Shukran sana mkuu, hata mimi nimejifunza kitu hapaSorry for late response, Kwa jinsi nilivyosoma uzi wake, inaonyesha mkewe amepoteza mimba takribani 3 hadi 5 mfululizo.kitaalamu tunaita BOH (Bad Obstetric History),
na kwakuwa kuna mfuatano wa miezi inayofanana kuna percent kubwa ikawa ni Cervical Incompetence..
pia nakubaliana na wengine waliosema ni ABO incompability
BOH (Bad Obstetric History) inaweza kusababishwa na vitu kadhaa kama Upungufu wa Homoni inayoitwa Progesterone (Hormonal Imbalance) Ili mimba itungwe na kukua, mwili unahitaji kiasi cha kutosha cha hiyo homoni Ikiwa homoni hii ipo chini, mfuko wa uzazi unashindwa kuishikilia mimba changa, na hivyo kutoka kwa njia ya mabonge ya damu ndani ya mwezi mmoja au miwili. so anatakiwa kufanya kipimbo cha Hormonal profile ili kujua kama hakuna tatizo la hormone lolote..
lakini anaweza kuwa na Hitilafu kwenye mfuko wa uzazi yaani Uterine Anomalies Huenda kuna uvimbe Fibroids au hata cyst, makovu kwenye mfuko wa uzazi kutokana na kusafishwa mara kwa mara ambayo tunaita Asherman's Syndrome, au umbo la mfuko wake wa uzazi lina shida inayozuia mtoto kupata nafasi ya kukua...
pia kunaweza kuwa na Maambukizi ya magonjwa Magonjwa sugu ya maambukizi, hasa tunaogopa sana kundi la magonjwa yanayojulikana kama TORCH, yanaweza kusababisha mimba kuharibika kila ikitungwa. hiyo TORCH ni (kifupi cha magonjwa kama T - Toxoplasmosis, O - Other infections (kama vile Kaswende/Syphilis, Homa ya Matumbo, na HIV), R - Rubella (Surua ya Ujerumani), C - Cytomegalovirus (CMV) na H - Herpes simplex virus (HSV)...
sasa nashauri nini...
kwanza anatakiwa kumuona daktari Bingwa wa magonjwa ya Kike kwa uchunguzi na ushauri ..siku hizi hata kama ana tatizo la cervical incompetence anaweza kuwekewa Shirodkar stitch au wengine wanaita Cervical Cerclage,
McDonald stitch)..
- Msijaribu kutafuta mimba nyingine kwa sasa. Kila mimba inapotoka na kusafishwa, mfuko wa uzazi unachoka na kuongeza hatari ya mimba ijayo kutoka.
- Mnapoenda kumuona Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kina Mama (Gynecologist), hakikisha unaenda naye. Usiache aende peke yake. Daktari atawapa ushauri wote na huenda akakuelekeza kumuona Daktari wa Mfumo wa Uzazi wa Wanaume (Urologist).
- Kama alivyosema "anahisi amelogwa", huyu mama anamchosha kiakilin maana anbamfanya aaenze kuwaza . Kazi yake kubwa sasa hivi ni kumhakikishia kuwa wako pamoja kweny hilo wala asimtenge wa;a kumnyanyapaa amwambie wazi kuwa hata upande wake (mwanaume) unaweza kuwa unachangia, hivyo mtapambana kupata matibabu wote wawili. hii itamfanya awe na amani
Mributz , ushauri fasaha wa kitabu kutoka kwa Daktari bingwa huo hapo, achana na ulozi na mambo ya waganga, Mungu akusimamie upite huu mtihani