UFASHE MLIBHONA
Senior Member
- Nov 28, 2012
- 177
- 51
Housegirl wetu kwa kweli alikuwa ni dada mzuri, kwa kazi, malezi ya watoto. Wote katika familia tulimpenda. Siku zinavyokwenda naona anazidisha upendo kwa familia yangu Majuzi kajilengesha hadi nikashindwa kujizuia, nikatembea naye. Nimejisikia vibaya sana, nimeamua kumshawishi mke wangu tumfukuze. Housegirl ameapa tukimfukuza atamweleza mke wangu kila kitu bora nimwache aendelee kuishi nasi. sina amani .Natamani kumweleza mke wangu ukweli. Natamani niikimbie nyumba Ninamwogopa sana mke wangu, namheshimu naona ataniona mtu wa ajabu kweli. sijawahi kufanya kitu cha namna hiyo. Maji yamefika shingoni. Naomba ushauri kwa wazoefu