Naombeni msaada mimba ya 5 sasa inatoka

Naombeni msaada mimba ya 5 sasa inatoka

Mributz hadi kufika mimba 5 bado tu unakaa na mwanamke nyumbani bila ya kwenda kwa wataalamu wa afya nina mashaka na uleaji wa mimba ikiwemo mwanamke kwenda clinic je huwa anaenda na kama anaenda huenda alificha kinachomsibu kipindi cha nyuma na hiki ndicho kitu ambacho wagonjwa wengi wanaficha ,hamjui kwamba historia ya ugonjwa/tatizo la nyuma likaleta changamoto nyingi nakushauri mfike hospital haraka sanaaa,Rhesus incompactibility,hormone imbalance,stress,previous history of abortion,use of contraceptive method,infections can be a major source/cause of recurrent miscarriage so hospital visiting is important
 
Asante
 
23897.jpg
23901.jpg

Tumeenda hosptal jana kapewa dawa hizi atumie
 
Kacheki Rhesus Factor.Kama anayo atatumia sindano ya Ant D
Mributz unajua kundi lako la damu na la mkeo???? Hii ilishamtokea workmate mmoja hivi .Chakufanya nenda hospitali waelezee watawapima blood grupu nakuwapa maelekezo..

Wanasema ikiwa mmoja ana O- mwingine nininini sijui 1st born ndo atasurvive mimba zinazofuata ........

Huyo workmate alienda hospitali kuna maelekezo ya sindano alipewa ambapo sindano hio huchomwa mwanamke mimba ikiwa miezi mingapi sijui nyingine huchomwa masaa 72 baada ya kujifungua.

Naye mkewe ziliharibika mimba kama nne tano hivi . Saii ana mtoto wapili mwenye afya njema tu

Cc Smart911
 
Mm nakuja nje ya box kidgo Wataalamu wataongezea .
Kuna issue inaitwa Rhesus factor (Rh) ambayo kila mmoja wapo anayo yakwake .
Inasifa hizi mwanamke ndio anayebeba kiumbe tumboni mwake katika damu yake ana (Rh) yakwake na kiumbe kinachoingia tumboni huwa na (Rh) ambayo inatokana na mchanganyiko wa baba na mama

Ikoje ?
Ikitokea Rh ya mtoto aliyetumboni ikaenda kinyume na Rh ya mama kwa mara yakwanza uwezekano wa kujifungua mtoto salam ni asilimia 100%

Baada ya kujifungua nini hufanyika
Akijifungua ubongo unabeba kumbukumbuku kuwa kuna kiumbe kilikuja katika mji wa mimba kikavamia matokeo yake ,mwili wa mama unajenga kinda kuja kupambana na hali ya kiumbe kinachokuja kwa wakati unaokuja .

Mimba nyingine nini hutokea?
Baada ya mama kubeba mimba ya pili na Rh ya mama na ya mtoto kwakua hazifanani mwili unaamulu kukiua kiumbe kile mwili ukijua kuwa hiki kiumbe si salama kwa mama .

⚠️ jaribu kufika kujua Rh zenu na uchunguzi zaidi .
Hapa umemaliza kila kitu kwa maana mm naye ni miongoni mwa watu ambao wake zao wana group la damu negative (-) kila mimba mke wangu anachoma sindano mbili za ant-D nadhan gharama yake inategemeana na eneo ila huwa ni kuanzia 120k hadi 150k hivyo nakushauri Mributz nenda kwanza ukapime group lako na la damu mke wako kama mkeo atakuwa na negative basi hajarogwa bali mfuate tu ushauri wa kutaalamu
 
Tuwa
Habarini wana jamvi

Mimi na mke wng tuna mtoto mmoja sasa amekua miaka 8 nahitaji mtoto wa pili
Sasa kila akishika mimba inavyofikisha miezi miwili inatoka.

"Nakumbuka ya kwanza kabisa kutoka mtoto alikuwa na miezi 3 alifia tumboni wakati sisi tunajua mimba ina miezi saba tulivyoenda utra sound tukaambiwa mtoto kafariki akiwa na miezi 2. Tokea apo zinazofata mimba ikifika mwezi tu akienda chooni anatokwa na mabonge ya damu mimba zinaharibika.

Tukikaa mwezi anashika mimba vizuri kabisa ikifikisha mwezi au miezi 2 inatoka
Naombeni msaada wana jamii nawaomba sana kama kuna mwenye mawazo utaaalamu
Imefika hatua mke wangu anasema amelogwa
Tuwasiliane naweza kukusaidia kiroho na kimaarifa
 
Asante
Hapa umemaliza kila kitu kwa maana mm naye ni miongoni mwa watu ambao wake zao wana group la damu negative (-) kila mimba mke wangu anachoma sindano mbili za ant-D nadhan gharama yake inategemeana na eneo ila huwa ni kuanzia 120k hadi 150k hivyo nakushauri Mributz nenda kwanza ukapime group lako na la damu mke wako kama mkeo atakuwa na negative basi hajarogwa bali mfuate tu ushauri wa kutaalamu
Sante
 
1. Tafuta gynecologist

2. Nenda madhabahuni kwa nabii NICOLOUS SUGUYE
"Uwe hai, YESU YU HAI"
 
Habarini wana jamvi

Mimi na mke wng tuna mtoto mmoja sasa amekua miaka 8 nahitaji mtoto wa pili
Sasa kila akishika mimba inavyofikisha miezi miwili inatoka.

"Nakumbuka ya kwanza kabisa kutoka mtoto alikuwa na miezi 3 alifia tumboni wakati sisi tunajua mimba ina miezi saba tulivyoenda utra sound tukaambiwa mtoto kafariki akiwa na miezi 2. Tokea apo zinazofata mimba ikifika mwezi tu akienda chooni anatokwa na mabonge ya damu mimba zinaharibika.

