Naomba ushauri jamani

Bro nashauri tena,huyu mke hakufai.Kama afya yako haijali anajali gari,utakufa bure achana nae mrudishe kwao.Huyo ni mmachame nn? Kaka huyo atakuua ili yeye aendelee kumliki mali funguka tua mzgo huo haraka sana.Vp hajakutarfu kwamba ashaona uzi huu?
 
Mkuu kwanza ninakupa pole Sana narudia tena pole Sana nimesoma kwa makini story yako huku mapigo ya moyo yakiongezeka kwa kasi Sana Kana kwamba ni Mimi yamenikuta!! Narudia tena pole Sana na nimesoma vizuri komenti za wachangiaji wengi wanaona kwamba hukua na mawasiliano ya moja kwa moja,! Kitu Kimoja ambacho kimekuponza ni uaminifu mkubwa Sana kwa mkeo na mkeo ameshakupima akagundua udhaifu wako Ndio maana yote hayo yanatokea! Unaogopa kelele zake na Ndio maana ukimkalisha Hakuna unachopata!! Swala langu ni moja tu MKUU KUANZA UPYA SI UJINGA UMEOA PEPO! Alijifanya mwema kwako wakati wa uchumba kukudhibiti matumizi ili uone huyu anafaa kumbe sio! Baada ya kuingia kwenye ndoa akua mmiliki sasa anafanya hata ambacho hukifanyi! Na kutokana na matendo yake machafu anajua na wewe unaweza fanya Ndio maana ukiwa hata na rafiki zako anakua mkali!! Tokea umemuoa maisha na uchumi unashuka sasa huyo mtu wa nini La mwisho ambalo Kama ni Mimi navunja ndoa siku ya harusi ni kutuma picha za utupu wake kwa wanaume wawili tofauti mkuu nikuulize swali mkeo ulimuolea Mahari milioni Mia sasa unazionea uchungu?!! Mzee ungekua bro wangu mie tungepigana Kama unaendelea kukaa na hilo jini nasikia uchungu Sana yaani!!

Wewe jamani usiite wenzio majini, sio vizuri
 
duh? kumbe na nyie matajiri mna mapito makubwa hivyo? nilizani ni sisi tusio na uhakika wa kula ata mlo mmoja kwa siku! ss tunaamini kwa kudra za mungu hata leo itaitwa kesho! mwamini mungu bro utapata mpenyo tu.

Mkuu, mie sio tajiri ni mpiganaji tu, naelewa hali halisi ilivyo na ndio maana nina hasira.
 
Sangarara pole kwanza kwa ugonjwa unaokusumbua Mungu wetu hawez kukutupa atakuponya kwa mkono wake kwan yy ndie tabibu mkuu. Back to ua topic ushauri tunakupa but mwenye maamuzi ya mwisho ni ww. Japo sijawh kuishi ktk maisha ya ndoa ila ntajitahid nitoe mawazo kwa mtazamo wangu. Mkeo cdhan km anamapenz ya dhat kwako yupo hapo kipesa zaid. Sikulaumu kwa kumpa pesa na kumwachia asimamie ujenz wenu ulijaribu kumfanya ajione part ya ww ktk kila kitu as words says mmekuwa mwili mmoja. Ulimwamin mno na kumpenda na ndipo mkeo kachukulia point ya kufanya afanyayo. Ma dia maisha ni mafupi na tunatakiwa tuishi kwa raha na shida ni changamoto hatuna budi kuzipitia. Biashara inahitaj nidhamu ya pesa ila kwa mkeo naona hili hana na kwa kushirikiana na nduguze. Nisiwe msemaji sanaa zaid ya yote kaa chini tafakari chukua maamuzi yatakayo kuwa bora kwenu. Usifanye maamuzi ya kumfurahisha mtu wakat maumivu unayapata ww. Cheer up!
 
Last edited by a moderator:
Pesa zako mwenyewe zimekuwa fimbo ya kukuchapia.
Ukweli mchungu ni kuwa Mwanamke wa kiafrika ni Mwafrika na unatakiwa kuishi naye kiafrika.

Hata mimi naona ulijivua nafasi yako kama kichwa cha familia ukamuacha Mke wako aongoze 'mapambano', na kwa kweli
'amekupiga' sawasawa.

Kosa la kwanza ni kufikiri ni mwaminifu kwa sababu wakati wa uchumba alikuwa anadhibiti matumizi yako. Hilo ni goli la kwanza alikufunga.........alikuwa 'anabembeleza' ndoa tu akijua fedha unazo na in long run atazikamata tu. Wewe mpaka kufikia mamilioni uliyokuwa nayo kabla ya ndoa alijua unajibana kiasi gani mpaka ukafikia hapo!!

