Mkuu ninadhani, kuna shida katika
1.Mawasiliano.
Ninadhani kama mngekuwa mnawasiliana, kwa ukaribu, haya yasingefika huku.
2. Ufuatiliaji.
Kama ulimpatia jukumu la kusimamia ujenzi wa nyumba, ingekuwa vyema kama ingekuwa ndani ya muda fulani, mf. kutokana na uwepo/upatikanaji wa pesa, kuweka malengo kuwa ni lini ujenzi unategemewa kukamilika, mfano baada ya miezi mitatu(kwa kuwa ilikuwa imefika sehemu nzuri), na tuseme labda baada ya mwezi mmoja kuweka umeme n.k.
Hii ingemfanya asimamie kwa karibu, ili kukamilisha lengo na pili ingefanya kuomba ushauri anapokwama mf. toka kwako(na kuwafanya mwe karibu zaidi).
3. Utafutaji.
Mkuu sina nia mbaya ila wakati fulani mambo haya kwa upande mwingine yanategemea uelewa (elimu).Ni ngumu sana kwa mtu asiyetafuta pesa kupewa jukumu la kusimamia jambo akalikamilisha (kwa kuwa kwa gharama anazoambiwa anaweza akakubaliana nazo kirahisi, kwa kuwa si yeye anayetafuta)..ingekuwa ni vyema kwa mtu kama huyo kuwa na chanzo gulani cha pato, ambacho kwacho anaweza kupata pesa ya kusimamia jambo jingine.
4. Matumizi.
Watu hubadilika, sisemi ndivyo mkeo alivyo, lakini nonasema kuna baadhi ya wanawake wenye kuonyesha umakini mkubwa kabla ya ndoa na baadae kuwa na mtazamo tofauti, hasa kutokana na marafiki kubadilika, kutaka kuonyesha hali tofauti kabla na baada ya ndoa! Kwa kuwa unasema hafanyi kazi yeyote, hebu katika pesa inayokuja asipate hata kidogo, kuonyesha uhitaji wako kwa sasa (simaanishi umfiche bali umweleze kwa nia njema tu, pili umfanye awe na rekodi ya matumizi (kiasi cha pesa kilichopokelewa na mchanganuo wa matumizi yake angalau kwa mwezi kama si kwa wiki.