Naomba ushauri kwa hili wana MMU

Naomba ushauri kwa hili wana MMU

ha haaaa, umenikumbusha kitu hapa rafiki, lol!
hawa watu ni wa kuishi nao kwa akili sana yaani

Kwani haujui nao wanajua kuishi kwa akili pia wakitaka? Unadhani unambembeleza na yeye hajui unamfanyisha makazi mwanao unadhani yeye mjinga kisha unabembeleza akae na wewe.

Sasa jua weye ndio haujamkamata huyo bali yeye kakukamata weye, na mwanao atakuja kukuuliza y mikazi na ulikuwa unalipa watu unaowaabudu kama vile sijui nini.
 
ha haaaa, umenikumbusha kitu hapa rafiki, lol!
hawa watu ni wa kuishi nao kwa akili sana yaani

kitu ambacho sikivumilii kwa hawa watu ni kuninunia, aisee hapo tutashindwana kabisaaa, sikai na mke mwenzangu ndani, ndio mana huyu alivyoninunia na kuniamkia na kisirani cha kuondoka sikumchelewesha kabisaaaa!
 
Yaani hawa ma housegirl wa siku hizi mnawadekeza hadi basi.....fukuza huyo housegirl first
ha haaa, ni kweli tunawadekeza sana......
si unajua tena maswala ya usawa ndani?
ngoja siku anitume mie, lol!
 
Loh! umenichekeshaje? ukanikumbusha na mie visa vyangu, hawa wasichana basi!!!

sasa huyo wa kukaa nje magetini nakupiga soga alikuwa pia anavaa nguo zangu, mie nikivua nguo leo kesho nakuta haijafuliwa nikiuliza mbona nguo haifuliwa naambiwa kazi zilikuwa zimenibana nikaona nifue kesho, kumbe nikivua leo, kesho yake anaiuzia sura magetini kesho kutwa ndio inafuliwa:shock: kuna siku nae nikamzukia mchana, nikakuta kapiga kitenge changu cha church nilichokivua jana yake.
 
kitu ambacho sikivumilii kwa hawa watu ni kuninunia, aisee hapo tutashindwana kabisaaa, sikai na mke mwenzangu ndani, ndio mana huyu alivyoninunia na kuniamkia na kisirani cha kuondoka sikumchelewesha kabisaaaa!
wangu hajaaga....... na wala hasemei kuhusu kurudi home kwao....
Muda wote anakuwa peke yake na anafanya kazi zote mwenyewe..... ila sasa mwenzie karudi ndo anajifanya kazi zimemzidi wakati hakuna kilichoongezeka
 
sasa huyo wa kukaa nje magetini nakupiga soga alikuwa pia anavaa nguo zangu, mie nikivua nguo leo kesho nakuta haijafuliwa nikiuliza mbona nguo haifuliwa naambiwa kazi zilikuwa zimenibana nikaona nifue kesho, kumbe nikivua leo, kesho yake anaiuzia sura magetini kesho kutwa ndio inafuliwa:shock: kuna siku nae nikamzukia mchana, nikakuta kapiga kitenge changu cha church nilichokivua jana yake.
Du! na kuvaa nguo zangu tena!
nikimkamata ndo siku atarudi kwao
 
sasa huyo wa kukaa nje magetini nakupiga soga alikuwa pia anavaa nguo zangu, mie nikivua nguo leo kesho nakuta haijafuliwa nikiuliza mbona nguo haifuliwa naambiwa kazi zilikuwa zimenibana nikaona nifue kesho, kumbe nikivua leo, kesho yake anaiuzia sura magetini kesho kutwa ndio inafuliwa:shock: kuna siku nae nikamzukia mchana, nikakuta kapiga kitenge changu cha church nilichokivua jana yake.

Hahahaah!! sikupatii picha ilikuwaje? na ka muda kangu kachache mie nimeamua nijifuliage tuu nguo zangu na za

hubby maana unaweza pata murder case bure!!!, niliwahi kukaa na binti wa Mtwara mbona nilikoma! chochote

kinachofanyika ndani kiwe kizuri au kibaya lazima kifike kwa majirani,sebulani kukawa jumba la sinema,mie

nikipita zangu kuelekea job watu wananing'ong'a tu wanajua a-z yangu, vitu vya ndani wanapewa majiran ukiuliza

mara kimevunjika,mara kimepotea, nilikuwa nalisha familia tatu bila kujua mchele unaweka ndani hata mwezi

haufiki,nilivyokuja kugundua kesho yake fasta nikarudisha kwao, sasahivi niko na wa Kigoma namshukuru Mungu siyo

mbaya sana yanavumilika.
 
Nawasalimu kwa Upendo wanaMMU.
Kuna hili jambo naomba unishauri maana sina uhakika na ninayoyafanya niyafanye vipi.
Nina binti ambaye yupo sekondari, boarding school.
Wadada wa kazi ambao nimeshakaa nao mpaka sasa wote ni wana umri mkubwa kwa binti yangu.
Huyu binti yangu ukweli tangu akiwa primary school huwa napenda sana anapokuwa home asaidie kazi za nyumbani kama ambavyo wadada wanafanya. na imetokea kawa mfanya kazi mzuri sana, kuanzia kupika, kufanya usafi na kazi zote za nyumbani.
Tatizo sasa linakuja, dada wa kazi niliyenaye sasa anataka kazi zooteee za nyumbani wafanye sawa na binti yangu. binti yupo nyumbani kwa likizo ya wiki 2, lakini ukweli hapati hata muda wa kupumzika au kufanya kazi zake za shule maana muda wote anafanya kazi za nyumbani.
Ni kweli napenda binti asaidie kazi za nyumbani, lakini kama leo nimejisikia vibaya sana sababu binti hapati muda wa kupumzika kama watoto wengine wa nyumba nyingine, dada wa kazi anataka kila kazi wafanye wote. Na mimi naona haipendezi kumwambia binti yangu apumzike wakati dada wa kazi anafanya kazi, hata kama ni kuosha vyombo.
Nimekuja hapa kuuliza wenzangu mnisaidie, nipangaje kazi ili dada ajue kuwa kazi za nyumbani ni wajibu wake yeye na siyo binti ambaye yupo hapa kwa muda tu?
Au wenzangu mnafanyaje?
NB: najua kuna wengine pia wanaishi na ndugu, wadogo zenu, mawifi, ambao ni wanafunzi, hao pia nawaweka kwenye kundi kama hili tu la binti. Mnapangaje hapo?
Natanguliza shukurani

kinachokusumbua hapo mkuu ni ratiba, na watu hawajui majukumu yao; Binti anajukumu la KUSOMA, hakikisha anasoma kwa ratiba sahihi, na ukiweza kupata muda wa "kusoma naye" soma naye kwa maana ya maongezi ya kirafiki amesoma nini mnafanya kama mnapiga stori kirafiki kuhusu nini amesoma na malengo yake siku inayofuata, hiyo itamkeep busy kwa kujua ana wajibu unamsubiri kama mwanafunzi. Kama ratiba iko wazi hata ddada wa kazi atajua kabisa kuwa kazi yoyote inayotokea katika muda huu inamhusu, hatakuwa na mtu wa kumtegea, kwa sababu atajua mwenzake naye yuko kwenye majukumu. TUWAPE WATOTO MUDA WA KUSOMA, NA TUHAKIKISHE WANASOMA HUO MUDA WA KUSOMA.
 
ni kweli hiyo ndo weakness yangu, kuwapangia ratiba......
nitajitahidi nifanye hivyo ili dada ajue anapaswa kufanya nini na wakati gani...... binti pia.
Shukrani
 
kazi alikuwa anafanya mwenyewe zote, na muda wa kulala mchana anaupata. ila sasa anataka kuajiri naye ili apumzike. Leo ndo kagoma kufanya lolote, tumefanya kazi zote na mwanangu...

Nilihisi tu kuna tatizo, na mmefanya kazi zote na haujamhoji kitu?!!!....ongea naye ujue tatizo, wakati mwingine kuwa strict inasaidia sana.
 
Nilihisi tu kuna tatizo, na mmefanya kazi zote na haujamhoji kitu?!!!....ongea naye ujue tatizo, wakati mwingine kuwa strict inasaidia sana.
kakasirika sababu juzi nimemnyang'anya simu na jana nimemnyang'anya karata ambazo vyote vyangu.....
alikuwa muda wote anakaa na simu na pia kucheza karata wakati bado anakazi za kufanya.....
na mimi sijamsemesha, ameona kazi zinaenda, jioni hii sasa anaanza kufanya kazi na kujiongelesha
 
Huyo housegirl amewapata
katupata si muchezo......
ila kwa leo nilitaka kumwonyesha hata yeye asipokuwepo ajue hatutalala na njaa. unajua tatizo hawa watu wanadhani hatuwezi ishi bila wao
 
Msaidizi wako anatakiwa kujua wajibu na majukumu yake,
Ikitokea akasaidiwa ni vizuri lakini sio kubishana na Mama mwenye nyumba
 
nimeipenda hii ratiba......
wangu yupo boarding, kwa hiyo likizo ndo anakuwa home, haendi shule.
basi kama hvyo mpangie kazi zake awe anazifanya na kupata muda wa kupumzka na kujisomea. Labda, usafi wa baadhi ya sehemu za ndan, either sebulen na koridoni, then hadi vyombo vya jioni au kupika mboga jioni au viwe vina-rotate kupka na vyombo.
Haitamchosha mwanafunzi na pia dada ataona anasaudiwa
 
Hahahaah!! sikupatii picha ilikuwaje? na ka muda kangu kachache mie nimeamua nijifuliage tuu nguo zangu na za

hubby maana unaweza pata murder case bure!!!, niliwahi kukaa na binti wa Mtwara mbona nilikoma! chochote

kinachofanyika ndani kiwe kizuri au kibaya lazima kifike kwa majirani,sebulani kukawa jumba la sinema,mie

nikipita zangu kuelekea job watu wananing'ong'a tu wanajua a-z yangu, vitu vya ndani wanapewa majiran ukiuliza

mara kimevunjika,mara kimepotea, nilikuwa nalisha familia tatu bila kujua mchele unaweka ndani hata mwezi

haufiki,nilivyokuja kugundua kesho yake fasta nikarudisha kwao, sasahivi niko na wa Kigoma namshukuru Mungu siyo

mbaya sana yanavumilika.
unajua nashindwaga kuelewa kwa nini kuna wamama wanakuwa na urafiki na wadada wa kazi wa nyumba za jirani na wakati maboss wao hawajawazoea
 
Back
Top Bottom