Naombeni ushauri kuhusu tabia ya dada yangu

Naombeni ushauri kuhusu tabia ya dada yangu

Usije kuzimia siku ya harusi dada yako akiibua zengwe kanisani kuwa ana mimba ya huyu mchumba wako! Muhimu kwenye kamati ya maandalizi msisahau kuweka budget ya kuwalipa FFU ili wakae standby dada yako akileta za kuleta wamvurumishie mabomu ya machozi maana anaonekana ni hatari kwa usalama wa ndoa yako! Halafu kaa chini na mama yako umuulize vizuri akuambie kama kweli dada yako ni mtoto wa baba kweli maana haiwezekani awe na tabia za broiler wakati yeye ni wa kienyeji!

hahahahaha umenichekesha ila umeonge point sana, yeye mwenyewe dada anadai mama yake siyo huyu eti kuna sehemu kaambiwa hivyo, ila kuhusu swala wa wazazi ni kweli wazazi ni wetu wote tena ni original, ila kwa kuwa mama yuko upande wangu kwa sasa ndiyo nae anaambiwa kuwa haja mzaa ila amemlea tuu. huwa tuna kaa kimya tuu, kuhusu ndoa wengi wamezoea ndoa jioni mimi yangu kumuhofia huyo itafungwa asubuhi, ila kiukweli inabidi kazi ya ziada ifanyike kumuweka sawa
 
Kwanza kabisa unatakiwa umuombe sana Munguuu kwa ajilii ya harusi yako na pili mueleze mchumba wako ujue kuwa muwazi kwa mwanaume unaetaka kfunga nae ndoa
Kila la kherii

ni kweli nimefikiria hili kulifanya kesho mapema sana baada ya kutoka kanisani niende kuongea nae kwa kifupi tuu na ndiyo ata elewa kwanini mpaka sasa anamsikia tuu dada na hawajawahi kuonana
 
Da sijawai kuumia kama hivi, haa huyo mwanamke anawivu sana, roho mbaya. Mungu atamuumbua tu siku za mbeleni. Muombe sana mungu maana yeye ni kila kitu kwenye ndoa yako...
 
yeye anapenda sana marafiki zake kuliko mimi, nashukuru sana

pole sana, hapo dada huna. kinachomsumbua ni wivu tu na hakuna kingine.. anajisikia vibaya ukiolewa kabla yake, na kwa tabia zake it seems yeye hana utayari wa kuolewa ila kuharibu tu.

kaa chini na mchumba ako mweleze tabia zake, yeye mwacheni atajua last minute.

kila la kheri mami, ukifanikisha kaa macho naye asije kukaribia ndoa huyoo.
 
Hiki kisa ni cha kweli? Basi lawama kwa dada ondoa. Kila unachokisema kuhusu yeye kinaonyesha ana tatizo la akili. Mna mgonjwa. Sasa kwa kuwa umeshaona tabia yake, wadau hapa wameshakutabiria ya mbele. Si ajabu akatia viwembe au moto gauni lako siku ya harusi ukaishia kuvaa batiki!! Hata kama utafanikiwa kufunga ndoa huyu atakuandama tu na si ajabu akaja kumsingizia mumeo hata ubakaji ilimradi akunyime raha. We mweleze huyo shemeji ukweli kuhusu shida ya dada yako (sema ukweli unaohusika hapo tu, kweli zingine ni baina yako na Mungu mpaka uingie nazo kaburini). Mkiweza kuishi nae mbali kijiografia itakuwa vyema pia.

hiki kisa ni cha kweli kabisa hata ukitaka kunitafuta niko sawa tuu, ni kweli nimepokea ushauri wenu na nimeelewa vizuri, kesho mapema nitaenda kuongea na mchumba wangu then nitaeleza atakavyonijibu
 
pole sana, hapo dada huna. kinachomsumbua ni wivu tu na hakuna kingine.. anajisikia vibaya ukiolewa kabla yake, na kwa tabia zake it seems yeye hana utayari wa kuolewa ila kuharibu tu.

kaa chini na mchumba ako mweleze tabia zake, yeye mwacheni atajua last minute.

kila la kheri mami, ukifanikisha kaa macho naye asije kukaribia ndoa huyoo.

asante sana nitalifanyia kazi kesho jumapili
 
Da sijawai kuumia kama hivi, haa huyo mwanamke anawivu sana, roho mbaya. Mungu atamuumbua tu siku za mbeleni. Muombe sana mungu maana yeye ni kila kitu kwenye ndoa yako...

hakuna kilichoniuma kama ile ndoa ya 2011 na mjapani wangu kila kitu kilikuwa sawa kaja kuniharibia kiukweli mpaka nimekuja kujiunga huku nikwa ajili ya hili, ila nimeona ni sehemu nzuri sana kwa kufarijiwa na kuelekezwa usichokijua, hili swala la kumweleza mchumba wangu nitafanya kesho
 
Xian mweee.. utanisamehe mami, sijui kwanini kuna kitu kinaniambia ninyi ni wamachame.

wanachame wanisamehe pia, just kubuni. Huyo dada ni komesha ptuuuuuuu mbaka.
 
Last edited by a moderator:
Kweli msumulie mchumba au atakutia aibu mbele yake na ndugu zake.

Yeye akijua atajua cha kuwaambia ndugu zake bila kuharibu yeye kukukimbia akidhani anaingia kwenye familia ya ajabu.

Huyo dada nyamaza apate mmshtuko ni wivu tu, sasa mweleze wako na sema dada huyo hayupo hapo mjini danganya

yupo mkoa mwingine ili asikushangae na usiseme yote ya mliopanga na familia yako kumficha atawashangaa sana na kuogopa.

Mweleze tu tabia ya dada na matukio labda mawili na sema mila na desturi zikafanya iwe hivyo usikubaliwe kuolewa. Usiongeee sanaaaaaaaa labda mbeleni mkishaoana eeehhh

Na ukiolewa usimkaribishe dada kulala kwako akija aje na wazazi au sema haupo akitaja kuja kukutembelea. Mchawi wako huyo hatakuachia kwa kutaka kulipizia kuwa ulimgundua akashindwa kukuzuia tena. Kaa nae mbali maishani mwako na ndoa yako kabisa au utakoma vituko atakavyofanya huyo.

ok, nimejifunza kitu hapa asante sana, nisimwambie mchumba kuwa tulimuondoa kwa kuwa wewe ulikuwa unakuja italeta picha mbaya, asante nitajua kuyaweka sawa, pia ni mtu mzima kwangu hivyo ni mwelewa sana nimeshamsoma ni mtu mstaarabu sana
 
duh!pole sana!mi nahisi umfahamishe huyo mchumba hali halisi kwa mazingira ya nyumbani anaweza akajua anytime,nawatakieni maandalizi mema na mwisho maisha mema ya ndoa!

Nadhani ataleta Uzi mwingine wa ndoa Hapa,Kama sijakosea wacha tusubiri ....
 
Xian mweee.. utanisamehe mami, sijui kwanini kuna kitu kinaniambia ninyi ni wamachame.

wanachame wanisamehe pia, just kubuni. Huyo dada ni komesha ptuuuuuuu mbaka.

hapana sisi siyo wamachame, baba yetu ni msukuma na mama ni mbagganda
 
Pm picha tu namba atanipa mwenyewe huyo mkorofi atanifaa mkorofi mwenzake
Pale sana
 
Chunga sana,huyo hakawii kumtega mumeo ili tu kulitibua.
 
Mh kweli kua uyaone, kuna vitu ndugu wa damu wanafanyiana mtu unabaki midomo wazi.
Mueleze mchumba wako hali halisi hata kama dada hatoambiwa lolote. Maana hata yeye akijua dadayako hajui kitu anaweza kufikiri wewe ndo kuna jambo linalokuhusu hutaki alijue hii inaweza ikamtatiza kwenye kukuamini.
 
Back
Top Bottom