Naombeni ushauri jamani

A girls always deep down in prayers pleading to the Almighty God for the Super Loving Husband.... Mimi naona hapa tatizo ni mwanamke kumpenda mwanamme ambaye hakupendi. Ni rahisi kugundua! If a man can't even call you once in a day let alone meeting you in month (nafikiri binti atatafutwa wakati jamaa atataka kumaliza shida zake za ulijali) jua kwamba hauko moyoni mwake, tafuta hamsini nyingine.

Sasa katokea njemba nyingine ni 45 yrs old.. what in the name of God was this man waiting for in order to get married? Miss / Mrs Right? Au alikuwa shule ndo kamalizia Phd yake. a lot has to be scrutinised au ndo kafiwa na wanawake labda wengi ambao hakuwahi kuzaa nao? There must be a very good convincing reason as to his delay to get married.

Ila ukichunguza saana kuku hutomla. Don't let this new man get what it takes to be the 'nuclei of marriage happiness' (msibanjuane) before marriage. Jitangazeni koote na uone if this new mchumba doesn't 'chicken out' of the uchumba. OTHERWISE age doesn't count in marriage.

I got married at 48 to the girl of 30. We have three children now and we are happy.

nimependa ushauri wako!
 
But be care na huyo wa pili pia. Unahitaji utulivu na usikivu wa ki_Mungu zaidi ya maslahi na haja ya kuolewa. Je mna uhakika kweli Mungu kawajibuni maombi yenu au ni akili zenu baada ya upenyo kujitokeza.
 
Binti asiwache hiyo opportunity la muhimu ni wenyewe kupendana na kukubaliana. Muda unakimbia na anahitaji kuanzisha familia.

Aangalie watoto jee wanamkubali? Maana hicho ndicho kitakuwa kikwazo kikubwa na hasa ikiwa ana binti. Kwa kawaida mabinti huwa hawapendi kuona baba zao wameoa wake vijana ambao watapata attention zaidi ya wao.

Jamani mbona munaleta kikwazo cha umri? Mimi na husband wangu mbona tofauti yetu ya umri ni 10+ lakini mpaka sasa tunaendelea vizuri tu miaka mingi imeshapita baada ya kuoana. Hivi sasa tuna mtoto mkubwa tu na namshukuru Mungu wale wengine hawakuleta matatizo.
 
hivi kwa nini watu wengine hupenda omba ushauri
kwa jambo unaloona kabisa lipo wazi?
 
Miezi 2 tu unawazia ndoa? upo desperate kiasi hicho? tulia msichana kama kweli unaomba utapata tu mume. miezi miwili ni michache sana kumwazia mtu kuwa mwenzi wa maisha
 
Kwanza kabisa mwambie anatatizo ambalo wasichana wengi wanalo la kutaka kuolewa tu bila kutaka kufanya utafiti na kujiridhisha na muoaji anayestahili. Pili yupo kwenye kundi la wasichana ambao hawana ujuzi wa kutambua muoaji huwa anavigezo gani (Tatizo hilo linawakabili wasichana wengi). kimsingi ni kuwa wote hao wawili hakuna muoaji, na yeye tayari ameshagundulika kuwa anahitaji kuolewa, hilo ni kosa kubwa ambalo wanawake/wasichana wanalifanyanya na ni mtego rahisi wa kuwanasa. Nasikitika kwamba kuna mambo kadhaa ambavyo siwezi kuyataja hapa kwenye JF ambavyo yangemsaidia kujua tabia za wanaume. mwambie awe mwangalifu na wanaume. hata hivyo mwambie bado hajapata mtu wa kumuoa!!!!! hao wote mambo yao ni.... :spit:

tusaidie mkuu kutambua hizo tabia za wanaume, wote hapa ni wakubwa tu
 
Age is no big deal!
Ila tofauti ya miaka 18 naona kama ni mingi sana ....:confused2: Sina la kuongea sana kama wamependana kwa dhati na mapenzi ya kweli waendelee na mipangilio yao mingine..kinachomata sana kama true love iko ndani yao mungu awasimamie ...Pia naomba huyo dada awe amefanya maamuzi toka moyoni mwake
Sio kama anatamani sana kuolewa au anaona umri unaenda na yule aliyempenda kwa dhati haonyeshi nia yoyote asijekujutia maamuzi yake baadae .
 
Mimi naona huyo wa kwanza hamfai huyu binti, huyo wa pili nae naona hamfai kwa sababu:
Kwanza huyo wa pili kwa inavyoonekana amekaa na mke wake about 20 years! kwani mtoto wa kwanza ana miaka 19. Ina maana hata baada ya 20 years mke wake alishindwa kuvumilia tabia yake au kuizoea hiyo hali aliyokuwa nayo mume wake, ni ngumu kwa huyu binti kuja kuzoea hali hiyo, itafika wakati yeye pia ataona alikosea kumchagua!!

Pili huyo mume si mtanzania, huyu dada hajui vizuri mazingira ya huyu baba, hajui maisha yake ameishije, watu huwa tunajua tabia ya mtru kwa kuangalia pia marafiki zake, sasa inavyoonekana huyu dada hajui hata marafiki wa huyu baba, so ni wazi hajui tabia yake vizuri, kwa sababu amempenda ni rahisi kusema ana tabia njema kwa sasa!!!

tatu huyu dada 25 bado ni binti mdogo, akubali kwamba kuna tabia nyingine au vitu alivyotamani kufanya akiwa kama kijana hataviona kwa huyu baba, automatically mtu anapokuwa huwa kuna vitu vinabadilika, maqmbo alityokuwa akifanya kwenye late 20's siyo ndio atakayofanya kwenye late 40's.

Nne huyu baba sijui utamaduni wa kwao ulivyo, lakini anaweza ikafika wakati akamuona kama mwanae hivyo akahitaji heshima kama ambayo angeipata kwa watoto wake, ambayo si sawa, huyu atakuwa ni mke si mtoto.

BUT ALL IN ALL KAMA AMEPENDA AOLEWE, AKIPENDA HATA YAKIJA KUTOKEA HATAJUTA, SABABU ALIPENDA.
 
ah ah ah Bramo,ingekuwa mm kwann nikudanganye?hujui mficha uchi hazai?sina sababu ya kudanganya bana
Usituzuge bana,huyo bint atakuwa wewe tu,usione Noma.
Kabla hujamkubalia huyo wa pili fanya hesabu hii ndogo.
45-27=18.
huyo wa pili atazeeka haraka sana na kukuacha bado bint mbichi,hivyo basi ashakumu si matusi,dada ujiandae kukaa EDA NA KUOLEWA KWA MARA YA PILI
 
ndio.....

ukweli ni kwamba tuseme huyo binti,27, kinachomvuta hapo ni pesa tu!hebu tuchukulie kuwa huyo jamaa wa 45 yrs angekuwa hana kitu, halafu katangaza ndoa!binti angekubali?tuwe wazi tu!
 
ukitembea huku mvua ikisnyesha jiandae kukanyaga dimbwi na tope seuse kulowa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom