Naombeni msaada mimba ya 5 sasa inatoka

Naombeni msaada mimba ya 5 sasa inatoka

Habarini wana jamvi

Mimi na mke wng tuna mtoto mmoja sasa amekua miaka 8 nahitaji mtoto wa pili
Sasa kila akishika mimba inavyofikisha miezi miwili inatoka.

"Nakumbuka ya kwanza kabisa kutoka mtoto alikuwa na miezi 3 alifia tumboni wakati sisi tunajua mimba ina miezi saba tulivyoenda utra sound tukaambiwa mtoto kafariki akiwa na miezi 2. Tokea apo zinazofata mimba ikifika mwezi tu akienda chooni anatokwa na mabonge ya damu mimba zinaharibika.

Tukikaa mwezi anashika mimba vizuri kabisa ikifikisha mwezi au miezi 2 inatoka
Naombeni msaada wana jamii nawaomba sana kama kuna mwenye mawazo utaaalamu
Imefika hatua mke wangu anasema amelogwa
Nitafute, nikueleke dawa utapata msaada. Ila uombe Mungu wivu unawasumbua watu
 
Nimekuchek dm
Mkuu achana na hizo mambo!
Kama bado hamjapima Rhesus factor nenda kapimeni,
Pia jitahidini mimba ikitoka mama apumzike miezi 6 kabla ya kubeba mimba nyingine.
Najua ukiwa na hamu ya kupata mtoto ni ngumu kusubiri hiyo miezi ila ni muhimu sana.
Na akipata ujauzito mnapogundua tu aende hospital kuna dawa atapewa pamoja na kuwekwa bedrest Inshaalah Mungu atawasaidia!
 
Akishika tu ujauzito nenda kwa mtaalam akupe dawa inaitwa duphaston!bei yake imechangamka!!kidonge kimoja 2500 Hadi 3000!!itasaidia hako kajamaa kujishikiza vizuri na kukaza kwenye ukuta wake!!

Kama aliwahi kutumia uzazi wa mpango kuzuia mimba baada ya huyo mzaliwa wa kwanza ! obviously hicho hutokea mara nyingi! Hormonal imbalance hiyo!!

Jaribu
 
Mkuu achana na hizo mambo!
Kama bado hamjapima Rhesus factor nenda kapimeni,
Pia jitahidini mimba ikitoka mama apumzike miezi 6 kabla ya kubeba mimba nyingine.
Najua ukiwa na hamu ya kupata mtoto ni ngumu kusubiri hiyo miezi ila ni muhimu sana.
Na akipata ujauzito mnapogundua tu aende hospital kuna dawa atapewa pamoja na kuwekwa bedrest Inshaalah Mungu atawasaidia!
Bado najiuliza miaka 8 yote hakuna daktari aliyewaambia tatizo ni nini
Watz wengi wanapenda kuchukua ushauri wa mitaani badala ya kwenda kuona wataalamu wa afya.
 
Usikute unamstress wife wako wakati akiwa na ujauzito

Hakikisha akipata ujauzito humstress na hamgombani hovyo
Pia kama ushagundua tatizo akifikisha tu miezi mitatu usimhangaishe na mambo ya kutembea sana au kupanda boda

All in All, anza kumwona Dr. wa Wanawake mapema sana aanze kumfanyia Monitoring immediately mimba ikiingia

Good luck.
 
Wanawake wamejaa duniani kwani lazima mimba zako zote abebe yeye? Tafuta wanawake wengine zalisha
Nyie vijana wa sikuhizi mpoje?
 
Mm nakuja nje ya box kidgo Wataalamu wataongezea .
Kuna issue inaitwa Rhesus factor (Rh) ambayo kila mmoja wapo anayo yakwake .
Inasifa hizi mwanamke ndio anayebeba kiumbe tumboni mwake katika damu yake ana (Rh) yakwake na kiumbe kinachoingia tumboni huwa na (Rh) ambayo inatokana na mchanganyiko wa baba na mama

Ikoje ?
Ikitokea Rh ya mtoto aliyetumboni ikaenda kinyume na Rh ya mama kwa mara yakwanza uwezekano wa kujifungua mtoto salam ni asilimia 100%

Baada ya kujifungua nini hufanyika
Akijifungua ubongo unabeba kumbukumbuku kuwa kuna kiumbe kilikuja katika mji wa mimba kikavamia matokeo yake ,mwili wa mama unajenga kinda kuja kupambana na hali ya kiumbe kinachokuja kwa wakati unaokuja .

Mimba nyingine nini hutokea?
Baada ya mama kubeba mimba ya pili na Rh ya mama na ya mtoto kwakua hazifanani mwili unaamulu kukiua kiumbe kile mwili ukijua kuwa hiki kiumbe si salama kwa mama .

⚠️ jaribu kufika kujua Rh zenu na uchunguzi zaidi .
🤣😂🤣 Mnapenda kudanganyana, ukweli ni kwamba sababu za mimba kuharibika mara kwa mara ni kutokana na mwanamke hapo nyuma kutumia P2 na kutoa mimba mara kwa mara.
Mwanamke anajua ukweli kwanini mimba zinaharibika ndio maana kakimbilia kusema amerogwa 😂
 
Mm nakuja nje ya box kidgo Wataalamu wataongezea .
Kuna issue inaitwa Rhesus factor (Rh) ambayo kila mmoja wapo anayo yakwake .
Inasifa hizi mwanamke ndio anayebeba kiumbe tumboni mwake katika damu yake ana (Rh) yakwake na kiumbe kinachoingia tumboni huwa na (Rh) ambayo inatokana na mchanganyiko wa baba na mama

Ikoje ?
Ikitokea Rh ya mtoto aliyetumboni ikaenda kinyume na Rh ya mama kwa mara yakwanza uwezekano wa kujifungua mtoto salam ni asilimia 100%

Baada ya kujifungua nini hufanyika
Akijifungua ubongo unabeba kumbukumbuku kuwa kuna kiumbe kilikuja katika mji wa mimba kikavamia matokeo yake ,mwili wa mama unajenga kinda kuja kupambana na hali ya kiumbe kinachokuja kwa wakati unaokuja .

Mimba nyingine nini hutokea?
Baada ya mama kubeba mimba ya pili na Rh ya mama na ya mtoto kwakua hazifanani mwili unaamulu kukiua kiumbe kile mwili ukijua kuwa hiki kiumbe si salama kwa mama .

⚠️ jaribu kufika kujua Rh zenu na uchunguzi zaidi .
Hii hutokea kwenye makundi ya damu. Ikiwa mama ana blood group lenye Rh - halafu kiumbe kinachoingia kina +Rh maana yake ni kitu kipya kinaingia mwilini mwa mama so kinga zake za mwili zinapambana nacho hivyo kiumbe kinakufa na ndo mimba zinaharibika.
 
Tuambie group lako la damu na la mkeo pia,tuanzie hapo kwanza.
 
Fanya kwenda hospitali za mabingwa mkaangalie afya ya mama pamoja na group za damu zenu...
 
Usikute unamstress wife wako wakati akiwa na ujauzito

Hakikisha akipata ujauzito humstress na hamgombani hovyo
Pia kama ushagundua tatizo akifikisha tu miezi mitatu usimhangaishe na mambo ya kutembea sana au kupanda boda

All in All, anza kumwona Dr. wa Wanawake mapema sana aanze kumfanyia Monitoring immediately mimba ikiingia

Good luck.
Asante
 
Back
Top Bottom