Niko dillema, naomba mawazo yako

Niko dillema, naomba mawazo yako

R_Breazy

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2025
Posts
273
Reaction score
559
Habari za w'end wakuu

Niende moja kwa moja tu bila chenga, akili imewaza ila sijapata mwafaka.
Thread zangu za nyuma zinaweza kuwa reference ya kile nachopitia, anyway:

Wakuu nipo mjini DSM na hadi Saivi nipo mahakama fulani nijitolea, kuna kipindi nilipitia wakati mgumu hadi nikatamani kurudi kwa mzazi mwenzangu, shida tu alikuwa likizo na bahati mbaya niliondoka baada ya ugomvi mkubwa sana - Saivi karudi na anataka niende nkafanye kilimo nikiwa nasubiri pengine kibarua, mwanzo nilishindwa kukubali moja kwa moja sababu nilikuwa nasubiri passport yangu, mpaka kuja kuipata tayari nilikuwa nimeshapata mahali pa kujitolea(mahakamani) niliona sawa kupata elfu tano tano mara moja moja kuliko kubaki iddle nyumbani.

Probability ya kuja kuajiriwa ni ndogo Sababu hasa wanahitaji watu wenye diploma (Rumors nilizosikia) kazi niliyopewa ni ukarani-kwa wiki mbili tu nlizoserve itoshe kusema wanaume tuwe makini sana na wanawake hasa hawa wanawake wa ndoa 🙌

Nistoke kwenye mzizi wa thread, nafanya with no hope kwamba pengine naweza kupata gape la kuja kuajiriwa, kiuhalisia sioni kama itakuwa kama navyotamani, kumbuka yote yanajiri nipo kwa mshikaji wangu-haonyeshi kunichoka kulingana na hali yangu ananisaport sana kwa kila namna. Kuna muda hadi nasikia aibu hapa ndipo mawazo yanapoanza kwamba nikiondoka ataona nimedharau jitihada zake, lakini pia fursa dar ni nyingi; je naondoka dar then What?? changamoto nyingine ni mimi nitabaki kwake hadi lini, jibu linakuja lazima nitafute kwangu kama kidume-kwa kazi ipi? Hili ni swali jingine.

Option yangu inabaki bora nirudi kwa mzazi mwenzangu ila changamoto kama mnavyojua jinsia upande wa pili hisia zikipungua plus yeye anahudumia dharau zinaanza, ijapo tayari tumeshapangilia nini cha kufanya, bad thing TAMISEMI wamemtupa KIJIJINI haswa Njombe ndani ndani uko so pow, mwaka huu kalima heka 1 kapata gunia 13 za mahindi.
Najua wengi humu mmepitia/kuona haya mna experience za kutosha, hivyo mawazo yako ni muhimu.
Nitachukua kile ambacho kitafaa ili nifanye maamuzi sahihi zaidi kwamba "nibaki Dar au niende Njombe"
Natanguliza shukrani, karibu nipate mawazo yenu🙏🙏
 
Ushauri juu ya kipi? Be precise
Kazi umepata japo tempo, tumia connection hiyo kupata sehemu ya kudumu.
Kazi haina assurance yoyote Mkuu datz y. Ushauri ni mimi nibaki kwenye hiyo kazi ambayo haina malipo zaidi ya chakula cha mchana/hakimu hadi ajisikie siku hiyo kukupa chcht so poa. Wazo jingine nikujikita kwenye kilimo kwa mzazi mwenzangu alipo, ila kipengele ni namna jinsia ke vile hawajui kukaa na mwanaume anamlisha, kitu ilinishinda mara ya mwisho hadi kugombana nikaondoka. Hapo ndo akili yangu inastuck kufanya maamuzi sababu naona yapo 50/50 hadi kufikia kuomba mawazo zaidi hapa.
 
Nenda Njombe kamsaidie mzazi mwenzako kulima mahindi. Mwanaume kamili huwezi kulelewa na mwanaume mwenzako. Bora ukajifanye zoba kwa mzazi mwenzako, ili maisha yaendelee.
Na hiki ndo kinaniwazisha, kulelewa na mshikaji si shida ila haisound good kabisa, kulelewa na mwanamke ni kujishusha mamaee😂😂
Maisha mtegoni.
Maamuzi ya busara sana yanatakiwa mkuu
 
Nenda Njombe ukalime bwana mdogo, kwa mazingira uliyopo sasa sioni NURU mbeleni zaidi ya kujipa matumaini hewa. DAR ES SALAAM ni mji unaopumbaza sana watu na kuwapotezea muda haswa ukiwa hauna uhakika wa kipato endelevu...

