Naomba Ushauri wa kitaaluma kuhusu uhusiano wa kitaaluma kati ya elimu ya bachelor na masters kwenye ajira

Drimatomps

Member
May 23, 2021
13
19
Mim ni kijana niliemaliza elimu ya degree/shahada miaka 7 iliyopita nilisoma bachelor of "education in economics and accounting " lakini sikuwahi kubahatika kufundisha kama mnavyoelewa nchi yetu unasoma hiki alafu kazi utafanya utakayopata

Nlibahatika kufanya kazi mbalimbali ila mwishowe nikaingia kwenye sekta ya logistics ambamo niko mwaka wa tano sasa, sasa nataka kujiendeleza niweze kuajirika kampuni kubwakubwa zaidi maana experience nimepata kubwa na hapa nilipo naona kabisa ni padogo kwangu kwa sasa,nimejaribu kufatilia kuna masters nyingi sana naweza kuzisomea nimependa moja ya udsm ( masters of science in international transport and logistics)ili niwe mbobevu zaidi ila nikapata shida baada ya kuona sehemu nyingi kuajiri huwa wanarefer sana degree yako sasa hapa najiuliza hii degree yangu na hiyo masters nikichukua nitakuwa nimecheza karata nzuri au ndo nitakuwa nimepoteza????

Naombeni Ushauri kwa wabobezi wa haya maswala please
 
Sawa ila pia kumbuka kwa sasa employment is all about networking. Jiendeleze masters ila usisahau kunetwork pia.
 
Back
Top Bottom