hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,539
Mkuu Sangarara, inaonekana kuna shida nyingi, na unashindwa kuzieleza...labda kutokana na hasira (kama ambavyo umesema mwishoni mwa uzi wako)..Tulia, andika kitu kinachoeleweka (focused) maana unasema picha, matumizi, na kulinganisha na uzi haviendani mkuu.
Sangarara leo nlikuwa nasoma kama guest tu ila umenifanya nilog in.
Eeee hilo dege ulilolivaa ni balaa.
Hapo huna mke.
Maneno mengi sina peleka kwa wazazi tena andika vizuri sana kwenye karatasi point zake toa photocopy au maandishi yaprint andika tarehe na weka sign.
Andika taratibu bila pupa kama siku tatu andika tu kila utakachokumbuka andika.
Pia peleka kama kanisani mlipofunga ndoa au msikitini.
Hivi hii midungayembe mnaitoaga wapi???????
Nimekasirika na nimehuzunika sana.
Dalili zilianza mapema lakini ukaziignore
Kwa kuwa ushamjua mkeo nakushauri maswala yote ya fedha unazochuma zicontrol mwenyewe
Nadhani ukichwa wa familia ni uwezo wa kutafuta pesa, huo uwezo ninao mkubwa sana na unaongezeka kila siku,
Mkuu nazungumzia Mamilioni ya pesa, sio kumi, ishirini. na ninaangalia huko nako kwenda, nataka kusitisha upotevu wa pesa, nilitegemea nikioa, nitazidisha nguvu za kutafuta pesa alafu kuna mtu wa kuzisimamia.
Utafutaji wangu wa pesa ni wa kukaa ofisini asubuhi hadi usiku, na muda unavyokwenda nahitajika kukaa ofisini zaidi, niliacha kazi ili niweze kusimamia pesa mwenyewe kwa kufanya mambo yangu binafsi, nimelazimika kurudi kwenye ajira, nimempa kazi ya kusimamia ujenzi wa nyumba, sikumuambia atafute pesa za kujenga nyumba lakini ameshindwa.
kwi kwi mwenzako hapa nawaza mtu anakabidhiwa asilimia 80 ya net salary,kutembea na 5 million,ndani kuzilalia si chini ya 20 milioni kila siku.
Weee afu natembelea bmw X5 afu mr anatembelea alteza kama si gx 100.
Mkuu ninadhani, kuna shida katika
1.Mawasiliano.
Ninadhani kama mngekuwa mnawasiliana, kwa ukaribu, haya yasingefika huku.
2. Ufuatiliaji.
Kama ulimpatia jukumu la kusimamia ujenzi wa nyumba, ingekuwa vyema kama ingekuwa ndani ya muda fulani, mf. kutokana na uwepo/upatikanaji wa pesa, kuweka malengo kuwa ni lini ujenzi unategemewa kukamilika, mfano baada ya miezi mitatu(kwa kuwa ilikuwa imefika sehemu nzuri), na tuseme labda baada ya mwezi mmoja kuweka umeme n.k.
Hii ingemfanya asimamie kwa karibu, ili kukamilisha lengo na pili ingefanya kuomba ushauri anapokwama mf. toka kwako(na kuwafanya mwe karibu zaidi).
3. Utafutaji.
Mkuu sina nia mbaya ila wakati fulani mambo haya kwa upande mwingine yanategemea uelewa (elimu).Ni ngumu sana kwa mtu asiyetafuta pesa kupewa jukumu la kusimamia jambo akalikamilisha (kwa kuwa kwa gharama anazoambiwa anaweza akakubaliana nazo kirahisi, kwa kuwa si yeye anayetafuta)..ingekuwa ni vyema kwa mtu kama huyo kuwa na chanzo gulani cha pato, ambacho kwacho anaweza kupata pesa ya kusimamia jambo jingine.
4. Matumizi.
Watu hubadilika, sisemi ndivyo mkeo alivyo, lakini nonasema kuna baadhi ya wanawake wenye kuonyesha umakini mkubwa kabla ya ndoa na baadae kuwa na mtazamo tofauti, hasa kutokana na marafiki kubadilika, kutaka kuonyesha hali tofauti kabla na baada ya ndoa! Kwa kuwa unasema hafanyi kazi yeyote, hebu katika pesa inayokuja asipate hata kidogo, kuonyesha uhitaji wako kwa sasa (simaanishi umfiche bali umweleze kwa nia njema tu, pili umfanye awe na rekodi ya matumizi (kiasi cha pesa kilichopokelewa na mchanganuo wa matumizi yake angalau kwa mwezi kama si kwa wiki.
Nashukuru sana kwa ushauri wako, nitaurudia kuusoma tena na tena.
1. Kuhusu Mawasiliano, nadhani nimejitahidi sana, kama ni kikwazo ni yeye, nimeelezea hili zaidi kwenye moja ya posts zangu.
2. Ufuatiliaji, kuhusu hili, wakati nampa jukumu la kusimamia nyumba nilimpa na maelekezo ya kutosha, na kumpa jukumu la kunijulisha mara anapotaka kufanya maamuzi tofauti ili nimshauri, sikutaka kumpa mtu jukumu alafu nibaki na authority, nilitaka na nikamuamini, hivyo nilimkubalia kufanya chochote anachotaka lakini tupeane habari kabla hatujaingia chumbani kulala, nikamkabidhi na file lenye records zote za ujenzi mpaka pale ulipofikia, nilijua upele umepata mkunaji.
limitation pekee, ilikuwa ni pesa, sikutaka kukopa, hivyo nisingeweza kumpa milioni kumi hata pa, alikuwa anajua kipato chetu, ni nikamueleza hiyo ndio limit ya matumizi yetu kwa mwezi.
yeye akaibuka na agenda ya kuweka kwanza, sikuona tatizo, kila mchezaji anastyle zake, then everything went to the south.
3. Utafutaji
baada ya kufunga ndoa, tulikubaliana tumalizie ujenzi, na ukikamilika ntampa mtaji anaotaka, Japo alianzisha biashara kwa kulazimisha, niliendelea kumsupport, lakini kwa makubalino na ujenzi uanze biashara na ujenzi vifanyike kwa pamoja, na watu wa kumsaidia walikuwapo yeye ndiye aliyewafrustate, na hata alipoanza kulalamika kuhusu hasara na liquidity issues, nilimfund. nilimpatia all the support she needed japo aliendelea kujizungusha kuhusu ujenzi kwa sababu ambazo na mimi nilikuwa mjinga kuzikubali.
4. Matumizi
Mpaka leo, saa moja na dakika kumi na moja kwa majira ya afrika mashariki, hajawahi kunieleza matumizi yake nikayaelewa, hata kulist tu kwamba, saloon milioni moja, mafuta ya gari milioni tatu n.k hajawahi,
Mh! Pole sana kaka unatakiwa ujiatizame wapi uliteleza ili uyaweke mambo yako km yalivyokuwa. Bt kuhusu kuachana na mkeo hutakiwi kufanya maamuzi ya haraka kaa naye tena mzungumze natumai mambo yataenda sawa.pole sana kwa kuumwa kina uf,,,,, hao
Ktk wanaume mabwege naweza kusema ww ni mmoja wao utampaje mwanamke mshahara wako?huyo mkeo kuna mahali hizo hela anazipeleka very soon atakumwaga akishatimiza malengo yake shauri yako tafakari chukua hatua