Naomba ushauri kwa hili wana MMU

Naomba ushauri kwa hili wana MMU

Fixed Point

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2009
Posts
11,304
Reaction score
12,753
Nawasalimu kwa Upendo wanaMMU.

Kuna hili jambo naomba unishauri maana sina uhakika na ninayoyafanya niyafanye vipi.
Nina binti ambaye yupo sekondari, boarding school.
Wadada wa kazi ambao nimeshakaa nao mpaka sasa wote ni wana umri mkubwa kwa binti yangu.
Huyu binti yangu ukweli tangu akiwa primary school huwa napenda sana anapokuwa home asaidie kazi za nyumbani kama ambavyo wadada wanafanya. na imetokea kawa mfanya kazi mzuri sana, kuanzia kupika, kufanya usafi na kazi zote za nyumbani.
Tatizo sasa linakuja, dada wa kazi niliyenaye sasa anataka kazi zooteee za nyumbani wafanye sawa na binti yangu. binti yupo nyumbani kwa likizo ya wiki 2, lakini ukweli hapati hata muda wa kupumzika au kufanya kazi zake za shule maana muda wote anafanya kazi za nyumbani.
Ni kweli napenda binti asaidie kazi za nyumbani, lakini kama leo nimejisikia vibaya sana sababu binti hapati muda wa kupumzika kama watoto wengine wa nyumba nyingine, dada wa kazi anataka kila kazi wafanye wote. Na mimi naona haipendezi kumwambia binti yangu apumzike wakati dada wa kazi anafanya kazi, hata kama ni kuosha vyombo.
Nimekuja hapa kuuliza wenzangu mnisaidie, nipangaje kazi ili dada ajue kuwa kazi za nyumbani ni wajibu wake yeye na siyo binti ambaye yupo hapa kwa muda tu?

Au wenzangu mnafanyaje?
NB: najua kuna wengine pia wanaishi na ndugu, wadogo zenu, mawifi, ambao ni wanafunzi, hao pia nawaweka kwenye kundi kama hili tu la binti. Mnapangaje hapo?
Natanguliza shukurani
 
ni wewe kumpa binti yako kazi za kufanya kama kuosha vyombo na kufanya usafi chumba chalke na kufua nguo zake mda unaobakia apate mda wa kusoma na kufanya mabo mengine.... ila mimi sijawa mama bado naeza kuwa nakosea pia
 
tatizo binti ni mwepesi sana kufanya kazi kuliko dada.
yaani ukituma tu, kama hujataja jina ujue mfanyaji pale atakuwa binti.
Asante kwa ushauri
 
Mpangie binti kazi nyepesi tu na na zinazobaki dada ajue ni jukumu lake.
tatizo langu pia naona kama dada ataona ana kazi nyingi. Ingawa sina mtoto mdogo wala mfugo, ni kazi za usafi wa nyumba na kupika tu
 
mpangie binti yako muda wa kufanya kazi za shule mfano baada ya chakula cha jioni au mchana na umwambie dada wa kazi kuwa wakati huo ni wa binti yako kujisomea!so kama kuna kazi za ziada dada achukue jukumu la kuzifanya wakati huo!
 
Kaache ka shosti kapumzike jamani my dada wee.

Huyo mdada wa kazi hawezi kuita shots wakati yupo kazini.

Assuming ka shosti hakakuja likizo nani angemsaidia?

Be stern on this and let her know her position.
 
tatizo binti ni mwepesi sana kufanya kazi kuliko dada.
Yaani ukituma tu, kama hujataja jina ujue mfanyaji pale atakuwa binti.
Asante kwa ushauri

lazima uwe na limitation kam hivyo unataja jina fulani fanya hiki... Na binti nae apate mda wa kupumzika
 
mpe work permit binti yako.

specify ni aina gani za kazi anatakiwa afanye!
 
mwite huyo dada na mwanao kaa na kuongea nao kiurafiki zaidi.Mwambie binti yako unatarajia makubwa zaidi kwake kielimu kuliko mambo mengne ha hivyo ungependa muda mwingi autumie katika elimu yake.
Dada wa kazi nae mwambie unatarajia mambo makubwa kutoka kwake hasa katika shughuli za hapo nyumbani,hivyo muda mwingi ungependa autumie katika majukumu yake kama dada wa kazi.
Usafi wa chumba cha mwanao na mavazi yake ni jukumu lake na apatapo muda si vibaya akisaidia kazi ndogondogo afanyazo dada.
Nina uhakika baada ya kuongea nao na wao kuwapa nafasi ya kuongea hakuna kitakachoharibika.
 
Nashukuru kwa ushauri nitaongea nao.
binti anafanya kazi zake zote mwenyewe, na anapenda sana kupika kwa hiyo anajikuta kila msosi anapika yeye. tatizo ssa dada anataka binti aoshe na vyombo, adeki nyumba, afue nguo za watoto n.k. kazi ambazo dada ndo tumemwajili azifanye
 
Ili mambo yaweze kwenda vizuri lazima kuwepo na mgawanyo wa kazi..!

Hata kama binti yako yuko sharp zaidi ya huyo dada wa kazi, lazima wote waelewe majukumu yao na wawajibike kutokana na hayo majukumu..!

Dada wa kazi lazima aelewe yuko hapo kwako kwa sababu gani!
 
Kaache ka shosti kapumzike jamani my dada wee.

Huyo mdada wa kazi hawezi kuita shots wakati yupo kazini.

Assuming ka shosti hakakuja likizo nani angemsaidia?

Be stern on this and let her know her position.
ha haaa, kashost nako kanatakiwa kufanya kazi.
tatizo nadhani sijajua cha kufanya ili yeye aone hapaswi kufanya kila kazi wakati dada ndo kaajiliwa kwa kazi hizo.
 
Ili mambo yaweze kwenda vizuri lazima kuwepo na mgawanyo wa kazi..!

Hata kama binti yako yuko sharp zaidi ya huyo dada wa kazi, lazima wote waelewe majukumu yao na wawajibike kutokana na hayo majukumu..!

Dada wa kazi lazima aelewe yuko hapo kwako kwa sababu gani!
Asante rafiki, itabidi nigawe majukumu. na pia nadhani inabidi niongee na dada kuwa huyo binti anamsaidia tu, asione kuwa ndo mfanyakazi wake
 
Back
Top Bottom