Naomba ushauri kudhurumiwa kiwanja

Mkuu umesema sahihi kabisa. Mimi huku ninahangaika na kesi iliyoamliwa kipumbavu na Mwenyekiti wa baraza la ardhi wilaya, eti ametoa mapendekezo hati yangu ifutwe. Nimeipeleka mahakama kuu, nina uhakika wa kushinda maana yule aliyeuziwa hicho kiwanja hana vielelezo vyovyote vinavyothibitisha kwamba aliyemwuzia ni mmilki halali wa kiwanja hicho. Na kosa kubwa kununua kiwanja kwa kusainishana na serikali ya mtaa tu bila kuwahusisha watu wa ardhi wala mwanasheria. Kwa kweli ndiyo maana watu wanafikia hatua ya kumiminia watu risasi! Niliomba sana Mungu anisaidie nisijekuwa na hasira na mwenyekiti wa baraza na wazee wake wa baraza, ningewaua!!
 
Huna kiwanja na hujawahi nunua kiwanja,skwata areas unaendaje kuhakiki wizarani
Kwani huyu mshikaji amesema amenunua kwenye squatter area? Huyu si anasema eneo lina ramani kabisa? Squatter area gani inakuwa na ramani?
 
Kwani huyu mshikaji amesema amenunua kwenye squatter area? Huyu si anasema eneo li a ramani kabisa? Squatter area gani inakuwa na ramani?
Ukisoma maelezo yake kwa kina ni squarter na ndio kuna huo ujinga wa kuuziana njia,surveyed areas kuna hati ya wizara kama kitabu fulani ndani yake kuna ramani na coordinates za kiwanja husika
 
Not necessarily eneo liwe surveyed, 90% ya maeneo TZ are not surveyed, does that mean people should not buy land Not at all. Katika unsurveyed areas hakikisha majirani wote wanaopalana na kiwanja hicho wameshujudia mipaka, njia na lolote unaloona Lina maslahi kaktika kiwanja hicho. Washirikishe viongozi wa mtaa wako , wao wanajua Hali halisi ya ardhi katika maeneo yao.
Kwa hili ambalo huna njia ya kutokea, Ni kuongea kiungwana na aliyeziba njia akupe njia hata kwa kumlipa otherwise utakiacha kiwanja maana huna pa kupitia kufikia kiwanja chako. Kuna case law inayosema Kama huna njia si jukumu la jirani kukupa njia.
 
Huko kinyerezi si ndo walikomuuwa mwalimu kisa kiwanja?

Umeshanunua, umeingizwa mkenge yote sawa, angalia namna utakavyouziwa njia ya kufika kwako.

Kama haiwezekani kupata njia amua upauze, hapo ujue utapata hasara kidogo kwani pesa yako haiwezi kurudi yote.

Then tafuta eneo lingine nunua.

Makosa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku,

Jitahidi usiingie hasara zaidi.
 
umemshauri vema kabisa! Hawezi kumalazimisha jiraji ampe njia, ni kuelewana naye au auze.....
 
Jaribu kwanza kuongea na huyo aliyeziba njia kwa kumlipa sehemu hiyo ya njia. Ikishindikana jaribu kutafuta tu njia ya kupita watu kwa miguu kuinigia hapo kwako halafu unajenga nyumba ya kupangisha au unakiuza kwa bei rahisi kufidia hasara.

Lakini huyo aliyekuuzia kwa kuwa alikuwa anajua anafanya nini mburuze polisi kisha mahakamani yeye na hao wenzake wa serikali za mitaa kwa sababu ya kukupa ramani feki. Na hao wenye ramani feki wanatafutwa sana na serikali kwani ndio wanaleta migogoro ya ardhi kiasi wizara ya ardhi na seriakli kwa ujumla inalaumiwa. Nina hakika wakifika polisi/mahakamani wataeleza vizuri hiyo ramani feki waliitolea wapi ili upatikane mtandao wote.
 
Haiwezi kula kwake itakula kea aliye uza atalazimika kumpa njia bureeee Wala asitishee TARATIBU zipo huwahaiwezekani kupima eneo la MAKAZI kukakosekana njia
 
Haiwezi kula kwake itakula kea aliye uza atalazimika kumpa njia bureeee Wala asitishee TARATIBU zipo huwahaiwezekani kupima eneo la MAKAZI kukakosekana njia
Ila mkuu hujaelewa nilichokuwa namaanisha! Fikria huyu mwamba kununua kiwanja kwa kutumia ramani aliyooneshwa na mwuzaji, sasa kama mwuzaji alijitengenezea ramani fake ikapishana na ile ya mipango miji atakuwa na haki gani hapo? Mimi nimemshauri aende mipango miji waje walianganishe huo mchoro na hicho kiwanja kuona hiyo njia imekaaje! Tusipende kuamini hizi ramani za wauzaji nyingi wanajitengenezea! Unaweza kuuziwa hata open space!
 
Sawa mkuu nimekuelewa
 
naomba kujua hili likoje mkuu maana kesho naenda kwenye ofisi za hawa jamaa kwa ajili ya kuwapelekea shauri langu
Haiwezi kula kwake itakula kea aliye uza atalazimika kumpa njia bureeee Wala asitishee TARATIBU zipo huwahaiwezekani kupima eneo la MAKAZI kukakosekana njia
 
Nenda wilayani ofisi ya ardhi ili upate ramani ya eneo husika. Hakikisha unapewa the most current one, kwa sababu kuna kubadilishwa kwa michoro kila uchao na hawa jamaa ukiwapa pesa tu wanafanya "amendment".

Katika michoro yote halali ya makazi rasmi, kila kiwanja (plot) lazima kiwe na barabara angalau upande mmoja. Ukiona ramani ya mipango miji ina plot ambayo haina barabara hata upande mmoja, nenda wizarani uka-dispute uhalali wake, na uweledi wa town planner. They will settle with you.

Nakusisitizia tena, kama una registered plot number bila njia hata upande mmoja, basi hiyo plan siyo halali kwa makazi, na hakuna namna eti zijengwe nyumba kukuzunguka wewe bila kuwa na njia.

Pia, nahisi kuna njia kenye ramani ila wewe unajichagulia njia unayoitaka wewe. Hii nishawahi kukutana nayo na ni mtu mkubwa serikalini nikamtolea nje kisa anataka nichangie kwenye njia. Nikaombwa na planner wa halmashauri nikatoa nje nikaomba permit ya fence, nikaipata kwa mbinde nikaweka ua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…