Naomba ushauri jamani

Naomba ushauri jamani

Aiseee sijui hata wa wapi wengine tunahangaika na maisha na kulea familia bila msaada halafu yeye anachezea nafasi kama hii..kweli akili ni nywele.
mxxiiuuuuu
yaani nimekasirika utafikir nn, huyu mwanamke ametokea sayari gani? sisi wengine hata hela ya mboga hatupewi yeye anachezea hela ya ujenzi, mxxxxiuuu
 
Je ktk ugonjwa wako,anaonyesha kujali?au ni ilimradi tia maji tia maji.kama anakujali basi ni hali tu itapita,ila km ktk kuugua kwako hajitumi bs huyo ni mwanamke mpmbavu na ataibomoa nyumba yake mwenyewe
 
Hapana hapo naona kama unakosea kuwa kichwa cha familia sio kwa kutafuta pesa pekee bali ni uwezo wa kuongoza mambo ndani ya nyumba,kwa mfano hapo kwenye ujenzi wa nyumba usingetakiwa umwachie majukumu yote hata kama ni kwa mapenzi tuu..bali ungepaswa mshirikiane..ila inaonekana kuna mengi yaliyokufanya ufikie uamuzi wa kuachana nae..siwezi kukupinga wala kukuunga mkono
Nadhani ukichwa wa familia ni uwezo wa kutafuta pesa, huo uwezo ninao mkubwa sana na unaongezeka kila siku,
 
Anyway. Nimekuta anachat na wanaume wawili tofauti, akiwatumia na picha kuonyesha mwili wake.

Duh pole kaka.....huhitaji kamati hapo....maliza mambo mwenyewe... mengine yataendelea tuuu.
 
Dah!
Mkuu pole sana

Nijuavyo mimi ni kuwa sina hakika kama alikuwa mwema tangu mwanzo ila alikuwa ana act tu

Cha kufanya ninachoona kwasasa ni kujaribu kuchunguza kama hapo mwanzo alikuwa na tabia hizi maana kujua mwanzo kama alikuwa na tabia hizi utatuzi wa tatizo hili utakuwa tofauti

Kama hakuwa hivyo mwanzo ni hapo utakapoanzia kutafiti kilichomfanya akawa hivi

Ila ki ukweli mke bora na anaefaaa ni yule anaejijua na kujua yeye ni nani
Kitendo cha wewe kumuamini kiasi hicho kinaweza kuwa kimemharibu kabisa

Yaani hata sijui niseme nini
Hii imeniumiza sana kwa kweli

Hebu ngoja nitafakari huenda nikaja na maelezo mazuri zaidi.......!!!
 
dah bro najua unapata tabu sana na hilo hapo usiite familly na kuwapa faida nyingi ukizingatia kwamba mke ni wewe ndie ulie mchagua mwiite shemegi mkae chini nyonte wawili muwe wa wazi kabisa muliongelee hilo suala halafu pima akili yake oune kama yupo tayari kubadilika basi anzeni ukurasa mwengine hayo ndio maisha huo ndio ukubwa ukiongea nae usiwe na jazba na ukiona humuelewi elewi basi mkuu hapo kuna jambo nakutakia kila la kheri ila na wee pia punguza kutoka toka sana au kukawia kurejea home hivyo ndio vitu ambavyo wake zetu hua ndio vina sababisha waingiwe na fikra potofu na gafla unaona wanabadilika
 
Sangarara leo nlikuwa nasoma kama guest tu ila umenifanya nilog in.
Eeee hilo dege ulilolivaa ni balaa.
Hapo huna mke.
Maneno mengi sina peleka kwa wazazi tena andika vizuri sana kwenye karatasi point zake toa photocopy au maandishi yaprint andika tarehe na weka sign.
Andika taratibu bila pupa kama siku tatu andika tu kila utakachokumbuka andika.
Pia peleka kama kanisani mlipofunga ndoa au msikitini.
Hivi hii midungayembe mnaitoaga wapi???????
Nimekasirika na nimehuzunika sana.

Amu, umenena.

Japo sikubaliani nawe kuhusu 'udungaembe🙂!

