NAOMBENI MBINU YA KUPATA WAGONJWA.

NAOMBENI MBINU YA KUPATA WAGONJWA.

Unatamani kufanya kwa moyo wako wote kwa ustawi wa kituo sio jamii kwa kuisaidia? Uko vizuri mkuu.
Fanya hivi, tengeneza ugonjwa kisha tengeneza dawa yake baada ya hapo ambukiza watu ili wafuate dawa kwako tu kwa ustawi wa kituo.

Kituo hakiwezi kustawi kwa kutoa huduma mbovu, hichi ulicho nishauri kitakuwa na ustawi hasi. Asante kama hichi ndicho uliona ni mchango ktk hili
 
Mh hii Kali, omba sana hata mlipuko wamagonjwa utokee.

"zingatia huduma bora na za uhakika ikiwezekana tia kibango cha 24/7"
 
Wana jamvi wenzangu mimi ni muajiriwa ktk clinic fulani kama meneja fedha wa kituo.
Ninaomba mawazo yenu wakuu kwamba ni njia gani naweza kuitumia kuvuta wateja waje kuhitaji huduma ktk kituo chetu? Je wagonjwa ambao ni wateja wanapendelea kuhudumiwa vipi? Mawazo yenu yatanisaidia kuboresha. Natamani kufanya kwa moyo wangu wote kwa mafanikio ya ustawi wa kituo.
Naomba kuwakilisha , nishauri chochote cha kujenga.
Mjitangaze mnatoa huduma gani, mna wataalamu wa magonjwa gani n.k. Wagonjwa watawatafuta kwa mnayojinasibu nayo, na pindi wanapokuja kwa ajili ya hizo huduma, msiwaangushe.
 
Ninaomba mawazo yenu wakuu kwamba ni njia gani naweza kuitumia kuvuta wateja waje kuhitaji huduma ktk kituo chetu?
#1. Fuatilia mada za Dr. Said hapa JF [ Mada za Dr. saidi zina mgusa mjasiria mari yeyote yule anayehitaji kupata wateja wengi kwa huduma au biashara anayofanya ]

#2. Ikibidi jiunge na moja ya course anazotoa.

Hakika utajifunza mengi na mafanikio utayaona.

Kila lakheri ndugu
 
Hehe!! Nazidi kuwaza muuza majeneza anatumia mbinu gani biashara iende vizur na asomeshe watoto shule..na anamtegemea Mungu kumtunza kila siku
 
binafsi yangu kuni win lazima uwe na DR. sio ma clinical officer namanisha M.D kama hao hawapo kuja kwenye clinic yako ni big No labda niletwe nimebebwa sijitambui.
Udaktari ni uzoefu ( case ngapi daktari ka-clerk ) siyo mavyeti tu

Waulize hata hao MD wanavyoenda.wodini, wanakutana na Nursing Attendants tu wapo wodini miaka 20 wanajua kila kitu practically siyo kama wewe umemeza desa tu.

Ukijifanya mjuvi anakuachia uone kama utatoka na theory zako za kwenye PROJECTOR.
 
Kitu ambacho watu tunapo umwa tukienda hospital hatupendi ni foleni kuwa kubwa au kukaa foleni Bila sababu chengine unambiwa pita pale baada ya pale nenda pale sehemu kama nne bado hujapata huduma alafu kote foleni.. Rekebisha hayo wateja wanakuwa wengi mno
 
Sekta ya Huduma kama hiyo mara nyingi watu huambizana kuwa kituo au Doctor fulani wako vizuri sana through word of mouth
Hivyo basi the best way kupata wateja wengi ni kuwahudumia hao wachache kwa huduma iliyotukuka.

Feedback, lazimisheni kwa staff wenu mechanism ambayo itawafanya mpate feedback toka kwa wagonjwa wenu. Kumbukeni tunaishi ktk dunia ambayo customer feedback ni mtaji mkubwa mno ili muweze kubadilisha WEAKNESS zenu ziwe STRENGTH (isije ikawa nimekuacha)
Ikiwezekana una hire hata "mysterious shoppers" ambao watawapa feedback jinsi gani wateja wanahudumiwa hapo

TAT, Turn Around Time ktk huduma yoyote muda wa kupata huduma ni kitu muhimu sana, nadhani kwenye suala la Afya umuhimu wake utakuwa maradufu. Hivyo ni lazima muweke standard ya muda tangu mteja anaingia, anajiandikisha mpaka anamaliza huduma itachukua muda gani ? Jee mteja kaletwa yuko hoi anatweta kwanini asipelekwe kwanza kwa Daktari wakati kujiandikisha kunafuatia.
Na mkishaweka hiyo TAT mnahakikisha mna system ambayo inaenda sawa na muda mlioweka

Tofauti, lazima mjitofautishe na watoa huduma wengine kwa mfano wateja wengi wanajuwa nikienda Marie Stoppes wako competent kwa tiba za aina fulani, nikienda Furaha Clinics pale Morocco ni kwa ajili ya watoto. Hivyo na nyie lazima muwe na utambulisho ktk specialisation zenu ingawa hawa wa Malaria, UTI na Typhoid nao mnawahudumia

Ubunifu, wekeni utamaduni wa ubunifu katika kuwahudumia wateja. Mnaweza mkawa na digital database ya customers wenu mkawa na tarehe za kuzaliwa za wateja, ambapo mnaweza mkawa mnawawish happy birthday wateja wenu kila wakati ikifika au hata kuwatakia Sikukuu njema zifikapo nyakati za Sikukuu

Usafi wa Mandhari, Wafanyakazi, Vifaa Tiba na Kauli za Watoa huduma nazo ni muhimu sana

Ciao
 
Back
Top Bottom