Kila la kheri
 
Na hiki ndo kinaniwazisha, kulelewa na mshikaji si shida ila haisound good kabisa, kulelewa na mwanamke ni kujishusha mamaee😂😂
Maisha mtegoni.
Maamuzi ya busara sana yanatakiwa mkuu
Maamuzi ya busara na ya kiutu uzima ni haya tu ya kwenda Njombe. Sijui ni kwa nini vijana huwa mnawachukulia wanawake kama watu wabaya sana.

Wanawake ukiwajulia, hata wawe pilipili kiasi gani! bado ni rahisi sana kuishi nao.
 
She so Sweet kiasi kwamba mwenyewe sioni ugumu kwenda tatizo lipo kwenye malumbano, leo ananipigia akinieleza kuna pahali ananiombea kazi ili nisogee alipo (kuna watu watakuja kusema ataliwa na boss wako) nasubiri mrejesho wake.
In short yule ni mke wa kuoa ndugu na ikitokea nimefeli kufanya hivyo basi ni sababu zilizo nje ya uwezo wangu, we turn 8-9 years now, tulipoendana skuli tukaja kukutana kwa mara ya kwanza kimwili 2018❤️‍🩹
 
Ww ni mwanaume kuendelea kulelewa na mwanaume utakuja ujikute umeloa nyuma oooh namuamin anaweza kupitiwa yule ni binadamu nenda kijijin kafanye kazi
 
Mkuu asilimia kubwa ya hizi taasisi za serikali ukienda kujitolea bila barua rasmi ya mkataba, wataishia kukutumia tu kusafisha ma-file yao na kukimbizana na makaratasi yao ambayo wao wenyewe yamewachosha kuyafanyia kazi. Umeshasikia tetesi kabisa kwamba wanataka watu wenye Diploma, wewe huna, unategemea nini? You are literally wasting your youth energy on a dead end job kwa matumaini ya miujiza.

Serikali wakitaka kuajiri wanafuata taratibu na budget yao. Hiyo elfu tano unayoichukulia leo poa, itakufanya uwe stagnant kwa miezi mingine sita ijayo, halafu mwisho wa siku unaachwa hewani.

Huyo mshikaji wako hatokuonyesha tabia yoyote ya tofauti kwa sababu pengine ni mtu muungwana sana, lakini don't abuse his hospitality mzee. Kila mtu ana maisha yake na ana mambo yake ya siri anayotaka kufanya kwenye geto lake. Unazidi kujishusha thamani ukikaa hapo Dar bila ramani kuliko ukienda Njombe kupambana na mzazi mwenzako.

Mzazi mwenzako kavuna gunia 13 za mahindi kwenye heka moja tu! Huoni kuwa huo ni ushahidi tosha kwamba hiyo ardhi aliyopo ina baraka zake kiaina?. Huyo mwanamke ameshkutengenezea njia, wewe kama dume la familia nenda kamsaidie, kama msimu uliopita amepata gunia 13 peke yake, mkienda wawili mkaongeza nguvu na akili mkabarikiwa kuvuna gunia 50 au 100 si mtatoboa?

Huko Njombe ndiko kuna fursa yako ya haraka kwa sasa mzee, mchezo wa kilimo ukiujua vizuri unaleta hela ya haraka kuliko kuendelea kubaki bila ramani, matokeo yake unazidi kujilemaza tu.
 
Nimesoma reply zako zinaonesha unataka kurudi kwa mshangazi ukalelewe, yani wale wanaokupa ushauri unaoambatana na kurudi ndio unawaona wanakushauri vizuri bila shaka unasumbuliwa na genye na upwiru wa kummiss huyo unaemuita mzazi mwenzio

Komaa town mzee wanawake sio wa kutegemea kabisa komaa ujenge kwako komaa upate kitu cha kufanya town mishe nyingi jichanganye acha kufungwa na mawazo ya kuajiriwa na elimu ulionayo

Usirudi kwa huyo mshangazi utakuta maumivu hakuna mwanamke anaemtafutia ugali mwanaume halafu akawa mwaminifu hakunaaa
 
Sikiliza moyo wako unavyokuambia.
Moyo na fikra naona 50/50 NAWAZA sipati majibu; kwamba nikibaki, je nitabaki kwa msela hadi lini(ye tayari maisha yake yana unafuu sana)pesa ya kodi, kula na other basic needs anaweza ku afford..
Lakini pia nikisema niondoke huko niendako ni heri kiasi gani au mihemko tu ya hisia (ikumbukwe mara ya mwisho nilitoka huko kwa ugomvi) so nachosita ni kutokea tena ugomvi kama ule.
 