Truly truly I tell you... Hakuna holistic solution for every marriage situation! Ndoa zingine mshahara wa mume aujua yeye tu, mke haujui and as far as matumizi (Development & Recurrent) vinaenda vizuri hakuna 'matata'. Ndoa zingine Mama na baba wajumuisha mapato yao bila kificho na mambo hayaendi. Ndoa zingine baba ampenda mama na ampa mshahara/mapato yote na mambo hayaendi, etc, etc..

Kwako Sangarara kilichokukwaza sana katika 'episode' hii ni picha za utupu kwa wanaume wengine ukiwa umemwamini sana sana sana mwandani wako mpenzi. Kwa hili sina ushauri wa kijasiri ndugu yangu. Ila Amu ameshauri uandike kwa utulivu matukio yote unayodhani yaliashiria matumizi mabaya, maamuzi mabaya na yasiyo shirikishi, na kadhalika. Ikitokea mmeenda katika kikao cha kujadiliana, wewe soma 'hotuba' yako kama Ben Mkapa kwani utakuwa umeiandaa na kuihariri kwa muda na hivo itakuwa imepunguza unnecessary emotions but facts.

I wish you a happy ending, brother!

PP
 
Siwezi kushauri uachane naye, lakini ndo option pekee ambayo itakufanya urudi kwenye mstari.
Kama unasoma vitabu vya dini zote mwanamke ametajwa kama kiumbe dhaifu na maandiko yameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa inatakiwa tuishi nao kwa akili. Mwanamke hawezi kusalimika kama atakuwa anafanya kazi ambazo muda mwingi zitamkutanisha na wanaume na hilo wanaume tunalijua ingawa huwa tunajiaminisha kuwa wa kwangu hawezi kunisaliti kwa kuwa ni mwaminifu. Mwanamke hatakiwi kuwa karibu na mwanaume na kuzoeana naye kwa njia yoyote ile, hata rafiki yako wa kiume kama anakuja nyumbani kwako haupo anakaa anakusubiri mara ya tatu atamtania mkeo, nadhani unajua nini kitafuata, kwa aibu ataambiwa hivi na wewe unaweza kunifanyia hayo?
Mwanamke akishakuwa na kipato chake mwenyewe cha kuweza kujitoshereza mahitaji, wanaishi na waume zao asilimia 20 hawafiki. wengine huwa wanadiliki kuwauwa waume zao kwa kuona hawana maana tena na wanawanyima uhuru.
Hayo maneno aliyokwambia na kuchati na watu na kuwaonyesha nyeti zake kurudi nyuma mpaka maombi, lakini si ushawishi wa wazee. Tuombe Mungu mrudiane, lakini ufanye juu chini wewe ndo utawale kipato cha familia na siyo yeye, huo ndo uanaume.
 
Dah!
Mkuu pole sana

Nijuavyo mimi ni kuwa sina hakika kama alikuwa mwema tangu mwanzo ila alikuwa ana act tu

Cha kufanya ninachoona kwasasa ni kujaribu kuchunguza kama hapo mwanzo alikuwa na tabia hizi maana kujua mwanzo kama alikuwa na tabia hizi utatuzi wa tatizo hili utakuwa tofauti

Kama hakuwa hivyo mwanzo ni hapo utakapoanzia kutafiti kilichomfanya akawa hivi

Ila ki ukweli mke bora na anaefaaa ni yule anaejijua na kujua yeye ni nani
Kitendo cha wewe kumuamini kiasi hicho kinaweza kuwa kimemharibu kabisa

Yaani hata sijui niseme nini
Hii imeniumiza sana kwa kweli

Hebu ngoja nitafakari huenda nikaja na maelezo mazuri zaidi.......!!!

kabisaaaa Eiyer alikuwa ana act ili aolewe
 
Eiyer huyu mke wa mleta thread enz za uchumba wao alikuwa anact as u said. Hawez akaolewa then tabia ibadilike ghafla.
 
Last edited by a moderator:
duu mkuu pole sana,huyo mtoto wa moshi atakusumbua sana kama umeamua we piga chini maisha ya songe kama zamani.
 
M najiuliza kwann during uchumba awe anajali matumiz ya pesa then baada ya kuolewa asiwe mtu wa kujali pesa?

Wanawake ni wazuri sana wa ku act siku hizi...!!!!!!!!!!
 
Aisee mwanaume wa kisukuma DILII EEH...
Unachezea kutafta ndoa wew,lazma ufiche u'golddigger ujitofautishe na wanawake wengi wapenda pesa...utazila vizuri ukisha olewa,ndoa si yako bwana
MTOA MADA,hela mpe na umtimizie mahitaji yake kama wife,BUT HAYO MAMBO YA UJENZI,SIMAMIA WEWE,AU IPE KAMPUNI IWAJENGEE,ishi nae cz tyr mshaoana but fatilia ya mmsingi na maendeleo kwenye familia yako...
 
Hii ni serious sana.

Nina Mke na mtoto mmoja, ndoa yenu inamiaka mitano sasa, katika swala la uaminifu katika ndoa sijawahi kumhisi mke wangu kutokuwa mwanaminifu, inawezekana ni kwa sababu nimeamua hivyo au inawezekana ni sahihi kabisa kwamba ni mwaminifu mpaka nilipokutana na kitu cha ajabu majuzi.

Naposema namuamini inajumuisha ukweli kwamba,sijawahi kupata kusikia wala kuhisi juu ya tabia mbaya juu yake,kiasi kwamba sikuwahi kufikiria kumfanyia uchunguzi wa namna yoyote ile.

Kwa upande wake, naweza kusema ama haniamini au anawivu sana na mimi, hataki hata nikae na rafiki zangu, ikitokea nimefanya hivyo atanisumbua sana kwa simu na kunikera kiasi cha kufanya hata hayo mazungumzo nayofanya kuwa hayana maana, sababu concentration inakuwa zero kwa ajiri ya kujieleza niko wapi,niko na nani,nafanya nini,kwa nini tuwe hapo na tusiende nyumbani,narudi saa ngapi, na vitisho vingi, na mimi natoka, na mambo mengine mengi tu, haiishii hapo nikirudi nyumbani ndio inakuwa tabu ni ugomvi usio wa kawaida. for five years now.Hiyo ni tisa.

KUMI
MATUMIZI YA PESA
Sijui nilielezeje hili. wakati namtongoza, nilimuona kama mtu mmoja makini sana kwenye mambo ya pesa, kwanza hakuwa tayari tutumie pesa nyingi tukiwa nae, kuna siku tulienda disco tulipotoka disco tukaenda kulala Kilimanjaro kemplinski, kesho yake ilileta ugomvi mkubwa sana, kwamba ninamatumizi makubwa na mabaya ya pesa ukizingatia tulipokuwa disco (maisha club) nilikutana na marafiki kadhaa nikawapiga pombe vibaya sana, so aliweza mpaka kunieleza kwenye pombe tu tumetumia kiasi gani (alichukua bili zote nilizolipia).

Na katika swala la Pombe akanilazimisha niache, nami nikapunguza kiasi.

Kabla ya Kufunga ndoa, tayari nilikuwa na maisha safi kabisa, nasomesha ndugu zangu, nimejenga nyumba yangu LockCity na nikawa naendeleza kiwanja viwanja viwili DAR.

Baada ya Kufunga ndoa, kila kitu kikasimama.

Nyumba moja niliyokuwa najenga, nilimpatia bwana mdogo wangu aimalizie alafu akae yeye, mimi nikaendelea kupanga nikiamini with my economist wife, ntamalizia hiyo nyumba nakuamia ndani ya mwaka mmoja. wapi, hiyo nyumba nimeishia kuiuza mwaka huu.

PESA ZINAKWENDA WAPI.
Nampa yeye, kwanza nilimpa kazi ya kusimamia hiyo nyumba iishe, kwa mantiki kwamba ni nyumba yake,aimalizie kwa namna roho yake inavyopenda na kuifurnish kwa umaridadi wa aina anayoiota yeye.

Kwanza alianza kunieleza anazungusha hizo pesa, na kweli nyumbani akawa na mahela mengi kwelikweli, japo nilikuwa namkanya, lakini aliendelea kusisitiza kwamba biashara anazofanya zinahitaji awe na pesa wakati wote, anakaa na zaidi ya milioni ishirini ndani, anatembea kwenye gari na si chini ya milioni tano, nikastudy biashara husika nikaona kuna ukweli wa kuhitaji kuwa na pesa mkononi, lakini nikimuambia tukae nimsaidie kupiga hesabu tujue anapataje faida anakataa tena anakuwa mkali kwelikweli.

