Naomba ushauri nisome Master's ipi kati ya MBA in Marketing na MSc in Natural Resources Management?

Mshua's

JF-Expert Member
May 22, 2013
801
546
Habari zenu wakuu?

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, naomba ushauri nisome Master's ipi kati ya hizo nilizozitaja? Na kama kuna chuo kizuri unakifahamu kwa masomo hayo usisite kunishauri, faida na hasara za kusoma kozi hizo pia ningependa kuzijua. Binafsi nafirikia kwenda UDOM ambapo shahada zote mbili zinapatikana, au CBE kwa kozi ya MBA Marketing.

Nilisoma shahada ya kwanza katika fani ya Utalii (Tourism), nimeajiriwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye moja ya taasisi zake zaidi ya miaka 8 iliyopita.

Nilikuwa na mpango wa kusoma shahada ya pili katika fani ya Utalii ili nibobee kwenye fani hii lakini kwa bahati mbaya Tanzania hakuna chuo kinachotoa shahada ya Utalii isipokuwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambacho siyo chaguo langu.

Ushauri wako utaniwezesha kupata maamuzi ili niweze kufanya maombi maana muda ndiyo huu.

Natanguliza shukurani za dhati wakuu!
 
Hii heritage management ipo chuo gani mkuu? Naona inaendana na mambo ya makumbusho?
 
Wakuu habari za jioni!

Ushauri wenu niliufanyia kazi. Niliomba MBA Marketing katika vyuo vya CBE na UDOM nimepata admission kwa vyuo vyote. Hapa nina changamoto ya uchaguzi, niende chuo gani kati ya hivi vyuo nilivyochaguliwa?
 
Wakuu habari za jioni!

Ushauri wenu niliufanyia kazi. Niliomba MBA Marketing katika vyuo vya CBE na UDOM nimepata admission kwa vyuo vyote. Hapa nina changamoto ya uchaguzi, niende chuo gani kati ya hivi vyuo nilivyochaguliwa?
We nae unatusumbua...sasa mpaka hilo nalo ni la kuomba ushauri kweli?
 
Back
Top Bottom