Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
- Thread starter
- #61
wadogo wana kazi zao, sheshe ni hawa mabinti....Mie nimewagawanyisha kazi, kijana bado mdogo. Nimempangia kazi ya kuandaa meza wakati wa kula, kutoa vyombo tukimaiza kula, kusuuza vyombo wengine wakiosha. Kazi za kutumwa tumwa nyiingi zote ni zake, sijui kupika chai jioni, leta maji ya kunywa, tafuta rimoti, funga mapazia jioni.
Dada kupika, usafi na kufua.
Wa boarding wakija sababu wao wakubwa, nampunguzia dada baadhi ya kazi zinakuwa zao. Ukizubaa, dada anakuwa bosi wa watoto wako. Mie kuna siku alinishangaza, nilimtumanaye akamtuma kijana wangu, kidogo nimlambue.
binti wa kazi sasa anataka kuona ana msaidizi ambaye anafanya kazi zake zote, lol!