Tukikaa mwezi anashika mimba vizuri kabisa ikifikisha mwezi au miezi 2 inatoka
Naombeni msaada wana jamii nawaomba sana kama kuna mwenye mawazo utaaalamu
Imefika hatua mke wangu anasema amelogwa
Hypersensitivity type two hiyo😮,

Dawa haina
 
Mkuu kama nakujua vile,wewe ndo yule umeona madam mwenye jina la C.M.M au!? Naye ana mtoto Mmoja akiwa na lundo la mimba kutoka.

Pole sana kama ndo wewe
 
Pole sana
cc DR Mambo Jambo hebu njoo utoe ushauri huku
Niliwahi kuona mada moja unashauri kuna sindano wanachomwa ili kuzikabili homoni za kiume zikizidi kwenye uja uzito ili mimba isiharibike, sikosei, ila wewe mtaalamu utamsaidia zaidi
Sorry for late response, Kwa jinsi nilivyosoma uzi wake, inaonyesha mkewe amepoteza mimba takribani 3 hadi 5 mfululizo.kitaalamu tunaita BOH (Bad Obstetric History),
na kwakuwa kuna mfuatano wa miezi inayofanana kuna percent kubwa ikawa ni Cervical Incompetence..

pia nakubaliana na wengine waliosema ni ABO incompability

BOH (Bad Obstetric History) inaweza kusababishwa na vitu kadhaa kama Upungufu wa Homoni inayoitwa Progesterone (Hormonal Imbalance) Ili mimba itungwe na kukua, mwili unahitaji kiasi cha kutosha cha hiyo homoni Ikiwa homoni hii ipo chini, mfuko wa uzazi unashindwa kuishikilia mimba changa, na hivyo kutoka kwa njia ya mabonge ya damu ndani ya mwezi mmoja au miwili. so anatakiwa kufanya kipimbo cha Hormonal profile ili kujua kama hakuna tatizo la hormone lolote..

lakini anaweza kuwa na Hitilafu kwenye mfuko wa uzazi yaani Uterine Anomalies Huenda kuna uvimbe Fibroids au hata cyst, makovu kwenye mfuko wa uzazi kutokana na kusafishwa mara kwa mara ambayo tunaita Asherman's Syndrome, au umbo la mfuko wake wa uzazi lina shida inayozuia mtoto kupata nafasi ya kukua...
pia kunaweza kuwa na Maambukizi ya magonjwa Magonjwa sugu ya maambukizi, hasa tunaogopa sana kundi la magonjwa yanayojulikana kama TORCH, yanaweza kusababisha mimba kuharibika kila ikitungwa. hiyo TORCH ni (kifupi cha magonjwa kama T - Toxoplasmosis, O - Other infections (kama vile Kaswende/Syphilis, Homa ya Matumbo, na HIV), R - Rubella (Surua ya Ujerumani), C - Cytomegalovirus (CMV) na H - Herpes simplex virus (HSV)...

sasa nashauri nini...
kwanza anatakiwa kumuona daktari Bingwa wa magonjwa ya Kike kwa uchunguzi na ushauri ..siku hizi hata kama ana tatizo la cervical incompetence anaweza kuwekewa Shirodkar stitch au wengine wanaita Cervical Cerclage,
McDonald stitch)..

  • Msijaribu kutafuta mimba nyingine kwa sasa. Kila mimba inapotoka na kusafishwa, mfuko wa uzazi unachoka na kuongeza hatari ya mimba ijayo kutoka.
  • Mnapoenda kumuona Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kina Mama (Gynecologist), hakikisha unaenda naye. Usiache aende peke yake. Daktari atawapa ushauri wote na huenda akakuelekeza kumuona Daktari wa Mfumo wa Uzazi wa Wanaume (Urologist).
  • Kama alivyosema "anahisi amelogwa", huyu mama anamchosha kiakilin maana anbamfanya aaenze kuwaza . Kazi yake kubwa sasa hivi ni kumhakikishia kuwa wako pamoja kweny hilo wala asimtenge wa;a kumnyanyapaa amwambie wazi kuwa hata upande wake (mwanaume) unaweza kuwa unachangia, hivyo mtapambana kupata matibabu wote wawili. hii itamfanya awe na amani
 
Endelea kupambana mkuu, jaribu kubadli dr. Bingwa, hawa wataalam wanazidiana,, yaani hapo Ultrasound za kufikia akishabeba mimba tena, baada ya wiki mnaenda kuchek, msingoje ifike miez 2,
Hata akihisi tofaut yoyote ile we chap mpeleke wakamchek,, akijamba tu we chap unampa pole 😁
 
Habarini wana jamvi

Mimi na mke wng tuna mtoto mmoja sasa amekua miaka 8 nahitaji mtoto wa pili
Sasa kila akishika mimba inavyofikisha miezi miwili inatoka.

"Nakumbuka ya kwanza kabisa kutoka mtoto alikuwa na miezi 3 alifia tumboni wakati sisi tunajua mimba ina miezi saba tulivyoenda utra sound tukaambiwa mtoto kafariki akiwa na miezi 2. Tokea apo zinazofata mimba ikifika mwezi tu akienda chooni anatokwa na mabonge ya damu mimba zinaharibika.

Tukikaa mwezi anashika mimba vizuri kabisa ikifikisha mwezi au miezi 2 inatoka
Naombeni msaada wana jamii nawaomba sana kama kuna mwenye mawazo utaaalamu
Imefika hatua mke wangu anasema amelogwa
Pole sana mkuu! mwamini YESU!
 
Back
Top Bottom