Naomba ushauri wenu

Naomba ushauri wenu

Baba ako ni mbongo au mkanada?
Kama ni mbongo mjengee huku nyumbani, then umrudishe na kama unaweza mfungulie biashara na atafute mke aoe, miaka 46 ni michache sana kwa mwanaume mwenye akili timamu kutangatanga kwenye familia za watu, labda awe ni mgonjwa na hawezi kuishi bila ww karibu.
 
Huyo ni BABA YAKO MZAZI
au baba yako mlezi?

KAMA NI BABA YAKO MZAZI, BASI KATI YAKO WEWE NA UBONGO WAKO KUNA KIMOJA HAKIPO SAWA!

Sina ushauri mwingi kwa umakolo wako zaidi ya kukuambia GHARAMA ALIZOTUMIA BABAKO KUKUTUNZA NI ZAIDI YA HIVYO VIDOLA!

1. maisha ni magumu kwa sababu umelifunga lango la baraka (kwa kumuona babako kero)

2. hakuna aliye mnanga babake mzazi akabaki salama.

3. MHESHIMU BABAKO NA MAMAKO SIKU ZAKO ZIWE NYINGI DUNIANI.

4. Mrudie muumba wako kwa imani yako ili ubaki salama!

5. MTUNZE BABAKO, MAANA WAKATI ANAKUTUNZA HAKUKUAMBIA UENDE KUTAFUTA KAZI.

6. Yeye kutalakiana na mamako haikuhusu maana huwezi jua tatzo liko wapi. ACHA UJINGA MTUNZE BABAKO.
Huwezi kunielewa hata ungekuwa mtakatifu husingeweza kuishi naye hata kidogo

Kama umesoma historia vizuri toka tuko afrika alikuwa ni mtu wa wanawake tu hakujali watoto wake wanakula sisi most of our life uko afrika yalibebwa na mama yetu
Tulivyofika uku canada 2017 tukafikiri atageuka tena bado akaendelea na tabia yake ya kijinga kama 2017 alitengeneza fix kuwa ameshika mama na wanaume wengine ili tu apate sababu za kuachana na mama na moja kati ya lengo lake lilikuwa mama afukuzwe ndani ya nyumba ndo maana alienda kustaki kuomba haki ya uongo kwa bahati mbaya polisi walifanya uchunguzi wao wakagundua ni fix tu akafukuzwa yeye nyumbani japo kuwa watu wengi walimshauria pamoja mama yake kipindi bado yupo hai hakusikia mtu yeyote kitendo icho kilimpeleka mpaka marehemu bibi kupoteza maisha kwa presha kutokana na tabia ya mwanaye wa pekee
Alifanikiwa kutoka akaenda kuoa mwanamke mwingine uko waliishi na uyo mwanamke toka 2017 mpaka 2021 wakaachana na toka 2022 mpaka leo amekuwa mtu wa kuangaika angaika tu watu walijaribu kumuombea msamaha kwa mama labda anaweza kurudi home mama alikataa nina wadogo wangu ambaye yupo nyuma yangu ana nyumba naye alikataa kabisa kumpokea mimi kama first born wake niliona nichukuwe mzigo nao imeanza kunishida
 
Tuanze kwanza, mama aliyetalikiwa na baba mwaka 2017 yuko wapi kwa sasa?,kingine una uhakika huyo ndio baba yako kweli?
Mama yupo nyumbani hajaolewa baba ni mtu wa fix sana anafanyaga mambo kama hana akili sana yeye alikuwa ni mtu wa mademu mara nyimgi wanaume sisi tukiwa na michepuko yetu hatuwezi kudharau mke wa kwanza au wetu kwasababu ya mchepuko sasa ni tofauti kabisa akiwa na mchepuko anapenda kuoa kabisa na moja ya kikwazo chake alikuwa anaona ni mama alikuwa kama kipindi tupo afrika alikuwa ana mfukuza kabisa nyumbani anakuja kuishi na mwanamke mwingine ndani ya nyumba mama kama 2017 alitengeneza fix kuwa ameshika mama na mwanaume ndani ya nyumba jambo likafika mpaka kuserekali uko lakini kwa bahati mbaya polisi walifanya upelelezi wao wakagundua ni uongo tu na moja ya plan zake zilikiwa afukuze mama pale ao mwanamke mwingine kama alivyokuwa anafanya afrika
 
Kama unawatoto wanne na mke Dingi yako ana 46yrs old,tatizo ni kwamba hii story ni chai,tuambie entirely truth tukushauri mkuu
 
Nahitaji ushauri wa watu wenu ndugu zangu wenye busara.

Ninaishi Canada kwenye nyumba ya serikali (HLM) pamoja na mke wangu na watoto wangu wawili. Baba yangu ana miaka 46. Nilimchukua aishi kwangu kwa sababu alikuwa ana maisha magumu, lakini tangu ameingia kwangu maisha yamekuwa magumu sana.

Tabia zake zimekuwa changamoto kubwa:

Ni muongo kupita kiasi, hasemagi ukweli hata nikimwomba nimsaidie kupata kazi.
Ni mvivu wa kazi, hajawahi kuendelea na kazi yoyote. Wiki 3 sasa hana kazi wala kipato.
Anadanganya kuwa anaenda kazini kumbe anazurura tu mitaani.
Ni mlalamikaji, mbishi, na anakasirika haraka.
Ni mbeya na ana historia ya kuleta migogoro ndani ya familia. Kwasababu ya uongo wake
ALimkataa mama yangu 2017 tena kwa talaka cha ajabu yeye ndo anateseka zaidi na wakati aliaminisha jamii kuwa mama yangu ndo mbaya
Ana tabia ya kutumia watu, akishapata mahali pa kula na kulala, anajisahau kabisa.
Anapenda kula sana, na gharama za chakula zimepanda sana. Zamani nilikuwa natumia $200–$300 kwa mwezi, sasa tunatumia $700+.
Hatoi chochote kwenye matumizi, mimi ndiye nabeba kila kitu.

Kwenye nyumba ya serikali (HLM) siruhusiwi kuishi na mtu mwingine yeyote ambaye hajatajwa kwenye mkataba. Hii inaniweka kwenye hatari ya kufukuzwa na kupoteza makazi yangu pamoja na familia yangu.

Ukweli mwingine mgumu ni kwamba baba yangu amezoea kufukuzwa kila mahali anapokwenda kwa sababu ya tabia zake. Akiachiwa aishi kwa watu, harudi tena kwao mpaka apate shida. Baridi ikianza ndipo anarudi kuomba msaada.

Nimejaribu kila njia za kumwonya, kumueleza, kumsaidia, kumuelekeza, lakini haelewi kabisa. Kila siku ni uongo, visingizio, lawama na kuonyesha ubabe. Ukimwambia jambo analalamika au kuchukia.

Sasa nimefika mwisho nataka kumfukuza ila kuna wakati huruma unanijaa moyoni tu

Ila Nina hofu kwa watoto wangu, mke wangu, ikiwa tutapoteza nyumba yetu kwa kuvunjiwa mkataba na serekali sisi ndo tutaangaika zaidi . Lakini pia ninajua huyu ni baba yangu mzazi, na akitoka kwangu atakuwa hana pa kwenda

Swali

Nifanye nini katika hali kama hii?
Nimfukuze kwangu kwa ajili ya usalama wa familia yangu, au niendelea kumvumilia huku familia yangu ikiteseka?

Naomba ushauri wenu
Fanya kuungua umpangishie mahali halafu before umwambie hiz nyumba za serikali kuna muda wanakagua wakikukuta mtu asiye kwenye mkataba unanyang'anywa nyumba. Mtokee kwa nyuma mkuu. Kingine jitahd uishi kama biblia inavyosema
Kuwa na kiasi na kila kitu. Usimuonee yeyote huruma kupita. Nimekumbuka Ontario
 
Mpeleke akaombe nyumba yake ya serikali, na kwa umri wake ana weza kupata pesa ya kula toka serikalini.
Umri wa miaka 46 aweza kupewa pesa ya bure ya jujikimu, kwani kawa mzee kwa umri huo?
 
Huyo baba ako tabia ya kipuuzi ya kupenda sana kula hana tofauti na mimi.
 
Ikiwezekana mlete na mama yako tukae naye, usipende kurukia kujibu comment hivyo.

Badala ya kumjibu mleta mada, una kuja kukimbilia kuni ambia mimi.
Kama haikuhusu unawashwa na nini? Tuliza boli huko shamba mzee. Mambo ya Unyamwezini huyawezi!
 
Kwahiyo baba yako mmbea, halafu mvivu na anakula sana??

Umesema unamshauri pia kuhusu kujenga maisha yake?!! 😹😹😹

Diaspora mna hekaheka sana
 
Back
Top Bottom