Mwisho wa siku, ananiletea story inayoonyesha kwamba kuna watu wanachelewa kumlipa pesa zake, namuongezea, wakati huo asilimia themanini ya mshahara nampatia.

Ni mengi Jamani, kuna mambo positive anafanya, lakini ndio kama kubadirisha thamani za ndani,kubadirisha gari,n.k

Mwaka huu mwezi wa saba, nikaachana na mambo ya kuajiriwa, nikaanza kufanya mambo yangu mwenyewe, niliamini kwamba, mambo ya chakula, nyumbani hayawezi kumshinda, pango la nyumba siwezi kushindwa kulipa.

Mwaka huu nikapata matatizo ya kiafya, nikalazimika kuuza haraka sana nyumba iliyokuwa haijaisha (ambayo alishindwa kuiendeleza kwa asilimia zaidi ya tisini), nikauza na kiwanja changu, magari mawili niliyokuwa natumia, nasikia gari analotumia yeye ambalo ndio lenye thamani kubwa kulinganisha na yale niliyokuwa natumia mimi alikataa kuuza, japo ndilo nilimuelekeza aliuze nikijua litauzika kwa haraka, yeye aliniambia hakuna mtu aliyejitokeza japo kuliulizia.


Naomba msaada, najua atapita hapa kusoma na ataelewa ni mimi nimepost, na namzungumzia yeye, lakini kwa kweli kabisa, nafikilia kulifikisha swala hili kwa wazazi na ndugu zangu ndani ya wiki mbili hizi nikiwa mwanza, nafikiria kuachana na huyu mwanamke.

Nimeamua kulileta hili hapa, kwanza ili kupunguza pressure na hazira nilizonazo, na zaidi kupata ushauri usioegemea upande wowote, sababu najua nilifikisha home, uwezekano wa kupita hata bila kujadiliwa ni asilimia zaidi ya mia, na nimejizuia kufanya hivyo kwa muda mrefu nikijua matokeo ndio yatakuwa hayo.

kaka ulifanya haraka sana kumkabidhi majukumu makubwa kama hayo ambayo humfanya mtu ajiamini kupitiliza juu yako..
Kuhusu picha maybe ni kweli anacheat ila pata data kamili kwanza ili kama utaweza kumuonya ufanye kwa uhakika bila ya yeye kujitetea...
Mwisho kaa nae ongea nae mueleze kila kitu hasa maamuzi yako ambayo unataka kuyafanya ili ajue kama hatabadilika kinachofata ni nini..
Kama unataka kulinda ndoa yako jaribu kufanya hayo ila kama umeshamchoka basi fanya yako.
 
Dah,pole sana bro.cna uhakika km alikua ana-act
Tatzo la wanawake ni 1 tyu...anamthamini anayemnunulia vocha kuliko yule alemnunulia simu.
Hapo lazma kuna mtu anampa jeuri tyu...fanya uchunguzi kwa ilo then utajua tyu
 
Dah!
Mkuu pole sana

Nijuavyo mimi ni kuwa sina hakika kama alikuwa mwema tangu mwanzo ila alikuwa ana act tu

Cha kufanya ninachoona kwasasa ni kujaribu kuchunguza kama hapo mwanzo alikuwa na tabia hizi maana kujua mwanzo kama alikuwa na tabia hizi utatuzi wa tatizo hili utakuwa tofauti

Kama hakuwa hivyo mwanzo ni hapo utakapoanzia kutafiti kilichomfanya akawa hivi

Ila ki ukweli mke bora na anaefaaa ni yule anaejijua na kujua yeye ni nani
Kitendo cha wewe kumuamini kiasi hicho kinaweza kuwa kimemharibu kabisa

Yaani hata sijui niseme nini
Hii imeniumiza sana kwa kweli

Hebu ngoja nitafakari huenda nikaja na maelezo mazuri zaidi.......!!!

Kiongozi
huyu mwanamke kabadirika, hakuwa hivyo, kabadirika kwa maneno na matendo.
 
Back
Top Bottom