Kosa la pili ni kumuachia madaraka ya uongozi kwenye menejimenti ya uchumi ndani. Hizo fedha na nyumba hakuzitafuta yeye hukutakiwa kumwachia uhuru wa kiasi hicho. Ulitakiwa umwonyeshe polepole na kwa udhibiti maalum (wewe Mwanaume unalijua hili).

Kosa la tatu ni kufikiri Maisha waliyoishi wazazi wako ni sawa na copy na paste. Wao walianza na wakafika hapo na wanajuana. Zama zinabadilika, hawa Wadada wa kileo wengi wao ni 'money oriented'...akikukuta nazo anazipigia 'hesabu ya pembeni'.

Nne kwa bahati mbaya sana siku hizi mahusiano ni kama ya kuwindana. Kuwa na akili kama nyoka na mjanja kama njiwa.

Mwisho: Jipange sasa kama Mwanaume wa Kiafrika (simaanishi umpige).
 
Mkuu pole sana. Mimi kwa leo sina cha kuachangia ila nataka niwakumbushe watu kama hutajali Sangarara. KWa wale ambao walipitiwa, mwezi Septemba au Oktoba hivi (wakati wa Mlipuko Wastegate) nduguyetu huyu alikuwa Nairobi akiwa na matatizo ya kiafya na alileta pst yake hapa mnaweza kuitafuta. Wengi tulitoa ushauri na kwa nature ya tatizo lake wengi tuliishia kumwombea tu kwa Mungu ambaye kwa neema alimponya ndugu yetu nadhania alienda Israel....

Wadau mnisamehe nilitaka kuwakumbusha wale wanaosema sijui Mkewe kabaki Moshi hataki kuanadamana naye Mwanza kwenye matibabu...Nilivyomwelewa no kwamba walienda Moshi kwa wazazi wa Mke then Mke akagoma kwenda Mwanza kwa wazazi wa Mumewe na kwamba wakati jamaa anahangaika na matibabu nje ya nchi, mkewe aligoma kuuza gari lake la thamani na hicho ndio kipindi alichotumia kufanya biashara zaidi...wale tuliosoma ile thread ya ugonjwa na haya anayoyasema hapa tujaribu kuunganisha dots....labda alijua jamaa hata rudi.....NItarudi asubuhi...HERI YA MWAKA MPYA
 
Last edited by a moderator:
Thanks. Hili nimeishalianzisha, sasa kazi yake au nafasi yake kwenye familia inakuwa nini?
kazi yake abaki nyumbani alee maana amewezeshwa kashindwa...inasikitisha kama kuna wanawake wa aina hii...wenzake wanapigwa wananyanyaswa yeye shida nin??alificha makucha???atakuua uyo..mwache haraka.....sio kama ulishindwa kuwa kichwa cha familia bali ulimpenda ukamwamin....mwacheeee
 
Biashara alianzisha nikiwa safarini, mawasiliano huvunjika pale anaposhindwa kutoa accounting ya pesa, nimeishamkaliza zaidi ya mara mia moja, mpaka nimempleka nje ya nchi kupumzika, na huko nikalianzisha, in a friendly and lovely manner, kwamba pesa zinatumika vipi, biashara fulani inaendeleaje, imekufakufaje, nikakuta baadhi ya partiners ni family members wake, kwa pesa alizokili watu wamekataa kumlipa ama kwa kutokuonekana au kwa kudai hawana nikamuomba anipe details zao za kutosha ili niwachukulie hatua za kisheria hata kwa ubabe sababu i have networks hakutoa ushirikiano mpaka leo.

Leo jioni naondoka moshi (nyumbani kwao), kakataa kwenda Mwanza kwamba atakuja baada ya mwaka mpya, bado hili sio tatizo sababu as long as atakuja na anabaki kwa wazazi wake natambua damu ni nzito, sio issue.

bado hapo ninatatizo la mawasiliano?

Mkuu huyo mkeo unamdekeza sana tatizo, unakubaliana nae kila jambo kirahisi so anatake advantage. DONT BE THAT SIMPLE!!
 
Hii ni serious sana.

Nina Mke na mtoto mmoja, ndoa yenu inamiaka mitano sasa, katika swala la uaminifu katika ndoa sijawahi kumhisi mke wangu kutokuwa mwanaminifu, inawezekana ni kwa sababu nimeamua hivyo au inawezekana ni sahihi kabisa kwamba ni mwaminifu mpaka nilipokutana na kitu cha ajabu majuzi.

Naposema namuamini inajumuisha ukweli kwamba,sijawahi kupata kusikia wala kuhisi juu ya tabia mbaya juu yake,kiasi kwamba sikuwahi kufikiria kumfanyia uchunguzi wa namna yoyote ile.

Kwa upande wake, naweza kusema ama haniamini au anawivu sana na mimi, hataki hata nikae na rafiki zangu, ikitokea nimefanya hivyo atanisumbua sana kwa simu na kunikera kiasi cha kufanya hata hayo mazungumzo nayofanya kuwa hayana maana, sababu concentration inakuwa zero kwa ajiri ya kujieleza niko wapi,niko na nani,nafanya nini,kwa nini tuwe hapo na tusiende nyumbani,narudi saa ngapi, na vitisho vingi, na mimi natoka, na mambo mengine mengi tu, haiishii hapo nikirudi nyumbani ndio inakuwa tabu ni ugomvi usio wa kawaida. for five years now.Hiyo ni tisa.

KUMI
MATUMIZI YA PESA
Sijui nilielezeje hili. wakati namtongoza, nilimuona kama mtu mmoja makini sana kwenye mambo ya pesa, kwanza hakuwa tayari tutumie pesa nyingi tukiwa nae, kuna siku tulienda disco tulipotoka disco tukaenda kulala Kilimanjaro kemplinski, kesho yake ilileta ugomvi mkubwa sana, kwamba ninamatumizi makubwa na mabaya ya pesa ukizingatia tulipokuwa disco (maisha club) nilikutana na marafiki kadhaa nikawapiga pombe vibaya sana, so aliweza mpaka kunieleza kwenye pombe tu tumetumia kiasi gani (alichukua bili zote nilizolipia).

Na katika swala la Pombe akanilazimisha niache, nami nikapunguza kiasi.

Kabla ya Kufunga ndoa, tayari nilikuwa na maisha safi kabisa, nasomesha ndugu zangu, nimejenga nyumba yangu LockCity na nikawa naendeleza kiwanja viwanja viwili DAR.

Baada ya Kufunga ndoa, kila kitu kikasimama.

Nyumba moja niliyokuwa najenga, nilimpatia bwana mdogo wangu aimalizie alafu akae yeye, mimi nikaendelea kupanga nikiamini with my economist wife, ntamalizia hiyo nyumba nakuamia ndani ya mwaka mmoja. wapi, hiyo nyumba nimeishia kuiuza mwaka huu.

PESA ZINAKWENDA WAPI.
Nampa yeye, kwanza nilimpa kazi ya kusimamia hiyo nyumba iishe, kwa mantiki kwamba ni nyumba yake,aimalizie kwa namna roho yake inavyopenda na kuifurnish kwa umaridadi wa aina anayoiota yeye.

Kwanza alianza kunieleza anazungusha hizo pesa, na kweli nyumbani akawa na mahela mengi kwelikweli, japo nilikuwa namkanya, lakini aliendelea kusisitiza kwamba biashara anazofanya zinahitaji awe na pesa wakati wote, anakaa na zaidi ya milioni ishirini ndani, anatembea kwenye gari na si chini ya milioni tano, nikastudy biashara husika nikaona kuna ukweli wa kuhitaji kuwa na pesa mkononi, lakini nikimuambia tukae nimsaidie kupiga hesabu tujue anapataje faida anakataa tena anakuwa mkali kwelikweli.

Mwisho wa siku, ananiletea story inayoonyesha kwamba kuna watu wanachelewa kumlipa pesa zake, namuongezea, wakati huo asilimia themanini ya mshahara nampatia.

Ni mengi Jamani, kuna mambo positive anafanya, lakini ndio kama kubadirisha thamani za ndani,kubadirisha gari,n.k

Mwaka huu mwezi wa saba, nikaachana na mambo ya kuajiriwa, nikaanza kufanya mambo yangu mwenyewe, niliamini kwamba, mambo ya chakula, nyumbani hayawezi kumshinda, pango la nyumba siwezi kushindwa kulipa.

Mwaka huu nikapata matatizo ya kiafya, nikalazimika kuuza haraka sana nyumba iliyokuwa haijaisha (ambayo alishindwa kuiendeleza kwa asilimia zaidi ya tisini), nikauza na kiwanja changu, magari mawili niliyokuwa natumia, nasikia gari analotumia yeye ambalo ndio lenye thamani kubwa kulinganisha na yale niliyokuwa natumia mimi alikataa kuuza, japo ndilo nilimuelekeza aliuze nikijua litauzika kwa haraka, yeye aliniambia hakuna mtu aliyejitokeza japo kuliulizia.


Naomba msaada, najua atapita hapa kusoma na ataelewa ni mimi nimepost, na namzungumzia yeye, lakini kwa kweli kabisa, nafikilia kulifikisha swala hili kwa wazazi na ndugu zangu ndani ya wiki mbili hizi nikiwa mwanza, nafikiria kuachana na huyu mwanamke.

