hai, oya washkaji vipi! Buku la fegi hilo! Ndiyo furaha yao. Hata urud saa sita usiku hawakuteki! Utawasikia! Mwanetu huyu! Sasa wewe umeenda kukaa uswahilini mtoto wa kishua! Kama hauwezi kujipendekeza kwao, basi unatakiwa uvae uso wa mbuzi mpige mkwara asikuzoee. Kakamaa! Pia, kama unaweza tafuta marafiki wa muda polisi au wajeda kadhaa, siku moja uwende nao pale kwako mjifanye kama ni marafiki ili ajue kuwa akizingua unamletea noma
Yes. Dogo anasumbuka bure ilhali naye anaweza kujiwekea mkakati wa kujinasua na wavuta bangi. Umempa akili - alifanyie kazi halafu ikimpendeza alete mrejesho hapa.
 
Wakuu kwema.

Nimekuwa nikiishi kwa amani sana mpaka pale nilipoenda kupanga mtaani,
Kuna mpangaji mgeni ila inaonekana yeye ni mwenyeji hapa mtaani , ni mvutaji bangi mkubwa mno, utulivu hakuna.

Juzi natoka zangu kampas nakuta mtu kanisubiri akisema nimeiba kitu chake ambacho hata mimi sikijui kwakweli,
Kaukuza ugomvi anasumbua sana.
Nasasa kasema atanifanya kitu kibaya kwakweli amekuwa akinitishia sana, ukizingatia pia jamaa ana magenge ya wavuta bangi wenzake, na wala huwezi kuzungumza naye akakuelewa anapiga kelele tu.

Wakuu naombeni msaada wa kimawazo, sijawahi kutishiwa hivi, Siwezi kuhama kwasababu nimelipa kodi ya miezi nane pia sina hela. Siwezi kuishi nahofia usalama wangu hivi
kakuona mnyongemnyonge mtoto wa mama atakusumbua sana huyo mkiambiwa wekeni miili yenu sawa kama wanaume hamuelewi muda wote mnachelea tiktok hamna ratiba za mazoezi
 
Ukute huyo ndio tabia yake hio ya kukugeuza mnyonge wake
Ndiyo haswaa. Si unakumbuka enzi zile jinsi form 2 walivyokuwa wanawahenyesha bulling Form1 wapya (new comers kwa maneno a.k.a. Nyuka/Njuka/Nyoya n.k. kwa vitisho na mikwara "huja wahi kunywa maji ya Sekondari ww Njuka n.k.? Kumbe ilikuwa ni kukuchangamsha au kukutoa ushamba.Teh,Teh, tehh ..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom