Naombeni ushauri kuhusu tabia ya dada yangu

Naombeni ushauri kuhusu tabia ya dada yangu

Picha yake tu inanitosha sbb umeshasema yupo wapi nitamaliza mwenyewe huyo ananifaa kabisa kuwa wangu sbb napenda wakorofi kama hao,kama hutojali nipm tu picha yake
 
mwambie namtaka ntampa anachotaka na hvyo vijisenti vyake vya carolite atatulia 2 ni pm
 
pole dada yako ana wivu. jealous is disability. Je huyu wa sasa kama ni mtu muelewa atakuwa by your side. BUT U ALSO NEED TO STAND UP ON UR OWN. DADAKO UBAKI UNDUGU ILA MAMBO YAKO USIMSHIRIKISHE SIO MTU Mzuri. Najua atakununia ila chunga sana. usikubali awe na mawasiliano ama mazungumzo yeyote na mumeo mtarajiwa. she is a bichywitchy. lol

asante sana niliongea na mchumba wangu jana na amenielewa sana
 
Wapendwa samahani sana kwa usumbufu,

Nina kitu ambacho kwa kweli kinaniumiza moyo wangu sana, sisi kwetu tumezaliwa wawili na wote ni wasichana, dada yangu ni mkubwa kwangu kwa miaka saba hajaolewa na kwa kweli sijawahi kuona yuko na mwanaume ambaye wanadumu kwa muda hata kwa wiki mbili.

Akiwa na mtu yeye ni mtu wa kumfokea mwanaume na kumtukana hivyo ni dada mwenye kazi nuzri msomi kiasi ila tatizo lake ni hilo.

Shida yangu kubwa iliyonifanya niilete hapa kila nikipata mchumba akija nyumbani kujitambulisha dada yangu anadai ni mpenzi wake wa zamani na maneno hayo anawaeleza wazazi hivyo yule mwanaume hawezi kukubaliwa kuendelea na mimi.

Mara ya kwanza nilijua kweli huyo kaka hakulalamika akaondoka zake ni muda mrefu sana, nikapata mwingine dada akadai hivyo nina amini kwa kuwa tanzania kubwa.

Cha kushangaza nikapata mwanaume wa nchi nyingine nimemleta Tanzania kwa ajili ya kujitambulisha dada yangu baada ya muda akadai yule baba atembea nae kipindi hiki nilichokuja nae Tanzania.Kiukweli niliumia sana.

Yule Mjapan akatuona sisi washenzi akaondoka zake yamebaki mawasiliano ya kawaida tuu. Mungu kanikumbuka tena nimepata jamaa mwingine, baba akashauri tupange tarehe ambayo dada hayupo, na kweli kila kitu kilienda sawa.

Harusi yangu inakaribia sana na mpaka sasa dada yangu hawajawahi kuonana na mchumba wangu huyu mpya na hajapata uhakika kama kweli nina mchumba kwani hata pete ya uchumba sivai kwa kumuogopa yeye.

Naomba ushauri je! nimweleze ukweli dada kuwa nina mchumba ila tamuona siku ya harusi?

Au nimweleze mchumba tabia za dada ili hata likitokea awe anajua?

Baba zangu wadogo wanashauri asiambiwe kitu na siku ya harusi astukizwe tuu kwani hakutakuwa na sherehe kubwa ni lunch tuu na vinywaji.

Asanteni nina imani mmenielewa.

Nisaidieni

Binti una bahati sana. Hongera kwa uamuzi wa kuolewa.
Naona kuwa mahusiano yako na ya dada yako inabidi yaheshimike no matter tabia zake hizo. Nahisi anasumbuliwa na upweke na anaona ueye anastahili kuolewa kabla yako sababu ni mkubwa.
Wewe endelea na mipango yako. Lakini ni vyema pia kuhakikisha dada anafahamu habari hizi sababu haipendezi ndugu wa tumbo moja wasiambiane mambo nyeti kama hili la ndoa. Aambiwe na wazazi kuwa unaolewa na asihusishwe kwenye maandalizi. Muwaze nayeye jinsi atajisikia akipata taarifa hizi kwa majirani! Huenda ikawa mbaya zaidi kwenu wote.
Kila lakheri
 
asante sana
 
Mi ningekushauri uwe unamtambulisha washkaji zako kua n wachumba zako wawe wanajipoone kama huna washkaji ni pm nije nijiponeamo humo. Hakuna mwingine anae taka kwenda kutambulishwa akapone. Dawa ndo hiyo huku unamficha mchumbaako asimuone.
 
Back
Top Bottom