Nimeamua kulileta hili hapa, kwanza ili kupunguza pressure na hazira nilizonazo, na zaidi kupata ushauri usioegemea upande wowote, sababu najua nilifikisha home, uwezekano wa kupita hata bila kujadiliwa ni asilimia zaidi ya mia, na nimejizuia kufanya hivyo kwa muda mrefu nikijua matokeo ndio yatakuwa hayo.

Sijaelewa in all this kwa nini unataka kumuacha Mkeo?
 
Biashara alianzisha nikiwa safarini, mawasiliano huvunjika pale anaposhindwa kutoa accounting ya pesa, nimeishamkaliza zaidi ya mara mia moja, mpaka nimempleka nje ya nchi kupumzika, na huko nikalianzisha, in a friendly and lovely manner, kwamba pesa zinatumika vipi, biashara fulani inaendeleaje, imekufakufaje, nikakuta baadhi ya partiners ni family members wake, kwa pesa alizokili watu wamekataa kumlipa ama kwa kutokuonekana au kwa kudai hawana nikamuomba anipe details zao za kutosha ili niwachukulie hatua za kisheria hata kwa ubabe sababu i have networks hakutoa ushirikiano mpaka leo.

Leo jioni naondoka moshi (nyumbani kwao), kakataa kwenda Mwanza kwamba atakuja baada ya mwaka mpya, bado hili sio tatizo sababu as long as atakuja na anabaki kwa wazazi wake natambua damu ni nzito, sio issue.

bado hapo ninatatizo la mawasiliano?

watu wanaotoka huku nasikia wako makini sana na pesa
 
Tatizo la msingi, ambalo limeoccupy ubongo wangu kwa muda mrefu ni kwamba, toka nimekuwa naye maendeleo yamesimama kabisa, maendeleo niliyofanya nikiwa mwenyewe miaka miwili kabla ya kuwa naye sijatafikia hata kwa asilimia tano kwa miaka mitano niliyokuwa naye. hayo mengine ni bonus tu. Na majibu ambayo amekuwa akinipa juu ya kutokuonekana kwa mamilioni ya pesa ni majibu ambayo huwa yananitoa machozi, sometimes anasema "mi sijui we fanya unalotaka kufanya"

swala la kukataa kuuza gari wakati nikiwa katikati ya kifo na uzima, naambiwa na ndugu zangu ambao najua wako biased naye pia, kwa hiyo sio issue, sababu inawezekana lilikosa mteja kweli.


kwani wewe unaumwa nini? inawezekana huo ugnjwa ukakupa pressure zaidi, ukiachia mbali hela za matibabu vp anakujali kwa jinsi unavyoumwa?
kuhusu pesa za ujenzi kwa nini umpe yeye kama unaona hawezi ungeacha mara moja kuendelea kumpa na ungefanya mwenyewe hayo maendeleo yako..yeye unampa hela yake ya mboga baaaaas..akinuna anune lkn umweleze ukweli mwanzo mwisho..
sioni haja ya kumuacha unless umeprove beyond resonable dought anakusaliti
 
kwani wewe unaumwa nini? inawezekana huo ugnjwa ukakupa pressure zaidi, ukiachia mbali hela za matibabu vp anakujali kwa jinsi unavyoumwa?
kuhusu pesa za ujenzi kwa nini umpe yeye kama unaona hawezi ungeacha mara moja kuendelea kumpa na ungefanya mwenyewe hayo maendeleo yako..yeye unampa hela yake ya mboga baaaaas..akinuna anune lkn umweleze ukweli mwanzo mwisho..
sioni haja ya kumuacha unless umeprove beyond resonable dought anakusaliti

Swala la ugonjwa limepita, ni miezi kama mitatu iliyopita, niko safi kabisa kwa sasa. nashukuru kwa ushauri.
 
Nadhani ukichwa wa familia ni uwezo wa kutafuta pesa, huo uwezo ninao mkubwa sana na unaongezeka kila siku,

basi usimpe pesa bana, yanini ugomvi fanya kama vile uanishi na katoto ambako hakajui matumizi ya hela halafu fanya kila kitu mwenyewe..naamini unaweza..halafu baada ya miaka 2 mkalishe chini umpe tathmini ya kabla ya ndoa, baada ya ndoa na baada ya wewe kumnyima fursa ya kushika pesa zako..ulinganishe maendeleo yenu yalivyo..
wala uismdai hizo hela ulizompa wewe mwache afanye hayo mabiashara yake na wala usimfuatilie, anza upya as if umeibiwa a utafanikiwa, na yeye ataona aibu km ana mshipa wa fahamu..
wanawake wengine bana wanatia kichefchefu kweli..sijui kwa nini sisi hatupati waume wa staili hii
 
Back
Top Bottom