Desierto
JF-Expert Member
- Aug 26, 2019
- 847
- 2,954
Nimepata mdau ameniomba aweke mtaji kwenye ofisi yangu kesho ndo nataka nikamsikilize.
Ila ni kuongeza bidhaa ofisini
Mm plani yangu ni kama ataongeza mtaji basi nilitaka nimwambie mtaji wake tuweke kwenye simu ndogo za batani radio za kuchajisha na sabufa zisizo zidi Bei ya 120
Na bidhaa completel mfano majagi pasi za umeme NK. Ila mm nibaki na kuuza tu vifaa mfano hapo kwenye picha.
Sasa wadau naomba mnipe mawazo je nifanye naye maongezi au nitemane naye tu.
Maana muuzaji nakuwa mm na faida tutagawanaje mfano labda iteli ndogo tumenunua 24 halafu tukauza 30 faida inakuwa ni 6000 je mgao utakuwaje hapo? Ofisi ni yangu na Kodi nalipa mm.
Ni mdada kwa mwonekano ni watu wanaojitambua.
Je? Ni mwekee kiwango gani Cha mtaji Cha kuanzia kisiwe chini ya kiasi Fulani?
Hili wazo kwangu pia naliona kama sio baya sababu maduka kadhaa mjini naonaga Kuna vijana wanauza au kufanya kwa pamoja.
Je nifanye taratibu zipi ili ukitokea usumbufu mbele labda usijekuniathiri pia kwenye ofisi yangu?