Naomba ushauri, naogopa kumuoa huyu mwanamke

Habari wanajamii,

Naimani wote niwazima mungu nimwema anaendelea kutupigania.

Niende moja kwa moja kwenye jambo husika. Kiukweli niko kwenye njia Panda sielewi nifanyeje. Niko kwenye mahusiano na mwanamke mmoja hivi kiukweli tunapenda sana lakini tulipo ngia kwenye mahusiano hakuna kitu nilikua najua lakini alikuja kunieleza ukweli kuwa ana mtoto mwanzo sikujua nayeye hakutaka kunificha akaamua kunieleza ukweli. Nikahitaji kujua kiundani zaid ilikuaje

Kweli alikuja kukaa na mimi na kuanza kunieleza ukweli kuwa alikuwa na mahusiano na jamaa akaja kupata ujauzito then baada ya kujifungua yule jamaa ikabidi amueleze ukweli kumbe jamaa alikuwa na mke na watoto wa2 na jamaa hakai Tz anakaa nje ya nchi na familia yake so ikabdi jamaa amueleze ukweli huyu mwanamke baada ya hapo ndo ikatoka conflict kati ya jamaa na mwanamke pamoja na wazazi wa mwanamke na kupepelekea kuachana na jamaa akaamua kuondoka kuludi nje anakokaa coz huyu mwanamke alimwambia jamaa sahau kama una mtoto na mimi.

Bas mwanamke akaanza kumlea mtoto mpaka now mwenyew na mpaka nilipokutana nae na kujikuta tumeingia kwenye mahusiano.

Kiukweli tushafanya mengi na tuna malengo mengi now nataka kumuoa kabsa lakini hofu yangu juu ya kumuoa mwanamke mwenye mtoto wa mwanaume naogopa coz changamoto huwa ni nyingi sana na je? Nawaza jamaa siku akija kurudi tena yaani sielewi mambo nimengi kiukweli.

Naomba mnishauri nduguzangu ilinijue nafanyaje kabla sijaingia kwenye matatizo hapo baadae na changamoto za kuoa single mother.

Kwenu wakuu nasubili ushauri wenu..
Kwanza hakuna cha nje ya nchi wala nini, mzazi mwenzake yupo hapa hapa bongoland na siajabu mji huo huo. Kukwambia bla bla za nje ya nchi ni kukulaghai ili ujue hawana uwezekano wa kukutana na hiyo ni dalili tosha anaficha na hayuko wazi kwa suala hilo kwakua BADO WANAWASILIANA na huenda WANAKUTANA.

Kwa kusema uongo huyo hakufai hata robo piga chini utakuja kulia machozi na unavyoonekana uko limwanaume wa Dar, baby baby nyingi afu mixa kama huyo mdada kashakuteka sana.
 
Duuh sawa mkuu nimekupata vyema sana [emoji120][emoji120]
 
Kaka hawa walipendana na ndomana wakaingia kwenye mahusiano mbaka mwanamke akapata ujauzito shida ilikuja baada ya jamaa kuamua kutoboa siri aliokuwa akimficha mwanamke kuwa kumbe ana make an familia huko Njee ya nchi apoishi ndo conflict ilipotokea na kupelekea kuachana kila mtu kuendelea na maisha yake
Fungua macho we dogo, HAKUNA CHA NJE YA NCHI WALA NINI, HUYO MWANAUME YUPO HAPA HAPA BONGOLAND na wanawasiliana na mwanamke hataki uwe na wasiwasi ndo kukudanganya yuko nje ya nchi bla bla WTF.
 
Mimi ni mwanamke lakini siamini kama kuna kuachana kati ya mtu na mzazi mwenzake(sijaandika kwa ubaya)
Huwa tunaongozwa zaidi na hisia japo wapo wenye misimamo

Wewe fanya unachoweza,kama ataamua kuwa muaminifu sawa...ikiwa ni kinyume chake pole in advance
I think i want to go out with u.....
 
Ni bora ukosee kujenga kuliko kuoa, fanya ibada zaidi utajua anafaa au hafai
 
Okay mkuu but still walikuwa bado sio mke na mume wa ndoa
We jamaa unauboya flani ni ngumu sana kukushauri. Kwani ndoa ni nini ?! Makaratasi na pete ? NDOA NI MAKUBALIAOO YA ME NA KE, SASA WAMEKUBALIANA WAMEKULANA WEEEE MPAKA WAMEPATA MTOTO afu unasema hawakua mke na mume, mkuu sina cha kukushauri una kichwa ngumu na KWA HAKIKA UTAVUNA UNACHOSTAHILI
 
Akirudi utamuazima jamaa kwa muda hakiishagi
 
Ukweli ni ukwelii mwanamke akishazaa tayari anakua mnemboni yani mda wowote baba mtoto akirudii penzi linarudi[emoji23][emoji23] kuna mwingine alimchukulia mkopo baba mtoto wake kwa madai ya kwamba afungue biashara aanze kumsapoti mtoto wake wakati alimkimbia kipindi cha mimba. Hizi shuhuda za masingle maza zipo nyingi sana unaeza sema wamewekea madawa na wanaume waliozaa nao na kibaya ndo ukute aliezaa nae alimwacha akaoa mwanamke mwingine hapo baba mtoto akirudi kulia lia atamrudia ili amkomeshe mkewe kumbe anajiharibia[emoji16][emoji16] wanawake mda ungine tunazinguaga sana[emoji119]
Umeongea ukweli mwingi mpaka nimevutiwa na wewe (sio kimahaba)
 
Habari wanajamii,

Naimani wote niwazima mungu nimwema anaendelea kutupigania.

Niende moja kwa moja kwenye jambo husika. Kiukweli niko kwenye njia Panda sielewi nifanyeje. Niko kwenye mahusiano na mwanamke mmoja hivi kiukweli tunapenda sana lakini tulipo ngia kwenye mahusiano hakuna kitu nilikua najua lakini alikuja kunieleza ukweli kuwa ana mtoto mwanzo sikujua nayeye hakutaka kunificha akaamua kunieleza ukweli. Nikahitaji kujua kiundani zaid ilikuaje

Kweli alikuja kukaa na mimi na kuanza kunieleza ukweli kuwa alikuwa na mahusiano na jamaa akaja kupata ujauzito then baada ya kujifungua yule jamaa ikabidi amueleze ukweli kumbe jamaa alikuwa na mke na watoto wa2 na jamaa hakai Tz anakaa nje ya nchi na familia yake so ikabdi jamaa amueleze ukweli huyu mwanamke baada ya hapo ndo ikatoka conflict kati ya jamaa na mwanamke pamoja na wazazi wa mwanamke na kupepelekea kuachana na jamaa akaamua kuondoka kuludi nje anakokaa coz huyu mwanamke alimwambia jamaa sahau kama una mtoto na mimi.

Bas mwanamke akaanza kumlea mtoto mpaka now mwenyew na mpaka nilipokutana nae na kujikuta tumeingia kwenye mahusiano.

Kiukweli tushafanya mengi na tuna malengo mengi now nataka kumuoa kabsa lakini hofu yangu juu ya kumuoa mwanamke mwenye mtoto wa mwanaume naogopa coz changamoto huwa ni nyingi sana na je? Nawaza jamaa siku akija kurudi tena yaani sielewi mambo nimengi kiukweli.

Naomba mnishauri nduguzangu ilinijue nafanyaje kabla sijaingia kwenye matatizo hapo baadae na changamoto za kuoa single mother.

Kwenu wakuu nasubili ushauri wenu..
ukipenda boga, penda na ua lake mkuu!!
 
Usioe ni haramu sio kwa sababu za kidini ni kwa mtazamo wangu ni hatar sana huko mbeleni .Narudia mwanamke aliyezaa nje hatakiwa kuolewa labda jamaa yake awe amefariki

Huyo demu jamaa yake siku akimtaka anakuwa kama mbwa kaona chatu atamfuat mwenyewe .kingine kashakuzidi hapo kete ana mtoto wa kumpa jeruri
Atakushukuru baadae!
 
Kila mtu ana hoja nzuri humu ndani. Naomba niulize swali. Je ingekua ni Binti kakutana na mjamaa mwenye mtoto na mwanamke mwingine mngeshaurije?

Yuko manzi wanapendana sana na mwanaume Huyo. Tena manzi mbichi (nadhani mnaelewa ), roho nzuri mcha Mungu ana upendo sana. Mjamaa na manzi walikuwa marafiki long time ila mjamaa aliogopaga kumfungukia. Sasa mwaka jana jamaa kavaa ujasiri akamtell manzi maukweli.

Sasa wako kwenye michakato ya ndoa. Enzi zake jamaa katika pita za hapa na pale alizaa na mwanamke sema familia ya mwanamke ikamkataa kisa masikini.

Je huyu dada aolewe? Huyu jamaa anaweza kukata mawasiliano na huyu wa mwanzo??kweli wanaye mtoto je hawatarudiana?? Mnamshaurije huyu dada??
 
Labda hujaelewa, mwanamke akizaa na mtu ni ngumu sana kuvunja bond. Mwanaume anaweza akawa na watoto na bado akawalea na mama mwingine.

Iyo ni nature ni biology hatuwezi kuibadili, ukioa single maza jiandae kulia au kufa.
 
Aisee sitosema chochote nina rafiki zangu humu Jf ni singo maza sipendi kuwakwaza.
 
Fungua macho we dogo, HAKUNA CHA NJE YA NCHI WALA NINI, HUYO MWANAUME YUPO HAPA HAPA BONGOLAND na wanawasiliana na mwanamke hataki uwe na wasiwasi ndo kukudanganya yuko nje ya nchi bla bla WTF.
Duuh Kimbe[emoji17][emoji17][emoji17]
 
Back
Top Bottom