Naomba ushauri kuhusu kutoa sadaka

Naombeni ushauri walimwengu

  • Argue or react

    Votes: 3 75.0%
  • Choose whatever

    Votes: 1 25.0%

  • Total voters
    4
Huku hamna mpaka mjini kiongozi.
badi ni vyema ukaangalia namna ya kuwapa watu wenye uhitaji kama wazee wasio na msaada, na hata wajane ,...kuna watu wanahitaji msaada mkuu,...huku kwenye nyumba za ibada ni kuchezea pesa kinafiki huku tukishindwa kusaidia watu wenye kutuhitaji kweli,...
 
Hivi ni kwanini Jesus alipokuwa akitenda alikataza watu & wanafunzi wasimwambie yeyote?
Kwa sababu hakutaka apate thawabu kwa wanadamu

Ukilazimika kuonekana huna budi kuonekana

Kinacho jalisha siyo watu wamekuona au la .

Kinacho jalisha unafanya mambo ukiwa na nia gani moyoni ili watu wakuone au la

Kama wewe tayali ufahamu wako unaonesha hahusaidii kwa kutaka sifa kutoka kwa wanadamu.

Kwa hiyo zingatia hayo nilivyosema ata ukitoa wakikuona utapata thawabu kwa Mungu

Kwa sababu huwafanyii wao bali Mungu.
 
Dogo laki saba tu inakuzuzua,ungekuwa na mabillion kama ya Chivayo si ungezimia kila dakika.

Huko kijijini hakuna walemavu,masikini kapuku mafukara.Mbona unataka tukuone hamnazo.Hao ndio wahitaji mungu yupo ndani yako sio msikitini wala kanisani acha upumbavu, amka kutoka kwenye huo usingizi mzito.
 
Kaongee na mchungaji wako kuhusu aina ya utoaji unaohitaji bila kufahamika na waumini wengine. Unaweza kufanya kupitia akaunti ya benki ya dhehebu lako ama kufanya muamala kwa njia ya simu.

Asilimia kumi (10%) ya 700K ni 70K kwa hiyo ni kiasi ambacho ni cha kawaida kabisa cha muamala kinachofanyika katika mitandao mbalimbali ya simu. Hao waumini wengine watakuwa hoehoe sana kubabaika na 70k yako tena inayotolewa kila mwezi mara moja.

Piga kazi na kuzidi kumtolea Mola wako kwa imani na kwa bidii ili watenda kazi mahali pa ibada wapate mahitaji yao ya kila siku kupitia sadaka zako.

Kama vipi nenda kwenye madhabau ya Mwamposa ukajilipue kwa chote ulichokuwa nacho ili baadaye uje ujutie anguko kuu la biashara. Kwa maana utabidi utoe,
1. 50K - 10K kwa ajili ya kuitembeza injili
2. Ulipe malimbuko
3. Sadaka ya kila ibada ya misa.
4. Zaka
5. Malipo ya kumuona mtumishi kwa maombi maalum ya upako maalum
6. Sadaka ya kujilipua ili kuziangusha ngome za Shetani
7. Sadaka kwa wenye mahitaji binafsi ya kifamilia
8. Sadaka maalum ya mtumishi
 
Sahihi labda kusomesha yatima
 
Kua mpole basi 😁
 
huwezi toa fungu la kumi kwenye kanisa la kilokole usifahamike tena kwa style ya kutoa vitu vinavyoonekana, utahubiriwa kama mfano na pastor
 
Kua mpole basi 😁
Lugha yangu huwa ni hii kila ninapojadili mambo VITAL katika mustakabali wa FUTURE YA KIJANA MPAMBANAJI.

MUDA NI MCHACHE SANA, KUANZA KUWEKA NAKSHINAKSHI KWENYE UJUMBE WENYE MAUMIVU KWA VIJANA ROJOROJO.

JUMBE ZANGU HUWA ZINAPASUA BONGO NA MACHO BILA KUJALI HISIA ZAKO ZITAJERUHIWA KIASI GANI, BALI NAJALI MANTIKI NA UHALISIA!

UKIONA MAUDHUI YANGU YANAKUIRRITATE UJUE BADO HUJAAMUA KUBADILIKA.NA UPO HAPA KUTAKA SUPPORT YA KUJUSTIFY APPROVAL UNAYOITAFUTA KWA STRANGERS HAPO KIJIJINI KWENU.
 
Asante sana, mwanazengo naona kuna mengi ya kujifunza kwako
 
huwezi toa fungu la kumi kwenye kanisa la kilokole usifahamike tena kwa style ya kutoa vitu vinavyoonekana, utahubiriwa kama mfano na pastor
Sahihi kabisa, kuna la kujifunza hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…