Nimesoma reply zako zinaonesha unataka kurudi kwa mshangazi ukalelewe, yani wale wanaokupa ushauri unaoambatana na kurudi ndio unawaona wanakushauri vizuri bila shaka unasumbuliwa na genye na upwiru wa kummiss huyo unaemuita mzazi mwenzio

Komaa town mzee wanawake sio wa kutegemea kabisa komaa ujenge kwako komaa upate kitu cha kufanya town mishe nyingi jichanganye acha kufungwa na mawazo ya kuajiriwa na elimu ulionayo

Usirudi kwa huyo mshangazi utakuta maumivu hakuna mwanamke anaemtafutia ugali mwanaume halafu akawa mwaminifu hakunaaa
Nmejibu kulingana na kile walicho changia mkuu, mimi kwangu naona 50/50 No More#
Kuhusu upwiru kwa hii dar tena buza😂😂 uswahilini 🙌🙌😁
 
She so Sweet kiasi kwamba mwenyewe sioni ugumu kwenda tatizo lipo kwenye malumbano, leo ananipigia akinieleza kuna pahali ananiombea kazi ili nisogee alipo (kuna watu watakuja kusema ataliwa na boss wako) nasubiri mrejesho wake.
In short yule ni mke wa kuoa ndugu na ikitokea nimefeli kufanya hivyo basi ni sababu zilizo nje ya uwezo wangu, we turn 8-9 years now, tulipoendana skuli tukaja kukutana kwa mara ya kwanza kimwili 2018❤️‍🩹
Tafadhali sana! Usimchukulie kama kahaba! Ukiwasikiliza hao utakesha, kikubwa ni kuziba masikio na kusonga mbele. Kwa Njombe, ukiamua kuacha u-mjini hutatamani kuajiriwa tena. Kule kilimo ndimo mwake, sema Sisi wengine tumezeeka sasa lakini huko ndiko kwa kupiga kazi. Mahindi, viazi mviringo, maharage n.k
 
Mkuu asilimia kubwa ya hizi taasisi za serikali ukienda kujitolea bila barua rasmi ya mkataba, wataishia kukutumia tu kusafisha ma-file yao na kukimbizana na makaratasi yao ambayo wao wenyewe yamewachosha kuyafanyia kazi. Umeshasikia tetesi kabisa kwamba wanataka watu wenye Diploma, wewe huna, unategemea nini? You are literally wasting your youth energy on a dead end job kwa matumaini ya miujiza.

Serikali wakitaka kuajiri wanafuata taratibu na budget yao. Hiyo elfu tano unayoichukulia leo poa, itakufanya uwe stagnant kwa miezi mingine sita ijayo, halafu mwisho wa siku unaachwa hewani.

Huyo mshikaji wako hatokuonyesha tabia yoyote ya tofauti kwa sababu pengine ni mtu muungwana sana, lakini don't abuse his hospitality mzee. Kila mtu ana maisha yake na ana mambo yake ya siri anayotaka kufanya kwenye geto lake. Unazidi kujishusha thamani ukikaa hapo Dar bila ramani kuliko ukienda Njombe kupambana na mzazi mwenzako.

Mzazi mwenzako kavuna gunia 13 za mahindi kwenye heka moja tu! Huoni kuwa huo ni ushahidi tosha kwamba hiyo ardhi aliyopo ina baraka zake kiaina?. Huyo mwanamke ameshkutengenezea njia, wewe kama dume la familia nenda kamsaidie, kama msimu uliopita amepata gunia 13 peke yake, mkienda wawili mkaongeza nguvu na akili mkabarikiwa kuvuna gunia 50 au 100 si mtatoboa?

Huko Njombe ndiko kuna fursa yako ya haraka kwa sasa mzee, mchezo wa kilimo ukiujua vizuri unaleta hela ya haraka kuliko kuendelea kubaki bila ramani, matokeo yake unazidi kujilemaza tu.
Ndivyo navyowaza au nilivyowaza ila nikawa NAWAZA kumdissapoint tena mshikaji ataniona jau kinoma.
Kwanini, nakumbuka ugomvi ulipotokea balance ilikuwa imebaki 30k tu, mwanamke alikuwa amefura kinoma sababu nilikuwa nimempiga makofi ya kutosha hivyo muda wwte polisi ningeenda kama ningeendelea kubaki pale ndo mshikaji kunitumia pesa mimi kuchomoka, kitendo cha kurudi naamini kabisa ntamdissapoint hiko ndo nakitafakari kulingana na juhudi na namna alivyojitoa kwangu till now, na hapo ndo mtego ulipo Mkuu
Zaidi Nashukuru kwa mawazo yako🙏
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom