Naomba ushauri wana jamii forum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba ushauri wana jamii forum

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Emecka, Jul 20, 2012.

 1. Emecka

  Emecka Member

  #1
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Ilikuwa ni mwaka 2005 nilipokuwa nasafiri toka Mtwara kuja Lindi, (mtwara ndio nyumbani na Lindi ni kituo cha kazi) ndani ya basi nilikaa kiti kimoja na mkaka mtanashati.. tulisalimiana na kila mtu akachukua hamsini zake… safari iliendelea lakini kwa bahati mbaya gari tulilokuwa tumepanda lilipata tatizo tuteremka na kusubiri matengenezo, ndipo nilipoanza kufahamiana na jirani yangu niliyekuwa nimekaa naye. Alijitambulisha kwa jina na Joe, nikajitambulisha naitwa Emecka. Tukaanza kupiga stori za hapa na pale, Lahaula kumbe Joe anaifahamua familia yangu na mimi nilikuwa naifahamu familia yake ila sisi wenyewe hatukuwa tunafahamiana kwani yeye anaishia Dar es salaam na mimi nilitoka Mtwara miaka mingi iliyopita kwa hivyo hatukuwahi kufahamiana ila Joe alisoma na baadhi ya dada zangu (watoto wa baba mdogo).

  Alinieleza short history ya maisha yake kwamba aliwahi kuzaa na mwanamke ila kwa vile Yule mwanamke alikuwa muislamu hawakuweza kufunga ndoa kwani wazazi wa Yule mwanamke hawakutaka binti yao abadili dini kwa hivyo aliachana na yule mwanamke ila walikuwa wamezaa mtoto mmoja… Gari lilitengemaa tuaendelea na safari, tukiwa tunapiga story zaidi na zaidi. Tulifika Lindi kwenye saa 02 za usiku, Joe alinisindikiza mpaka kwa dada yangu ambako ndio nilikuwa ninaishi kwa kipindi kile then akarudi kaw mdogo wake alipokuwa amefikia. Tuliandelea kuwasialiana kwa muda wa wiki moja ambapo Joe alikuwa bado yupo Lindi ghafla tulianza kupendana na na baada ya muda tukawa wapenzi. Joe alirudi zake DSM na mimi niliendela na kazi hapa Lindi, kuna wakati nilikuwa nakwenda DSM kumsalimia Joe, nilikuwa nafikia kwake kwani alikuwa anaishi yeye, mwanaye na housegirl.. nilikuwa free kwa chochote kile.. Tulidumu kwa muda wa mwaka 1 hivi baadaye mawasiliano yakapungua na mwishowe yakaisha,”kama mnavyojuwa mapenzi ya mbali” tukajikuta tumeachana automatically na kubaki kuwasialiana mara chache sana mwishowe tukapoteza mawasiliano kabisa..

  mwaka 2008 nikakutana na mdogo wake Joe akanieleza kuwa joe kafunga Ndoa na mjukuu kwa kigogo mmoja hivi wa CCM mwenyeji wa Tanga, basi sikutaka kuchukua mawasialiano, nilisema tu hongera zake na kuendelea na misha yangu. Mwaka 2011 mwishoni alikuja mdogo wake na Joe akitaka kuzungumza na mimi, nilikubalia wito wake tulikaa mahali flani tukazungumza mambo mengi, ila kikubwa ni ujumbe kutoka kwa Joe akiomba msamaha kwa kukatisha mawasiliano, na anaomba namba yangu ya simu ili awasiliane na mimi, nikamuuliza kwani si ana mke anataka nini kwangu tena?
  Basi ndo mdogo wake Joe akanisimulia visa vya Yule mke.. kuwa ni mkorofi na wameshindwana na ameshaomba talaka na kesi ipo mahakamani… nilimpa namba yangu kwa shingo upande na kwa masharti kwamba mimi nina mchumba (ingawa nilikuwa na mpenzi ila hatukuwa na makubaliano ya kuonana) kama anataka kuwa na mimi tena hiyo nafasi haipo tena. Basi Joe alinipigia kila mara kutaka maendeleo yangu na mchumbaangu…

  nilimpiga tarehe ila hakukata tama akasema nitatakata tama siku nikisikia umefunga ndoa ndo utakuwa mwisho wangu wa kukusumbua.
  Basi tuliwasiliana na mwisho wa siku Joe alifunga safari kutoka DSM na kuja Lindi kutaka kuzunguma na mimi kuhusu ndoa kati yangu mimi naye. Kwa bahati mbaya au nzuri alifika wakati niliokuwa nimeachana na Yule mpenzi wangu kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu. Nilijikuta naanza kurudisha upendo kwa Joe. Niliomba ushauri kwa ndugu zangu wakanieleza kama aliweza kuachana na mkewe wa ndoa atawezaje kuishi na mimi bila kuachana? Naomba ushauri jamani nipo njia panda katka kutoa maamuzi ya kukubali kufunga ndoa na Joe.. Samahani sana kwa kuwachosha..
   
 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  "GHAFLA TUKAPENDANA" tatizo liko hapo!Upendo upi wa ghafla?
   
 3. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sasa hofu ipo wapi mdada, kama hakuna kipingamizi oaneni muendeleze maisha. Usiogope kuwa ameachana na wa kwanza, inawezekana wewe ndie bahati yake na wa kwanza alitangulia tu kukamilisha maisha.
   
 4. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hujawahi kumpenda mtu ghafla? Wajikuta unampenda tu bila sababu hali ya kuwa humfahamu vizuri huyo mtu?
   
 5. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,733
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Usiogope! Usiogope! Kumkubalia mtu si kufunga ndoa. Fanya taratibu zote za uchumba, kwa kuwa mahusiano (urafiki) ulikuwako toka awali na familia zinafahamiana. Ila usiendeshwe na 'hasira' za kimapenzi. Pata muda wa kutosha. Mapenzi hayana kanuni.
   
 6. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  jamaa anaoa then mambo yanatokea badala asolve anatafuta mwingine wa kuoa then matatizo yatokee afu aoe mwingine.....na wew utaolewa,ataona kuna mambo na matatizo yanakuja atakuacha ataoa mwingine...akili zako changanya na za mbayuwayu...
   
 7. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2012
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ewaa kwa mwenendo wa huyo jamaa ategemee maumivu tu
   
 8. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Sema unahemkwa.Upendo una taratibu zake bana!
   
 9. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  "kama mnavyojuwa mapenzi ya mbali"nimechukuwa haya maneno ili ujue kosa lilianzia wapi.Tukiachana na hayo maana yameishapita,una haki ya kuwa njia panda,sikiliza kwanza wewe mwenyewe upendo wako kwake,huwezi jua mipango ya Mungu inawezekana mpaka kifo kikawatenganisha.Nikutakie kila la kheri.Yangu ni hayo machache ngoja na wengine waje.
   
 10. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Joe asije kuzusha kizaazaa ukarudi JF kuomba ushauri...........tulia acha haraka na ikiwezekana nenda Dar ili angalau upate ukweli wa kuutafuta si kuletewa
   
 11. mdida

  mdida JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 1,608
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  jamaa hajatulia kabisa, kwa nini ampoteze mawasiliano then akiona kimenuka ndo akutafute, control+alt+delete=end task.
   
 12. Mwanawalwa

  Mwanawalwa JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 1,015
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  dah you know , at the right time and circumstance God will bring to you the right person whom you will share you whole life together may be it's your right time now piga maombi sana huenda ndiye uliyepangiwa bana . yesterday is history tommorow is mystery ,jus bury the past , only God knows what will happen next all the best my dear
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  binti unapenda kuwa spare Tyre eeeehhhhhhhhhh?

  alivyooa hakujua kama upo?

  au kipindi kile hukuwa na vigezo vya kuolewa nae?

  sasa hivi vigezo umepata wapi?

  kweli kuna wanawake mnapenda kutumika.....angekupenda na kukuthamini asingeoa.....

  nakutakia u-spea tairi mwema...
   
 14. Emecka

  Emecka Member

  #14
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  ndugu huenda kiswahili ndio kigumu kwangu, katika mawasiliano ndipo upendo ulipoanza halafu tukawa wapenzi.. pole kama hukunielewa
   
 15. Emecka

  Emecka Member

  #15
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  asante kwa ushauri, na hilo ndilo nitakalolifanya kwanza kabla ya yote.
   
 16. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  hiki ni kizungumkuti ingawa you are free kujaribu bahati yako kwa Joe... it might work
   
 17. Emecka

  Emecka Member

  #17
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15

  BADILI TABIA, to be honest kipindi hicho alitaka sana kuniona kabla hajafunga ndoa na mwanamke wa pili ila kwa kipindi hicho mimi nilikuwa sijui ndoa ni nini yaaani nilikuwa sijakuwa kiakili kumbuka ilikuwa mwaka 2005, nilikataa kwani nilijiona bado ni mdogo. kwa hiyo ni mimi ndie nilikataa sio yeye nilikwua nachukulia kama b-friend na g-friend tu, wazo la kuwa na familia sikuwa nalo, sasa nimekuwa nina maamuzi yangu na nina imani kuwa naweza kuimudu familia na maisha kwa ujumla. pia kumbuka kipindi hiko nilikuwa naishi kwa dada yangu kwa hiyo ahata masuala ya kuishi kwa kujitegemea sikujua.
   
 18. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Unajua sisi binadamu tunaona yanayoonekana kwa MACHO yetu tu..bali yasiyoonekana hayo ni ya MUNGU!
  Kukushauri kuhs hii mada yako..labda niseme tu kuwa..USIKILIZE moyo wako na jaribu kujiwekea vigezo vyako ili umpime kwa hivyo..kama walau kwa asilimia kubwa atafit basi chukuaneni..Lakini hii habari ya kusema..'mbona kamuacha flan na wewe atakuacha'..hizi ni swaga tu!!..mbona kuachana kwenye mapenzi ni kitu cha kawaida tu!!!
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,194
  Trophy Points: 280
  Mpe nafasi nyingine lakini usiruhusu muda mrefu kupita kabla ya ndoa. Kila la heri.
   
 20. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,857
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  dada sugua goti.kila mtu na bahati yake. yawezekana huyo ni wako ndo mana kazunguka kote huko lakin bdo karud kwako! all da best mdada. . . .
   
Loading...